Je kukondeana ni dalili ya kuwa na roho mbaya...................?

Inawezekana, ila wapo wengi tu ambao ni wembamba sana lakini kukondeana kwao hakutokani na roho mbaya walizonazo hata kidogo, ni nature tu ya maumbile yao! Tunao mifano ya watu wengi tu ambao jamii inawatambua kwa kuzijali familia zao na kuisaidia jamii iliyowazunguka ila miili imekataa kabisa kuongezeka. Mifano ni mingi ili nisingependa kuwataja hapa ili kuepusha mjadala mwingine.

Kwa upande wa akina dada ndo kabisa. Wengi wao wana roho nzuri na hawana ukatili lakini unakuta wamekondeana/wembamba either kwa kupenda (wanafanya diet), kumaintain figure(umbile), au tu ndivyo walivyozaliwa! Hivyo kwa kiasi jibu linaweza kuwa waliokondeana wana roho mbaya na kwa kiasi si wote wanaoangukia kwenye fungu la roho mbaya ...
Ni mtazamo tu ndugu yangu Mtambuzi .....

Mkuu nilishaweka angalizo kuhusu hilo ulilosema, unaweza kurudia kusoma hapo kwenye red.....................

Kama walivyo wagonjwa wengine, suala la udhaifu wa mwili hujitokeza sana kwa watu hawa, kwani pamoja na maradhi yanayoletwa na hisia chafu, kinga ya mwili hushuka sana pale miili inapohemkwa mara kwa mara. Ni rahisi kwa hali hiyo watu wenye roho mbaya kukondeana na kukosa afya imara. Hata hivyo sio kweli kwamba watu wote wenye afya mbovu inatokana na roho mbaya, hapana. Lakini kwa wale walio na roho mbaya, yaani kufikiri na tabia zenye kuzalisha nguvu hasi, nirahisi zaidi kwao kukosa afya bora, kama tulivyoona.
 
Mkuu Blaki Womani ebu tupatie status ya huyu mdogo wako (kwa wakati huu). Je ana roho mbaya au ilikuwa ni mambo ya utoto ktk 'foolish age'?

@Osoka ilikuwa utoto ameacha uchoyo na kulialia kwa sasa unakula kabla hajala so amenenepa lol
 
Nakubaliana na hiyo ya mihemko hasi kuleta shida za afya!
Lkn lakutokunenepa, kama ulivyosema mwenyewe back then juu ya stress na kunenepa na baadhi yetu tukakupinga. sasa hilo la kukondeana lina vichocheo vingine vingi tu na si rahisi kusema kipi kinashinda kipi. Labda hiyo roho mbaya imfanye owner asile vizuri na vya kutosha, afanye kazi sana (aunguze calories zaidi ya anazoingiza) yumkini atakonda. Lkn akiwa mlaji mzuri na mvivu (anakaa tu na kulalamika na kuonea wivu wanaofanya kazi na kufanikiwa), uwezekano mkubwa akawa bonge hata kama anaroho ya shetwani!
 
Asilimia kubwa ya wanawake wembamba wana roho mbaya.Kuna siku tullikaa familia wifi akauliza jamani mbona me senenepi karibu ningemwambia apunguze ghubu nikaguna tu.halafu huwa wana wivu sana cjui why?
 
Mi napinga kwa nguvu zote unless unambie unatafsiri ipi ya kukondeana? Kama mgonjwa wa HIV au kuwa na healhty figure????

Kuna watu unawaona jinsi walivyo kwa kuwa wako in control of their body including what they eat pamoja na exercises.

Na hawana mawazo hasi ila wanajipenda kupitiliza hence wana feel good seeing how shapely they could be
 
Mi napinga kwa nguvu zote unless unambie unatafsiri ipi ya kukondeana? Kama mgonjwa wa HIV au kuwa na healhty figure????

Kuna watu unawaona jinsi walivyo kwa kuwa wako in control of their body including what they eat pamoja na exercises.

Na hawana mawazo hasi ila wanajipenda kupitiliza hence wana feel good seeing how shapely they could be

Haki ya Mungu sikujua kwamba hujui kutofautisha kati ya wembamba na kukondeana
 
Siwezi kua assume bila wewe kufafanua...kwa kuwa kuna watu mtu unamuona poa tu wao wana define amekondeana. Ndio maana nikauliza kama mgonjwa wa HIV au TB?...nikiwa na maana mabega yamepanda juu?

Again hata kama anaonekana kama mgonjwa...who knows landa mgonjwa kweli...si unajua ugonjwa ni siri ya mtu...hivyo si fair kuwambia wagonjwa wana roho mbaya.


Maana kwa kiswahili rahisi mtu ukisema kakonda ina maana alikuwaga mnene before; am I right? Otherwise utasemaje kakonda. Ndio maana naona kunaweza kuwa na unyanyapaa kama si unyanyapaa basi nilivyoeleza mwanzo kuwa si kukonda ni health figure nilikuwa right.

Na kama unakubali kuwa kusema mtu amekonda unamaana amebadilika toka unene kwenda wembamba...je na tabia ya mtu ubadilika...nikiwa na maana alipokuwa mnene alikuwa na roho nzuri sasa amekuwa na roho mbaya ndio maana kakonda? Kukondeana ni changes...changes from unene to wembamba

Haki ya Mungu sikujua kwamba hujui kutofautisha kati ya wembamba na kukondeana
 
nitaongelea nitokako.

Mwanamke akishaolewa, akapata na watoto halafu akaendelea kuwa mwembamba moja kwa moja tunajua ana 'wivu, roho mbaya na fitina'

kwa hiyo mwanamke yeyote aliyeolewa na kuzaa lazima anenepe maana kazi ya mme ni kumlisha.

Hata mwanamme mwenye mke mwembamba sana huwa anaona aibu maana anaona kashindwa kumridhisha mkewe.
 
Mleta Mada anaweza kututhibitishia kuwa Stephen Wassira ana roho nzuri sana kuliko Mwl Nyerere?

Aliekuambia mwl Nyerere alikua amekoneana nani?Tuna matatizo ya kufikiri sana.Kwa mtazamo huu Mike Tyson amekondeana ukimlinganisha na marehem Umaga!!Kazi kwelikweli!
 
Hahahahahahahahaha
umenichekesha sana!

Kweli kabisaa! Tanzania nchi imekondeana kiuchumi kwa sababu ya wivu wetu dhidi ya UK na USA, pia hatujawasamehe wakoloni jinsi walivyotutenda hasa ktk ziwa nyasa, jamani tuwasamehe wakoloni na tuache roho mbaya na wivu dhidi ya mataifa yaliyoendelea, huenda tukifanya hivyo tanzania itanenepa kiuchumi.
 
nitaongelea nitokako.

Mwanamke akishaolewa, akapata na watoto halafu akaendelea kuwa mwembamba moja kwa moja tunajua ana 'wivu, roho mbaya na fitina'

kwa hiyo mwanamke yeyote aliyeolewa na kuzaa lazima anenepe maana kazi ya mme ni kumlisha.

Hata mwanamme mwenye mke mwembamba sana huwa anaona aibu maana anaona kashindwa kumridhisha mkewe.

sasa mbona wewe hunenepi? lol
na mchele magunia tele lol
 
Daaah! Hata ukishinda muda mrefu jukwaa la siasa lazima upate tatizo hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom