Je, Kuna Haja Ya Kubadili Mfumo Wa Elimu Yetu Tanzania

bmk

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
571
857
Habari zenyu!

Wiki kadhaa zilizopita, tulimsikia mbunge mmoja bungeni akizungumzia mstakabali wa elimu yetu Tanzania, Sote tunafahamu kuwa Elimu yetu inatumia miaka mingi mpaka kupata ajira ama kujiajiri. Kwa mfano:

Elimu ya chekechea: Mwaka 1
Elimu ya msingi: Miaka 7
Elimu ya sekondari: Miaka 4
Elimu ya sekondari juu: Miaka 2
Elimu ya chuo kikuu: Miaka 3

Ukijimlisha ni miaka 15 jumlisha na miaka yako yumkini ni miaka 5. Utakuta unamaliza ukiwa na miaka 20 bado hujaanza kutafuta kazi uipate.Kumbuka maisha hapo ndo yameanza misukosuko ya mabadiliko ya kimwili na kujitegemea ndo wakati wake.

Na katika yale tujifunzayo mengi hujirudia kwa mfano uliyosoma olevel ndo yaleyale utayosoma alevel tofauti ni kwamba alevel utaingia deep sana.
JE, HATUONI HAPO NI KUPOTEZA MDA?

Kingine, Kadiri miaka inavyoongezeka ndivyo idadi ya watu huongezeka hivyo kupelekea kuwa na watu wengi waliosoma ili hali ajira ni ndogo hasa serikalini.
JE, HATUONI KUNA HAJA YA SERIKALI KUBADILI MFUMO WA ELIMU NA KUINGIZIA SOMO LA KUJITEGEMEA KAMA MSINGI WA MTANZANIA KUJIANDAA KUJITEGEMEA?

Wakati wa mwalimu, alijenga vyuo vingi vya VETA, Vilitoa watu wengi wenye ujuzi wa kujiajiri na kuajri wengine. JE, SERIKALI HAIONI UMUHIMU WA KUREJESHA KWA KASI VYUO HIVYO, AMBAVYO VITATENGENEZA WASOMI WALIONA UJUZI WA VITENDO NA SIYO UJUZI WA DARASANI?


86c2272d1e8569ad6bbaaf565c9852b9.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom