Je, Kuna haja ya kuendelea na mbio za mwenge wa Uhuru?

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,572
9,809
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike na hata nje ya mipaka ya nchi yetu, ulete matumaini mahala pasipo na matumaini, faraja palipo na huzuni, upendo palipo na chuki, heshima palipo na dharau" - Forojo Ganze

Kwa kuirejea na kuinukuu kauli hii ya mganga maarufu hapo juu akiwa na wenzake, ndiyo tulipata sababu hasa ya kuanza kutumia mwenge wa Uhuru kama alama mojswapo ya taifa la Tanganyika hatimaye kuanza kukimbizwa kwa mbio za mwenge zilizolirithiwa baadaye na JMT.

Naandika mada hii pasipo kujali kuzidi kuwepo kwa alama hii ya taifa, bali najielekeza zaidi kwa haja ya uwepo wa mbio za Uhuru kila mwaka. Tuliona ya kwamba mbio hizi zilisitishwa kutoka pale zilipoasisiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2020 kutokana na tishio la janga la ugonjwa wa Covid 19.

Kwa hakika sina kumbukumbu kuhusu uwepo wa mbio hizi kipindi cha vita vya Kagera, na hata kama zilikuwepo inaonyesha dhahiri nchi ilidhamiria na kimaanisha kuhusu uwepo wa mbio hizi. Mwaka huu tunafikia miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Je, Sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mbio hizi bado zipo? Je! Kwa kupitia tathimini ya jumla tunaweza kuthibitisha tija ya kuzidi kuendelea nazo ama kuachana nazo! Je! Umefika muda sahihi wa kufanya mijadala ya kitaifa ili tuweze kutambua hatma ya mbio hizi?
 
Wewe jamaa! Acha kuwakumbusha bhana! Walikuwa wameshasahau!! Ona sasa!! Wiki ijayo tu utashangaa wanaleta zile barua zao za kutulazimisha kuchangia!

Cha kushukuru Corona bado yupo, hivyo watajisikia aibu. Ila natamani hizi mbio zingefutwa tu! Maana hazina faida wala tija yoyote ile kwa nchi yetu. Zaidi tu zinahamasisha vitendo vya ngono zembe na usumbufu tu kwa raia na watendaji wa serikali.
 
Hii ndio Legacy ya jiwe inatakiwa kuendelezwa. Ya kuzitelekeza hizi mbio.
 
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike na hata nje ya mipaka ya nchi yetu, ulete matumaini mahala pasipo na matumaini, faraja palipo na huzuni, upendo palipo na chuki, heshima palipo na dharau" - Forojo Ganze

Kwa kuirejea na kuinukuu kauli hii ya mganga maarufu hapo juu akiwa na wenzake, ndiyo tulipata sababu hasa ya kuanza kutumia mwenge wa Uhuru kama alama mojswapo ya taifa la Tanganyika hatimaye kuanza kukimbizwa kwa mbio za mwenge zilizolirithiwa baadaye na JMT.

Naandika mada hii pasipo kujali kuzidi kuwepo kwa alama hii ya taifa, bali najielekeza zaidi kwa haja ya uwepo wa mbio za Uhuru kila mwaka. Tuliona ya kwamba mbio hizi zilisitishwa kutoka pale zilipoasisiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2020 kutokana na tishio la janga la ugonjwa wa Covid 19.

Kwa hakika sina kumbukumbu kuhusu uwepo wa mbio hizi kipindi cha vita vya Kagera, na hata kama zilikuwepo inaonyesha dhahiri nchi ilidhamiria na kimaanisha kuhusu uwepo wa mbio hizi. Mwaka huu tunafikia miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Je, Sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mbio hizi bado zipo? Je! Kwa kupitia tathimini ya jumla tunaweza kuthibitisha tija ya kuzidi kuendelea nazo ama kuachana nazo! Je! Umefika muda sahihi wa kufanya mijadala ya kitaifa ili tuweze kutambua hatma ya mbio hizi?
Mwenye ufute hauna faida yoyote
 
Lakini tukumbuke hii ni nyenzo na zana muhimu sana itumiwayo na CCM kuwapumbaza Watanzania wengi wasiojielewa hasa waishio vijijini. Wewe subiri kidogo na utaona baada ya muda watakuja kwa kasi na kuanza kuhamasisha mbio zianze tena kwa kisingizio cha kutaka kuwaenzi waasisi wa muungano na mapinduzi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom