Je, kuna athari zozote kiafya kwa kumeza makohozi?

al1983

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
328
373
Ningependa kufahamu iwapo mtu akiwa na mazoea ya kumeza makohozi anaweza kupata athari zozote kiafya. Na kama athari zipo ni zipi?
 
Mhhh... ngoja wataalam waje,

ila yanashibisha mda flani.

Sina hakika, labda kama una TB
 
Ndiyo
1.uchafu.
2.unameza vimelea vya magonjwa
Hakuna hatari yoyote kwani hata bacteria waliopo eneo hilo ni normal flora kwahiyo kama akihama kutoka kwenye koromeo kwenda tumboni atakufa kutokana na mazigira sio rafiki kwake kubuka tumboni kuna balaa la acid kali kuliko maelezo.labda kama mtu ana TB.
 
Alafu pia sio uchafu zile ni mucous
Hata ziitweje,bado ni uchafu kwa kuwa umekusanya vitu vingi,ukivimeza havikupi kirutubisho wala kukushibisha kwanini umeze?Umewahi kutema chini koozi ukaona linavyofanana???
Kama upo kwenye position ya kutema kwanini usiteme?
 
Hata ziitweje,bado ni uchafu kwa kuwa umekusanya vitu vingi,ukivimeza havikupi kirutubisho wala kukushibisha kwanini umeze?Umewahi kutema chini koozi ukaona linavyofanana???
Kama upo kwenye position ya kutema kwanini usiteme?
Kwanini uteme wakati unaweza kumeza na ukaepusha kusambaza magonjwa wakati tumbo lako linaweza kuwamaliza hao wadudu sio uchafu sema wewe unakinyaa tu
 
Fafanua kidogo mkuu
Kazi ya makohozi ni kusafisha mfumo wa hewa. Hivyo yanatengeneza kulingana na uhitaji. Na hivyo mengi sana huwa unayameza hata sa hivi unavyosoma hapa utakuwa umemeza 3/8 lita
 
Natumai jukwaa limejaa wataalam wa afya ya binadamu,

Msimu wa mafua huu, Nmejaribu TU kuwaza kwa sauti

Endapo nimebanwa na makohozi
(Yale mazito mazito ya tunayotemaga nje)
na nikaona mahala nilipo hayaruhusu kabisa kutema makohozi.

Nikaamua kulivuta puani lielekee Kwenye koromeo Kisha nikalimeza mpaka tumboni.

Ni athar gani kiafya naweza kupata?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom