je kuna dalili zinazo fanana za mwanamke mjamzito?

Mghoshingwa

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
305
73
ni muda mfupi tu tuko kwenye ndoa na huwa tunashirikiana tendo effectivelly! juzi mke wangu aliona matone machache ya damu mithiri ya hedhi lakini muda wa hedhi ulishapita na alipata hedhi. Pia ananiambia mapigo ya moyo yanaenda sana mbio na anakosa nguvu. Tafadhali wadau naomba kufahamu ni kitu gani? je ni dalili za mimba? bado hatujaenda kupima bado coz ni siku kama ya tatu tangia dalili hizi zijitokeze.
 
chief yaweza kuwa mimba au siyo mimba .kwanini nasema yaweza kuwa siyo mimba? kuna matatizo ya kisaikologia mfano hofu ,wasiwasi, msongo wa mawazo yanazidinganya na kuzibadilisha tezi za endocrine zizalishe au kutoa homonia zinazosababisha mwili wa mwanamke kuwa na dalili kama anamimba kama ulizotaja
chamsingi ili kuhakiki kama anamimba unaweza
1)kwenda hospitali na kupima kama ni mimba au ni tatizo la kihomonia au ni magonjwa mengine kama infection na magonjwa ya ngono
2)kama unaona uvivu kwenda hospitali nenda hata pharmacy ukachukua kipimo kinachoitwa urinary preganancy test maelekezo jinsi ya kutumia utaelekezwa na mphamasia,doctor, au nurse anayeuza hapo pharmacy
 
Back
Top Bottom