Kakende
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 2,741
- 1,231
Ndugu zangu kuna aja ya wananchi kuwa waalendo kwa nchi yao katika mambo ya msingi. Kuna nchi ambazo zimefikia hatua ya kwenda kumshitaki jirani yake iwapo anaharibu miundombinu au kukwepa kodi, wanaona kukwepa kodi ni dhambi kubwa. Wenzetu wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kabisa kuwa kodi yake inafanya kazi kwa kupata huduma ya maji safi, umeme wa kuaminika, elimu safi na rahisi, na asikii kuna fisadi kaiba pesa za umma.
Hata katika nchi zetu masikini unaweza kuwa mzalendo hata kama huduma hazijawa nzuri sana lakini unaona kabisa kiongozi anafanya kazi kwa uhadirifu bila wizi, ukiwa na matumaini kuwa siku moja mtafika kwenye neema kama za wenzetu.
Mimi najiuliza kama kuna haja ya kupoteza muda wangu wa kutumia internet eti nipige kura Kilimanjaro na Ngorongoro vingie kwenye maajabu saba ya dunia. Hivi katika hali ya ufisadi kama huu ambao nikianza kuutaja nitakesha, watu wanaiba Twiga na kuwasafirisha pamoja kwamba wana shingo ndefu lakini bado polisi na usalama wa taifa hawakuweza kukamata waarifu. Ukiangalia TANAPA, BOT nk wamejaa watoto wa vigogo. Hali ya elimu ni mbaya, kama huna pesa jiandae mwanao afaulu akiwa hajui kusoma
Nasita kupigia kura Kilimanjaro na Serengeti, nina wasiwasi kama watalii wakiongezeka na mimi mwananchi wa kawaida nitafaidika au zitaishia kwa wenye nchi kula kuku, kuendesha magari ya kifahari na kusafiri kila siku kwenda ulaya kutanua. Inawezekana na mimi nikafaidika?