Je, kuna haja ya kufanyia vikao vya Bunge Dar...

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
ili kupunguza ajali kama hizi zilizofuatana na zilizotuchukulia wapendwa wetu? Kikazi nilikuwa nasafiri sana kwa mabasi na wakati mwingine na magari madogo. Siku zote nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana ninapokuwa safarini hasa ukitilia wingi wa ajali za barabarani Tanzania na kulikuwa na kosakosa nyingi sana, Mungu ashukuriwe. Je, mnafikiri umefika wakati wa kurudisha vikao vya bunge Dar au tuendelee kupoteza tuwapendao? Je kama vikao vikirudishwa Dar, jengo la Bunge liligharimu mabilioni ya pesa litatumika kwa shughuli gani?

Kifo cha Wangwe chatisha!

2008-07-29 14:21:06
Na Waandishi Wetu, Dodoma na Dar


Ajali iliyotokea jana mjini Dodoma na kumuua Mbunge wa Tarime Mheshimiwa Chacha Wangwe (CHADEMA), imeibua vitisho vya aina yake kwa baadhi ya wabunge ambao husafiri kwa magari yao hadi Mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kibunge.

Wakizungumza na mwandishi wa Alasiri kwa nyakati tofauti mjini Dodoma, baadhi ya wabunge wamesema kutokea kwa ajali hiyo ambayo imekuja siku chache tu baada ya ajali nyingine iliyoua watu wawili akiwemo mtoto wa Mbunge Saverina Mwijage aliyekuwa ametoka kutambulishwa ndani ya Ukumbi wa Bunge, kumewapa hofu kubwa kuwa pengine, nao wako hatarini.

``Kwakweli ajali hii imetutisha... ni kifo cha ghafla mno na kwakweli, binafsi nimeingiwa na hofu kubwa juu ya ajali hizi zinazopoteza wapendwa wetu kila kukicha,`` amesema Mbunge mmoja wa kambi ya upinzani.

Naye mbunge mmoja wa chama tawala CCM, amesema kama walivyo wabunge wengine wote, naye amesikitishwa mno na kifo hicho.

Aidha, akasema namna mwenzao huyo alivyokumbwa na ajali mbaya, imempa hofu kubwa moyoni.

``Ni ajali mbaya sana... namna gari lilivyoharibika, ni wazi kwamba haikuwa ajali ndogo.

Binafsi, kwa moyo wa kibinadamu, najikuta nami nikiingiwa na woga kwa sababu kila siku huwa safarini wakati wa utendaji wa kazi zetu hizi za kuwawakilisha wananchi,`` akasema mbunge huyo wa CCM.

Mheshimiwa Wangwe alifariki dunia jana baada ya gari yake aliyokuwa akiliendesha mwenyewe aina ya Toyota Corolla, namba za usajili T 865 AMR kupata ajali katika eneo la Pandambili wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Omary Mganga, marehemu Wangwe alifariki dunia papohapo, mishale ya saa 2:15 usiku, huku mwenzie aliyekuwa akisafiri naye, Bw. Deus Mallya, akinusurika na ndie aliyefikisha taarifa hizo polisi.

Gari hilo liliparamia mti na kupinduka mara kadhaa kabla ya kusababisha kifo cha Mheshimiwa Wangwe.

Kwa mujibu wa Spika Samuel Sitta, marehemu Wangwe alimuaga kuwa anakwenda kuwahi mazishi ya mwanasiasa `veterani` Bhoke Munanka, ambaye mwili wake unatarajiwa kuagwa leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kuzikwa.

Aidha, leo asubuhi, Spika Sitta ametoa tamko rasmi la kifo cha mheshimiwa Wangwe na kulifanya Bunge lizizime kwa majonzi makubwa.

Wakati akitoa taarifa hizo za huzuni, yeye binafsi (Spika Sitta) alishindwa kujizua na kuonekana wazi namna alivyoguswa kiasi cha kumwaga chozi, hali ambayo pia iliwakuta waheshimiwa wabunge wengi ndani ya ukumbi wa Bunge.

