JE KUNA HAJA YA KUENDELEA NA MFUMO WA VYAMA VINGI NCHINI TANZANIA?
Na Kilawa the Iron
La hasha!
Mh. John Pombe Magufuli Rais wa jamhuri ya Muungano Tanzania alipokuwa akihutubia katika sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM) zilizofanyika mkoani Singida aliibuwa maswali mengi na mjadala mkubwa kwa wananchi hasa wa vyama vya upinzani na wasomi wa kada
mbalimbali.
Kauli nyingi alizotumia Mh Dr. Magufuli katika maazimisho hayo ziliibuwa mjadala mzito katika mitandao ya kijamii, vijana wengi wa upinzani na wasomi wengi walikosoa vikali kauli za mh Rais lakin pia wapo waliompongeza kwa kauli zake alizozitumia.
Yawezekana Rais alitumia kauli hizo kwa nia njema, au kwa kutokutambua faida na madhara yake katika jamii au alitumia kauli hizo kwa furaha za ushindi aliopewa na kuwa Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano Tanzania.
Moja ya kauli iliyoonekana inamkanganyiko mkubwa na ya kidikteta ni hii hapa nanukuu "Hakuna mtawala yeyote anayependa kutawaliwa, na bahati mbaya atawaliwe na vyama vya hovyo hovyo, vya ajabu ajabu"
Wananchi wengi, wasomi na wasio wasomi walijiuliza kupitia mitandao ya kijamii na hata kwenye vijiwe mbalimbali nilivyopita. walijiuliza
Je kuna haja gani ya kuita nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi?
Je Rais John Pombe Magufuli amesahau kwamba yeye mwenyewe alisema atakuwa Rais wa wote?
Lakini katika yote hayo wapo walioongeza na kijadili zaidi juu ya sakata la Zanzibar, watu hawa waliendelea kusema yawezekana matokea ya Zanzibar yaliyofutwa na Bwana Jecha ambaye ndiye mwenyekiti wa ZEC yalipangwa na Viongozi wa juu wa CCM kwa kuwa hawapo tayari kutawaliwa. Wakaongeza kwa kusema Mh Rais atangaze tu hadharani kuwa mfumo wa vyama vingi umefutwa ili ijulikane moja badala ya nyingi.
Mh Rais hakuzungumza maneno hayo tu juu yaliyoibua mjadala pia alisema
"Mimi Rais, lakini ni Rais niliyechaguliwa na chama cha mapinduzi.......... Ambayo ukweli serikali hii nimepewa na chama cha mapinduzi....... Kisingekuwa chama cha mapinduzi leo nisingekuwa Rais "
Hakuishia hapo aliongeza kwa kusema"Mimi mh m/kiti nakuhakikishia serikali ninayoiongoza itaendelea kuwa nakuonesha Mshikamano mkubwa na Chama Cha Mapinduzi, Hakuna serikali kama hakuna CCM"
Hapa ndipo palipowadhihirishia wananchi kuwa upinzani si kitu ndani ya Tanzania, na ndio maana wabunge wa upinzani wankamatwa hovyohovyo na polisi, wanachama na baadhi ya viongozi wa upinzani kupigwa, kuumizwa na hata kuuwawa.
Katika haya yote Mh Rais ameonekana kwamba ana dhamira ya kumaliza upinzani na sio kuimarisha demokrasia, kitendo cha kusema serikali ya awamu yake itashikamana na CCM inaonesha kuwa upande wa upinzani hawana nafasi katika nchi yao inayojinasibu kuwa ni ya kidemokrasia.
Anaposema "hakuna serikali kama hakuna CCM"sasa kuna haja gani ya kufanya uchaguzi na kupoteza mabilion ya pesa ilihali wao wanajua watatawala milele. Wanafanya uchaguzi kuridhisha mataifa ya kibepari aua kuridhisha wananchi au?
Kuna haja kubwa kutengeneza katiba mpya ya nchi yetu ili maswala ya kidemkrasia yapewe nafasi badala ya kupuuzwa kama chama tawala kinavyofanya.
Msema kweli ni adui wa wapenda maovu