Je kukondeana ni dalili ya kuwa na roho mbaya...................? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kukondeana ni dalili ya kuwa na roho mbaya...................?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 22, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni jambo ambalo watu hulisema bila kujua maana yake. Unaweza kukuta mtu akisema “Ndio maana amekondeana, ana roho mbaya sana” Ukimuuliza ni kwa nini anahusisha kukondeana au afya mbaya na roho mbaya au kukosa upendo alikonako mtu, hataweza kukupa jibu sahihi. Lakini anajua kwamba kukondeana huwapata wenye roho mbaya.

  Kauli hiyo ina ukweli mkubwa wa kutosha. Watu ambao wanatengeneza nguvu hasi nyingi, hatimaye nguvu hizo huwarudia na kuwadhuru. Kwa sehemu kubwa madhara ya nguvu hizo huja kujitokeza kwenye miili yao. Mtu ambaye anaumwa mara kwa mara anaweza kuwa anaumwa tu kwa sababu nyingine, lakini pia anaweza kuwa anaumwa kutokana na nguvu hasi anazotengeneza. Nikisema nguvu hasi nina maana ya kufikiri na matendo ambayo yanamuumiza mwenye mawazo na matendo hayo, pia wale wanaomzunguka.
  Kwa mfano mtu asiyeweza kusamehe, mwenye visasi, mwenye kijicho, mpenda makuu, mshindani na mengine ya aina hiyo.

  Kuna watu ambao hutengeneza sana nguvu hasi kwa kufikiri kwao na tabia zao. Kwa kawaida nguvu hasi zinadhuru hisia na mwili wa mhusika. Kwa vipi? Hebu tutazame kushindwa kusamehe na kijicho.
  Mtu ambaye hawezikusamehe anajiweka mahali ambapo muda wote anakuwa kwenye hasira, hisia chungu na mikakati ya kulipa kisasi. Hii ni sawa na mtu ambaye ana kijicho, kwa mfano. Huyu naye, muda mwingi wa maisha yake atakuwa akiumia kwani kila wengine wakifanikiwa kwa chochote, atahisi vibaya. Kwa hiyo hisia zake zitakuwa zinachokozeka karibu muda wote.

  Kwa kawaida hisia zetu zinapochokozeka tunaiingiza miili yetu kwenye kuzalisha kemikali au homoni ambazo wakati huo hazihitajiwi. Kwa uzalishwaji huo wa kemikali zisizohitajika mwilini, tunaiumiza miili yetu kwa njia mbalimbali. Kemikali hizo hatimaye huanza kutuumiza na kutuletea maradhi mbalimbali miilini mwetu. Hili ni jambo ambalo limethibitishwa kitaalamu. Kuna maradhi zaidi ya kumi ambayo chanzo chake ni mihemko yetu, maradhi ambayo kitaalamu hufahamika kama Emotionally Induced Diseases.

  Haya ni pamoja na maumivu ya mwili, tumbo, kufunga choo, na mengine . Ndio maana wale watu wote wanaokwenda hospitalini wakiwa wanaumwa, ambao wanaambiwa vipimo havioneshi maradhi yoyote, ukiwachunguza utagundua kwamba wanakabiliwa na hofu, mashaka, visasi na matatizo mengine ya kihisia. Sisemi kwamba wote wanaopimwa na kuonekana hawana maradhi ndivyo walivyo, la hasha. Lakini wengi kati yao ndivyo walivyo. Hata wale wanaodaiwa kuwa na mapepo pia, utakuta ni wale wenye hisia chungu.
  Kwa sababu ya maumivu ya kimwili na yale ya kiakili unakuta watu hawa wakiwa dhaifu.

  Kama walivyo wagonjwa wengine, suala la udhaifu wa mwili hujitokeza sana kwa watu hawa, kwani pamoja na maradhi yanayoletwa na hisia chafu, kinga ya mwili hushuka sana pale miili inapohemkwa mara kwa mara. Ni rahisi kwa hali hiyo watu wenye roho mbaya kukondeana na kukosa afya imara.
  Hata hivyo sio kweli kwamba watu wote wenye afya mbovu inatokana na roho mbaya, hapana. Lakini kwa wale walio na roho mbaya, yaani kufikiri na tabia zenye kuzalisha nguvu hasi, nirahisi zaidi kwao kukosa afya bora, kama tulivyoona.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mimi naamini hivyo
  ni hali ya kukosa 'kuridhika'
  na sometimes 'wivu' kwa wengine
   
 3. c

  cheichei01 Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu zipo nyingi,kwa mfano ukiwa na mawazo hata ule nn mwili hauji,,smtymes hali ya ubongo wako ndo chanzo cha kila kitu...
   
 4. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi kama kuna kaukweli vile kuna wengine roho korosho muda wote manung'uniko......imenikumbusa tukiwa watoto mdogo wangu alikuwa kutwa kulilia vya wenzake akiona mwenzake anapewa chakula anataka apewe yeye wakati kula hawezi basi anabaki kulia na kukondeana basi mama anamwambia roho mbaya ndio maana hunenepe
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  dah,kumbe ndo sababu shost angu kadumaa. ana miaka 30 lakini ukimwona utadhani under 18. asante Mtambuzi kwa somo zuri
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. m

  markj JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  si kweli! kwa mana walioishikilia hii nchi wengi ni wanene na wanaroho mbaya sana sana sana! lakini wanao itetea hii nchi wengi ni wembamba na wanaroho safi sana sana sana! mpaka wanaamua kuitetea nchi yao.
  angalieni watu maarufu wote ambao wenye roho nzuri wengi ni wembamba, na wengi wanene ni roho mbaya mnooo.
  hata adamu na eva walikuwa wembamba! na manabii wengi walikuwa wembamba.
  dunia ya sasa wengi ni wanene kwa vya uharamu! pombe,ufisadi, kula vyakula kwa kudhulumu n.k
  anayekuwa mwembamba kwasababu ya mtu fulani, ujue anachukia yale mabaya yanayofanywa na mtu huyo.
  mifano tazameni nchi yenu na viongozi wake,celebrit wake n.k na pia angalienie viongozi wa nje wenye roho nzuri na maceleb wao na watu maarufu wenye roho safi.
   
 7. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisaa! Tanzania nchi imekondeana kiuchumi kwa sababu ya wivu wetu dhidi ya UK na USA, pia hatujawasamehe wakoloni jinsi walivyotutenda hasa ktk ziwa nyasa, jamani tuwasamehe wakoloni na tuache roho mbaya na wivu dhidi ya mataifa yaliyoendelea, huenda tukifanya hivyo tanzania itanenepa kiuchumi.
   
 8. peri

  peri JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  lol, mtambuzi umenipa somo ila umeniacha kwenye utata.
  Naomba nisiuseme, ngoja niufanyie kazi naamini nitapata majibu.
   
 9. N

  Neylu JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahahaaa.... Wembamba njooni mtuthibitishie jamani...!
   
 10. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ebu mkuu thibitisha hapo kwenye rangi ya violet!
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kabla hamjatoa kibali cha watu kunyanyapaliwa kumbukeni kuwa sio kila mwembamba ana roho mbaya
   
 12. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Inawezekana, ila wapo wengi tu ambao ni wembamba sana lakini kukondeana kwao hakutokani na roho mbaya walizonazo hata kidogo, ni nature tu ya maumbile yao! Tunao mifano ya watu wengi tu ambao jamii inawatambua kwa kuzijali familia zao na kuisaidia jamii iliyowazunguka ila miili imekataa kabisa kuongezeka. Mifano ni mingi ili nisingependa kuwataja hapa ili kuepusha mjadala mwingine.

  Kwa upande wa akina dada ndo kabisa. Wengi wao wana roho nzuri na hawana ukatili lakini unakuta wamekondeana/wembamba either kwa kupenda (wanafanya diet), kumaintain figure(umbile), au tu ndivyo walivyozaliwa! Hivyo kwa kiasi jibu linaweza kuwa waliokondeana wana roho mbaya na kwa kiasi si wote wanaoangukia kwenye fungu la roho mbaya ...
  Ni mtazamo tu ndugu yangu Mtambuzi .....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. k

  krungi Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi huwa nakukubali sana, lakini kwa hili nina mashaka kidogo, ingawa sijafanya utafiti wa kutosha. maana kuna watu ninaowafahamu fika kwamba wana roho nzuri ajabu lakini ni wembamba, na kuna ninaowafahamu fika kwamba wana roho mbaya mbaya lakini ni wanene mi nafikiri ni maumbile ya mtu na tabia ya mtu. mfano ni majambazi wangapi wanakesi za mauaji au wamehukumiwa kwa mauaji lakini ni wanene?
   
 14. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu Blaki Womani ebu tupatie status ya huyu mdogo wako (kwa wakati huu). Je ana roho mbaya au ilikuwa ni mambo ya utoto ktk 'foolish age'?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. m

  markj JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  soma vitabu vya dini, na sikiliza adidhi mbalimbali zinazoelezea sifa za manabiina wachamungu waliotangulia. usidumaze akili yako. mfano: wewe siumeiona picha ya yesu na unaiamini ndo ile jinsi alivyo, je?yesu alikuwa mnene, mama yake je? nawale waliokuwa wakimfuasi yesu je?na kuna aadhi ya vitabu vingi vinajaribu kukupa picha jinsi adam na eva walivyokuwa na naamini unaviamini je, vinawaonesha ni wanene? hacha iyo, kwenye familia na ukoo wenu ninaamini kabisa mwenye roho ya ajabu huko ni mnene tu!
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Bwana Boss,

  Kuna sababu nyengine pia au ni hizo tu?
   
 17. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu Krungi hapo kwenye red sijaelewa! Hivi kuna binadamu wameumbwa kuwa 'majambazi'?
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  ha ha haaa
  lol...
  nyiingi mno
  hizi ni few of them....lol
   
 19. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ....du!
  Kumbe ndo maana nimekonda eeeh!!
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Naafiki hoja moja kwa moja!

  Mtu aliye kukasirisha, kukuchukiza na ukazalisha hisia hasi (negative emotions) wakati mwingine baadaye unaweza hata kumuona ndani ya ufahamu wako kama taswira ya tukio zima vikijrudia...Tukio linalojirudia ndani ya ufahmu (moyoni) kwa muathirika linakuwa kama tukio pacha lililojengwa na hisia hasi na kuwa kama vimelea moyoni kama likiachwa na kukomaa ...(Emotional Parasite) ...

  Emotional Parasite ni hali ngeni kabisa, mgeni asiyetakiwa ndani yetu, ni adui asiyetakiwa ... ni kama ambukizi ... Ndani ya mwili wa ufahamu wa mtu ...!!

  Kinga ya mwili mara moja huhisi kuna adui mwilini (kwani hata ufahamu ni mwili wako).... na kuzaliwa kwa chembe nyeupe nyigi sana kwa jili ya kumshambulia adui ambaye ...hayuko kwenye damu ....!!

  Hii hudhoofisha kinga ya mwili kwani itatumia nguvu kubwa sana kumtafuta na kupambana na adui ambye hayuko kwenye damu ILA YUKO MOYONI ...kama kinyogo, kutosamehe, chuki mbalibali (Resentments)
  Mtambuzi nakubaliana bora Kusamehe (eliminations of emotional parasites) kwa gharama yeyote ... ili kurudisha kinga ya mwili ... uhai na afya ya mwili kwa pamoja!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...