Katika kutoa tamko la kuthibitisha kifo hicho cha Mhe. Wangwe, Spika Sitta pia akatangaza kusitishwa kwa shughuli za Bunge hadi baadaye mchana ili aweze kutoa maelezo zaidi ya taratibu zitakazofuata.

Akieleza zaidi, Spika Sitta amesema majeruhi aliyesalimika katika ajali hiyo, Bw. Mallya, ambaye ni mfanyabiashara Jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na tayari Ofisi ya Spika imeishakwenda kumuona na kuwasiliana naye.

Aidha, baada ya kutangaza hayo bungeni, mheshimiwa Sitta alitoa pole kwa familia ya marehemu, wananchi wa wilayani Tarime hususan wapigakura wake, Chama chake, waheshimiwa wabunge na watu wote walioguswa na msiba huo.

Katika kuahirisha shughuli za Bunge, Spika akatumia kanuni ya Bunge ya 149 aliyoinukuu kuwa: ``Endapo mbunge atafariki wakati shughuli za Bunge zikiendelea, Spika analazimika kuahirisha shughuli za bunge siku hiyo.``

Taarifa nyingine zinasema kuwa, mwili wa marehemu Wangwe utaagwa leo mjini Dodoma kabla ya taratibu nyingine, ikiwa ni pamoja na kuusafirisha kwenda Tarime zitafuatia.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa amesema chama chake kitatoa taarifa ya mipango ya mazishi baadaye leo baada ya tamko la Spika bungeni kuhusiana na kifo hicho.

Naye Mwenyekiti wa UDP Mheshimiwa Jaoh Cheyo amesema kifo hicho ni pengo kuwa sio tu kwa chama cheke cha CHADEMA, bali pia kwa kambi nzima ya upinzani.

SOURCE: Alasiri
 
No .. viendelee kuwa dom .. maana infrastructure hairuhusu ... au watengeneza fly over brigdes .... maana barabara zote zitafungwa sisi walala hoi tutashindwa kufanya shughuli zetu ...

Wakienda tu airport .. au kuwa na ziara kidogo tu ... basi tunakanyaga kwa miguu mpaka majumbani kwetu ... usafiri unakuwa shida maana foleni haisemeki

Ukisikia kafa mtu basi Mungu ndivyo alivyopanga ... tuacheni bwana ..
 
Vibaki huko huko Dom na watakaoendelea kufanya ufisadi wafe waishe kije kizazi kipya safi! Maana mahala pengine Mungu anajaribu kuwapunguza wengine ili wasiendelee kuharibu kanchi ketu.
Ole wao wanaodhani ni utani kwa kuishi wakifisadi nchi yetu. Watakipata.
 
Sioni sababu ya kufanya vikao Dodoma kama mpango wa kuhamia Dodoma haupo_Ofisi za serikali zote zinajengwa Dar!! Kweli ni hatari hasa barabara ya Dodoma- Morogoro. Ni gharama pia ku shuttle between Dodoma na Dar wakati wa vikao.
 
bunge hata likifanywa dar , nafikiri wabunge watatakiwa kufanya safari mara nyingi za kwenda na kurudi majimboni kwao.

kwa maana hiyo suala la ajali kama lipo litaendelea kubaki pale pale vikao vya bunge vikifanyika dodoma au dar.
 
..........Ila ninavyojua wengi wao hasa wanawake huwa wana madereva ambayo nafikiria ni njia nzuri pia..maana wana mambo mengi...na majukumu memngi pia...na hawana uzoefu(wengi wao)kuendesha safari ndefu na hasa usiku.....
 
Hivi ajali za akina pangu pakavu huko maporini kwetu mbona hatusemi? Mabasi yanabinuka kila siku na kumaliza walalahoi kibao kila siku,je na wao tuwahamishie Dar?

Ni mipango ya Mungu,hata Dar kila siku ajali zipo.
 
Back
Top Bottom