Je, kulikuwa na haja ya Polisi kufyatua risasi?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Polisi wapambana na wananchi kwa risasi

na Mkolo Kimenya
Tanzania Daima

POLISI wa Kituo cha Wazo Hill, jijini Dar es Salaam, jana walilazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya wakazi wa vijiji vya Chasimba, Wazo na Madala, ambao walifika eneo hilo kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Wananchi hao, ambao wana mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na Kiwanda cha Saruji Tanzania (TPCC), walifika katika kituo hicho baada ya kupata taarifa kuwa, Lowassa alikuwa afanye ziara kiwandani hapo.

Hata hivyo, Lowassa, ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mtambo mpya wa kiwanda hicho, hakufika na badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Batilda Burian.

Wakati waziri huyo akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho kinachozalisha saruji ya Twiga, ambao ndio wanaomiliki mtambo huo, ghafla risasi zilisikika, hali ambayo ilizusha mtafaruku na kuvuruga usikivu baada ya waandishi wa habari na baadhi ya watu kutimka kuelekea zilikosikika risasi hizo.

Risasi hizo zilifyatuliwa na askari polisi kutoka mbele ya kituo hicho.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia kundi la wanakijiji hao wakiwazomea polisi, huku wakiwarushia mawe, wakishinikiza kuonana na mgeni rasmi katika uzinduzi wa mtambo huo.

Wakazi wengine walisikika wakipaza sauti zao wakisema wanataka wenzao, waliodai kuwa walikamatwa na polisi awali na kufikishwa kituoni hapo, waachiwe haraka.

Polisi waliendelea kufyatua risasi hewani, lakini wakazi hao hawakuonekana kuogopa na zaidi waliendelea kulisogelea eneo la kituo, hali ambayo iliwafanya polisi waanze kuwatawanya kwa nguvu na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.

Sakata hilo lilidumu kwa muda, na polisi wakafanikiwa kuwatawanya watu hao, huku wananchi zaidi ya wanne wakitiwa mbaroni, wakiwemo wanawake wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kanali mstaafu, Fabian Massawe, ambaye alikuwepo katika hafla hiyo, alionyesha kusikitishwa na hali hiyo na akawataka wakazi hao kufuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yao.

“Kama wanaona hawakutendewa haki, ni vema waende polisi wachukue RB, kisha waende mahakamani, lakini sio kutumia njia za vurugu na vitu vingine vya namna hiyo,” alisema Massawe.

Massawe alionyesha kuwashangaa wananchi hao huku akidai kuwa wao ni wavamizi wa maeneo ambayo wanayalalamikia.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kunduchi, Wamula Maranda, aliyesema kuwa, kitendo cha wananchi hao ni vurugu zisizo na msingi, kwani ni wavamizi katika maeneo hayo.

“Hata nyumba hakuna katika hayo maeneo wanayodai kuwa ni ya kwao, wamevamia na hata mawe ya mipaka katika viwanja hivyo ambavyo vina wamiliki halali, wameyang’oa,” alisema.

Maranda alisisitiza kuwa, mara kadhaa amewasisitizia wananchi kufuata utaratibu katika kuwasilisha madai yao, lakini wamekuwa wakikaidi.

Aidha, mmoja wa wakazi hao, aliyejitambulisha kwa jina la Sheikh Lukindo Lyimo, alidai kuwa, walifika kituoni hapo kwa lengo la kutaka kuwaona wenzao ambao walikuwa wamekamatwa awali.

“Sisi tumefika hapa kwa lengo la kutaka kuwaona wenzetu watano ambao walikamatwa na si vinginevyo, lakini cha kushangaza, badala ya kusikilizwa, tunaanza kufukuzwa, na kama hivi unavyoona, vurugu tupu… kama tupo kwenye mapigano, na wengine wameshakamatwa na kuwekwa ndani, sasa hii ni haki kweli?” alihoji.

Alisema kwa sasa hawana makazi na wanaishi porini kutokana na kufukuzwa katika maeneo ambayo walikuwa wakiishi awali, kwa kuelezwa kuwa si wakazi halali wa maeneo hayo.

Hivi karibuni, Massawe alifanyiwa vurugu na wananchi hao, alipofika katika eneo hilo kwa lengo la kutatua mgogoro huo.

Siku kadhaa baadaye, Mahakama Kuu ilitoa amri ya muda, ikiwataka wananchi hao waendelee kuishi hapo hadi hapo kesi yao itakapoamriwa.
 
Hakuna yeyote kati yetu aliyezungumzia kuingia msituni, kubeba mapanga, mishale au mikuki ili kupambana na mafisadi wanaohujumu Watanzania na rasilimali zao. Ndio maana nilimshangaa sana Warioba alipokuja na kitisho cha umwagaji damu.

Tunachotaka kuona ni kwamba wale wote waliotumia nafasi zao kujitajirisha na kuwadhulumu Watanzania utajiri wao wafikishwe mahakamani bil kujali nafasi zao katika uongozi na wakionekana wana hatia basi wafilisiwe mali zao. Hilo ndilo tunalolitaka Watanzania wote wapenda maendeleo katika vyama vya upinzani, tusio na vyama na hata baadhi ya walio CCM.
 
Hongera kwa kazi nzuri Ng'wanakijiji! najua hii habari yote ni dalili njema ya kuipenda nchi yetu.

Naamini lengo la kila mmoja kwenye JF ni kuitakia mema Tanzania yetu... maana hakuna chuki binafsi kwa mtu yoyote hapa. ni kwamba walio madarakani kama wamejisahau waamke.. hawapo kwenye hizo nafasi kwa lengo la kuongeza mafuta kwenye vitambi. wanatakiwa kutukumbuka watanzania ambao dhamana yetu ndio imewaweka kwenye hizo nafasi. Pale Tabora boys secondary school kuna maneno mazuri sana ya mwalimu Nyerere yameandikwa ukutani... sikuyanakili lakini yanaongelea mtu aliyetumwa kutafuta chakula kwa ajili ya ndugu zake wakati wa njaa... lakini baada ya kukuta msosi akala na kuwasahau ndugu zake. nafikri waliopita hiyo shule wanayafahamu hayo maneno ya busara!
 
sasa mnasema dalili njema kwa watu kutaka kupigwa risasi na kuipenda nchi kwa kuwa mwanakijiji said so ? wakati watakaokuwa wanapigwa risasi ni hao wenzangu na mie (raia wema) huku mwanakijiji anakula kuku mrija ndani ya ze d-town ! ama kweli laana mbaya !
 
kama kupigana risasi wazee mie simo yaani sitaki hata kushuhurika kabsaaaaa, nitawaachia hao wengine ! mie kelele zangu JF kwenyewe nanga inapaa !
 
Hakuna yeyote kati yetu aliyezungumzia kuingia msituni, kubeba mapanga, mishale au mikuki ili kupambana na mafisadi wanaohujumu Watanzania na rasilimali zao. Ndio maana nilimshangaa sana Warioba alipokuja na kitisho cha umwagaji damu.

Tunachotaka kuona ni kwamba wale wote waliotumia nafasi zao kujitajirisha na kuwadhulumu Watanzania utajiri wao wafikishwe mahakamani bil kujali nafasi zao katika uongozi na wakionekana wana hatia basi wafilisiwe mali zao. Hilo ndilo tunalolitaka Watanzania wote wapenda maendeleo katika vyama vya upinzani, tusio na vyama na hata baadhi ya walio CCM.
hali kama hii inaweza kujitokeza sept mosi?
 
Safari hii Kamanda Lowassa lazima mahakama ya mafisadi imguse. Umeongea point sana hapo juu.
 
CCM na Polisi wao hawajui kuwa na sisi tuna damu, na sisi tnaumia na tukichoka kuumia hatutanyamaza...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom