Je, kuna dawa ya kusafisha na kutibu meno yaliyooza?

JIWE2

Senior Member
Sep 17, 2010
125
18
Meno yangu mengi yana rangi ya kahawia na baadhi yametoboka toboka. Ingawa najitahidi kudumisha usafi wa kinywa kwa kutumia dawa za kawaida za meno inaelekea yanaendelea kutoboka, kumeguka na kuvunjika.

Naomba yeyote mwenye ujuzi anisaidie kujua dawa itakayoweza kutakatisha na kutibu meno yangu. Natanguliza shukrani.
 
Pole sana ndugu. Nashauri umwone Dentist akupe ushauri wa kitabibu. Ikishindikana tumia dawa inayoitwa Forever Bright tooth gel. Inapatikana kwa wasmbazaji wote wa Forever Living Products.
 
Pole sana jiwe2 kwanza kabisa jitahidi na usafi zaidi kwa dawa nzuri zaidi na hata ukichoka vipi usilale bila kupiga mswaki.

pili kuna matibabu ya meno kusafisha jino hadi jino kama limeoza kabisa dokta atalingoa kama bado au limeharibika kidogo atasafisha na kuziba.

Kwa yale yaliyoharibika kabisa ni vema utoe tu kwani si afya kuwa na meno mabovu kinywani nishashuhudia mtu kupata kansa ya kinywa na nilisononeka sana na ukumbuke kuna meno ya bandia km jino ulilongoa lipo mbele.

baada ya tiba utashauriwa kufika hospitali baada ya muda fulani either miezi 3 au sita.ukifata maelekezo ytakuwa na meno yenye afya nzuri tu.

Plz usiende hospitali za mitaani. Chagua hosp moja kubwa ya binafsi hata ya serikali!ukishatibiwa ni pm nikutajie dawa zingine za asili.
 
Tafadhali nijulishe streight hao wasambazaji au wauzaji wanapatikana wapi tanzania
 
hii kitu kama nilishaisoma humu jf, hata hivyo baking soda inayotumika katika mandaz nk, tumia kublash kwa mswaki. kama ni rangi sana fanya x2 kwa siku, meno yatakuwa white kama ya mtoto ila haitibu inasafisha. ila uwe mvumilivu ina ladha mbaya.
 
Dedii,ni baking soda?au baking powder?na je ni kwel meno yanakua meupe?plz reply wangu bac
 
Jamani nisaidien wapendwa meno yangu yameoza mno

Pole, ila nna tatzo la meno km lako lkn mi hayajatoboka sana ni kama ma2.Fata ivi
Tumia iyo dawa ya forever living uiangalie kama itakusaidia koz iz dawa si unajua tena kwa mfano mim imenikataa kabisa na ikanibid nitumie dawa ya meno za GNLD ni ya maji.
Pili,piga mswaki vizuri na haswa ukimaliza kula chakula la usiku.

Tatu, acha kutumia vtu vya sukar kama biscut,na v2 vnavogandia ktk meno kama karanga,pia uspnde kula nyama ngumu,hakikisha imelainika ili kuepuka kuivutavuta na kutafunatafuna ili yasimeguke.

Then nenda ukayaweke risasi hospital(ukayazibe) yanayowezekana utakua poa tu ila mashart hayo yote yafate .
 
Unamkuta mtu ni kijana/msichana mzuri tu wa kuvutia cha kushangaza ngoja acheke.
ha ha ha ha utadhani amengata mchanga.
 
Pole sana ndugu. Nashauri umwone Dentist akupe ushauri wa kitabibu. Ikishindikana tumia dawa inayoitwa Forever Bright tooth gel. Inapatikana kwa wasmbazaji wote wa Forever Living Products.

Mkuu dawa hii inauzwaje?. Inafanya kazi gani kwenye meno?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom