Je kujua idadi ya kura za uraisi vituoni si haki ya kidemokrasia ya wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kujua idadi ya kura za uraisi vituoni si haki ya kidemokrasia ya wananchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by marshal, Nov 6, 2010.

 1. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa nasikiliza habari ya mwenyekiti wa ccm akiapa uwanja wa uhuru.
  Pointi moja aliyosema, "wananchi waliopiga kura walitimiza haki yao ya kidemokrasia".
  Swali langu kubwa je si haki ya kidemokrasia kwa wananchi kujua matokeo ya uraisi vituoni???kwa nini matokeo yasibandikwe vituoni baada ya kuhakikiwa na wasimamizi wa uchaguzi wakishirikiana na wagombea udiwani/pamoja na mawakala????
  Nahisi kuna mwanya mkubwa uliojikita hasa wakati wa kuhakiki matokeo.mfumo ulipo utaendelea kuleta vurugu na kuwanyima watu haki yao ya msingi vituoni kutambua wamemchagua nani!!sijapenda watu wanaojiita wasomi na wazee wenye busara kushindwa kuja mfumo wa wazi na usiokuwa na mashaka juu ya zoezi zima na kupiga kuhesabu na kutangaza matokeo ya kura.
  Sidhani kama tunahitaji ma professor kwa ajili ya kuja na mfumo ambao ni cost effective and feasible.
  Serikali itambue ina dhaman kubwa ya kulinda haki za kiraia za wanachi wake bila kujali itikadi za kichama,kidini wala kikabila. Mfumo wetu kwa sasa unalinda maslahi ya jamii moja na mfumo wake.hopeless leaders ambao wanalinda maslahi ya chama kimoja kuna siku wataifikisha nchi pabaya.natamani nyerere angekuwepo labda hata angewashauri maana naona sa hivi ccm na serikali haina washauri ambao nia yao ni kulinda maslahi ya nchi na wanchi wake.mafisi na mafisadi ndio wateule wa vyama na wanatumia umaskini kuwa ghiribu wananchi.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ni haki ya kila mpiga kura kujua idadi ya kura za rais zilizopigwa vituoni, lakini siyo haki ya mpiga kura kujua idadi ya kura za rais zilizochakachuliwa na usalama wa taifa (National Intelligence Security).
   
Loading...