Je, kulikuwa na ulazima wa kuwadai Acacia?

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,730
2,388
Kiuhalisia, kiasi tunachokidai ni kikubwa sana, haijalishi kampuni hyo inapata faida kiasi gani. Ila hela ikishaingia mfukoni, tena toka miaka mingi iliyopita, ukija kuidai leo, ni ngumu sana kulipwa. Yawezekana kweli ni haki yetu kabisa, ila mfumo ulikosewa toka mwanzo, so kufukua makaburi hakutasaidia kwa sasa.

Kwa sasa wamesema hawana hiyo hela ya kulipa, na hakuna anayejua hii ishu itaishaje. Na kwa kaliba ya mkuu, nadhani haitakuwa na mwisho mzuri, hasa kwa sababu kwamba, moja ana hasira by nature, na ya pili alishatuaminisha watanzania kwamba TUMESHINDA na kubeza upinzani na wote waliokuwa wanaleta hoja hasi dhidi ya ishu nzima ya makinikia na mikataba ya madini.

Nadhani serikali ingetaka zaidi kuanza NEW TERMS na hawa jamaa bila kujali tulishaibiwa kiasi gani, ili kuanza kupata mapato stahiki na kwa wakati. Hii ni kwa sababu:

1. Uwezekano wa wao kulipa trilion zaidi ya 400 ni mdogo sana au haupo kabisa.

2. Wakiamua kususa na kuondoka watatuachia mashimo tu migodini ambayo kwa hali ya uchumi wetu wa sasa HATUWEZI kuendesha shughuli za uchimbaji kwa sababu hatuna vifaa vya kisasa.

Ingekuwa ni busara sn kukubali yaliyopita kuliko kuingia katika mgogoro mwingine ambao mwisho wake ni kama giza.

Ni bora tungewatumia hao tunaowaita "wabobezi wa sheri" kupitia upya mikataba ya madini, tungeangalia the best way kuachana nayo na kutengeneza upya sheria za madini na kuanza kufaidika kwa kiasi fulani.
 
Kisheria wakati hakuna madai tokea mwanzo miaka zaidi ya kumi hamna kitu na ndio maana wakatuahidi kutupa rushwa ,tukaridhia kiukweli hatuna kitu hapo .
 
Sasa yale makontena si walisema yana madini ya maana sana sasa ni wakati muafaka wa nasi tujue tumepata ngapi za ushuru huko! Maana naona hamuongelei tena hayo.
 
Mikurupuko na matambo ya mfalme wa ccm aibu na anguko lake nifedheh,sana hasa kwa yule mbunge aliyeharisha kwa kinywa bungeni,na kumpa Lisu kichambo.mkiambiwa ccm bungeni ni ukoma mnateka watu ! Sasa leo wanafiki semeni ndio yote kwa uzuzu wao ndioooo ! Na mfalme wenu aliwajua mlivyo vilaza kama yy na job description hakuwapeni ! .ccm imeuwa nchi kabisa.mlaaniwe na kila mwanadamu,viumbe vyote nchini,hata na mimea,kwakuifikisha nchi hapa ilipo.na madini yaliyopo ardhini yawalilieni kilio kitakacho watafuna hadi kizazi chenu cha saba,naiwe kwenu ccm wote,mlioshiriki dhambi hii.
 
Mkubwa bado anaulimbukeni na ushamba yaani hana tahadhari anaporopoka ila anapata kushangiliwa na mapopoma wa rangi ya kijani hadi unawaonea huruma
 
Back
Top Bottom