Je kuna haja gani ya kuwa nawakuu wa mikoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kuna haja gani ya kuwa nawakuu wa mikoa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitalolo, Aug 25, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nimeshuhudia baadhi ya wabunge kuwa ni wakuu wa mikoa tena mbali na mikoa ya majimbo yao.
  Kama hili linawezekana je kwanini tusiondoe hiki cheo cha wakuu wa mikoa na mmbu wa endeo husika ndio awe mkuu wa mkoa husika, kwa fikra zangu kwakuwa mbunge ni mtu wa kuchaguliwa na wananchi na kwakuwa kwa kipindi kirefu kunakuwa hakuna vikao vya bunge na kwakuwa tuna pia wakuu wa wilaya wanaoweza kukaimu nafasi ya mkuu wa mkoa kipindi mkuu wa mkoa ambaye pia ni mbunge anaweza kuwa kwenye majukumu mengine kama vikao vya bunge na vikao vya kamati za bunge.
  Na kwakuwa hili limekwishaonekana kuwezekana kwa baadhi ya bunge kuwa pia wakuu wa mikoa. je hatuoni kuna haja sasa ya kukifuta hicho kiti cha mkuu wa mkoa na akawepo mmbunge ambaye ndiye mkuu wa mkoa?.

  kwakufanya hivi sio tu tutaweza kuokoa baadhi ya pesa kama mshahara wa mkuu wa mkoa, gari la mkuu wa mkoa ambapo mbunge kwa kutumia mshahara wake wa ubunge atakuwa akikitumikia pia cheo cha mkuu wa mkoa In a reflex manner lakini pia atatumia gari hilo hilo la ubunge kutumikia mkoa na pia italeta changamoto ya uwajibikaji kwani mkuu wa mkoa ambaye pia ni mbunge wa kwa kuchaguliwa na wananchi atatumia rasilimali za mkoa na kujitahidi kuleta maendeleo ya mkoa kwa leo la kusaka kura tena kwa kipindi kijacho.
  Pia ofisi ya mbunge haitakuwepo kwani tayari tuna ofisi ya mkuu wa mkoa hivyo ataitumi kwa shughuli za mkoa na bunge unafiki ni kiasi gani tunaweza kukiserve kwa hili.

  Kitu kingine kitakachoangaliwa ili kumpunguzia mkuu wa mkoa ambaye pia ni mmbunge majukumu na kumpa wakati wa kuutumikia mkoa ni kwamba kunakuwa na sheria inayosema mbunge anayetoka katika jimbo ambalo ndio liko mkoani moja kwa moja ndiye anayekuwa mkuu wa mkoa na kwasababu hiyo basi hatachaguliwa tena kwenye kamati za bunge. ili kumpa muda wa kufanya shughuli za mkoa [pia kwakuwa tunaamini wabunge wengi tu wana uwezo kuwatoa wabunge kwa idadi ya mkoa hakuta athiri kamati za bunge.
  kwa mfano mkoa waa Arusha una majimbo mengi ya uchaguzi inkuwa wazi Jimbo la Arusha mjini ndilo litakalotoa mkuu wa mkoa.Changamoto itatokea kwenye baadhi ya mokoa kama Dar kila jimbo litataka kutoa mkuu wa mkoa basi kuundwe utaratibu kwa majimbo kama haya lakini pia inawezwa kuamuliwa kuwa jimbo flani kwa mkoa kama Dar ndilo litakalokuwa linatoa mkuu wa MKoa

  Tatizo la nchi yetu ni vyeo vya kulipana fadhila yaani kunaeza hata kubadili wilaya kuwa mkoa ili tu kuanzisha cheo cha mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa wapya kwa lengo la fulani asije kunilaumu kuwa sikumpa uongozi.

  NARUHUSU MAONI NA USHAURI PIA KUNIKOSOA PALE KWA LENGO LA KUJENGA PALE AMBAPO UNAFIKIRI SIO SAWA KWA HILI LENGO NI KUPUNGUZA MLOLONGO WA VYEO AMBAVYO MWISHO WA SIKU NI MZIGO WA WANANNCHI NA UFANISI UNAKUWA MDOGO. PIA KUOKOA FEDHA AMBAZO ZINGETUKA KWENYE SHUGHULI NYINGINE ZA KIMAENDELEO.

  NAOMBA KUTOA HOJA
   
 2. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Hapa mkuu ni kupendekeza wakati wa kutoa maoni ya katiba hiki kipengele kinachompa rais mamlaka ya kuteua ma-rc na ma-dc kiondolewe,nakupongeza kwa mchango wako
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa mkoa ni part ya serikali alafu tena huyo huyo anakua mbunge na kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali sa hapo wapi na wapi mtu huwezi simamia serikali na vile vile ukawa part of the government yaani bongo bana i hope akina warioba wanajua kuhusu hili swala
   
 4. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ukiangalia karibu kila mkoa kuna majimbo ya uchaguzi zaidi ya moja hivyo mmoja kati ya wabunge kutoka kwenye mkoa anakuwa sehemu ya serekali kwamaana ya kuwa mkuu wa mkoa hivyo kama ni kuiwajibisha serekali basi wabunge walibakia katika mkoa na wabunge wa mikoa mingingine kwamaana ya majimbo wataiwajibisha tu serekali.
  Na pili ikiwa mkuu wa mkoa ambaye ni mbunge anachaguliwa na wanainchi uwajibikaji wake utakuwa kwa wananchi zaidi kuliko kwenye serekali.
  Tatu lengo ni kuondoa Mtu mmoja Ambaye ana act tu kama mkuu wa mkoa na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji wa serekali
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Ili kupinguza vyeo hata kwenye vyama, awepo na mwenyekiti tu.
  Kwa mfano katika CHADEMA Mwenyekiti anatosha kufanya shughuli zote za chama.
  Hii kuwa na katibu mara uenezi ni kupeana vyeo tu.
   
Loading...