Je kuna haja ya kukaa nyumbani kusubiri kuhesabiwa?

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
1,231
Wana JF, hivi mnafikiri serikali kama hii itafanya jambo la maana muhimu baada ya sensa katika maendeleo au tutabaki kujulikana idadi tu?.
 
Hakuna haja,kwanza wanasema sensa ni kwa manufaa ya govt,sii umma wa watanzania.mfano kukataa maoni ya waislam
 
Mkuu, uelewe kuwa sensa inafanyika kila baada ya miaka 10, tena kama bajeti inaruhusu. Uelewe kuwa serikali hii imebakiza miaka mitatu kuondoka, tena iwapo haitatokea dharura uchaguzi ukafanyika kabla. Sasa kama unadhani sensa hii ni kwa ajili ya serikali hii, basi sidhani kama umetumia muda wako kufikiri kabla. Kinadharia, kama haitatokea dharura, idadi hiyo ya watu katika sensa hii inaweza kutumika katika serikali tatu tofauti!
 
Tusubiri serikali makini ndo tuhesabiwe lakini si sasa
 
Mkuu, uelewe kuwa sensa inafanyika kila baada ya miaka 10, tena kama bajeti inaruhusu. Uelewe kuwa serikali hii imebakiza miaka mitatu kuondoka, tena iwapo haitatokea dharura uchaguzi ukafanyika kabla. Sasa kama unadhani sensa hii ni kwa ajili ya serikali hii, basi sidhani kama umetumia muda wako kufikiri kabla. Kinadharia, kama haitatokea dharura, idadi hiyo ya watu katika sensa hii inaweza kutumika katika serikali tatu tofauti!

nillikuwa natamani kila mtu apitie huu uzi wako
 
Mkuu, uelewe kuwa sensa inafanyika kila baada ya miaka 10, tena kama bajeti inaruhusu. Uelewe kuwa serikali hii imebakiza miaka mitatu kuondoka, tena iwapo haitatokea dharura uchaguzi ukafanyika kabla. Sasa kama unadhani sensa hii ni kwa ajili ya serikali hii, basi sidhani kama umetumia muda wako kufikiri kabla. Kinadharia, kama haitatokea dharura, idadi hiyo ya watu katika sensa hii inaweza kutumika katika serikali tatu tofauti!

Kutumia ktk kufanya mambo gani ya maana kuongeza bajeti na kuomba misaada inayonufaisha mafisadi au wananchi ambao wamekata tamaa? Ngoja tusubiri kuona namna sensa itakavyotumika kuleta maendeleo
 
Hakuna haja ni kutaka kujikweza kwa serikali yetu, utaratibu wote umejaa ubabaishaji mtupu, nadhani hawakujipanga kwa zoezi hili.
 
Wana JF, hivi mnafikiri serikali kama hii itafanya jambo la maana muhimu baada ya sensa katika maendeleo au tutabaki kujulikana idadi tu?

Sensa ina lengo kubwa la kupata takwimu juu ya watu wote kuhusu hali ya kiuchumi, kijamii na kidemografia ambapo ktk takwimu za elimu itasaidia serikali kujua kiwango cha elimu kwa watu wote km kusoma na kuandika, level ya elimu. Pia takwimu za Umri zitasaidia kujua umri wa watoto wanaostahili kwenda shule yaan miaka 4 na zaid na ambao bado pia ambao wameshafikisha umri wa kwenda shule ila hawaja anza kusoma, Pia takwimu za kiuchumi zinalenga kujua hali ya kaz na ajira kwa watu wenye umri kuanzia miaka 5 ambapo watajua walio ajiriwa na wasio ajiriwa YOTE HAYO ITASAIDIA KUPANGA SERA NA MIKAKATI YA MAENDELEO YA KIPINDI KIJACHO
 
NDIYO.Japo hakutakuwa na posho kwa usumbufu wa kukaa nyumbani bila feni wala kiyoyozi na viti vya kuzunguka(labda mpaka uende saluni au ofisini kama vipo)kama walivyopendelewa waheshimiwa kule mjengoni mpaka wanasinzia wakati wa vikao baada ya kupata moja baridi,moja moto na kuku wa kuchoma pale Chako ni Chako bar. Kama unabisha mwuulize Mheshimiwa ngumi ya jiwe atakuambia.Kumbuka tunatakiwa kuzitii mamlaka japo hatuna maarifa.
 
Back
Top Bottom