Je, kujivunia kwetu Kiswahili kuna usalama?

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
763
Kila ninapotazama mbele –tuseme miaka 20 ijayo – kuhusiana na lugha yetu ya Kiswahili, naona tunakoelekea kama taifa si kuzuri sana.

Zamani ilizoeleka utani kwa watu wa kanda ya ziwa ambao kwa ujumla hupata tabu sana kutenganisha /l/ na /r/. Unaweza usijue kasema “kura” au “kula” – maana yote mawili anayatamka kwa kufanana.

Lakini hivi sasa kumezuka shida kubwa isiyohusiana na kabila, na inaendelea kukua hususan kutokana na kurahisika kwa mawasiliano – facebook, instagram, nk.

Kuna shida nyingi hivi sasa lakini mojawapo ni ya matumizi ya /a, e, i, o, u/ kwa upande mmoja na /h/ kwa upande wa pili. Yaani panapotakiwa /h/ anaiondoa; na isikotakiwa anaiweka.

Mfano, mtu anasema: “Ana ela yule” kumbe anamaanisha “Hana hela yule.”

Sasa Watu wanasema:

“apa” balala ya “hapa”
“abari” badala ya “habari”
“adi” badala ya “hadi”
“hingia” badala ya “ingia”
“hona” badala ya “ona”
“hangalia” badala ya”angalia” nk

Na kibaya zaidi, hadi kwenye vyombo vya habari (redio, TV) haya yapo.

Kuna utani usemao: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kikakulia na kulelewa Tanganyika, kikaugua Kenya, kikalazwa hospitali na kufia Uganda, Rwanda na Burundi na kuzikwa Zaire.

Tusipoamka, usemi huu utakuwa kinyume. Wenzetu Rwanda wanaamka; Kenya wako macho – Kitafia kwetu baada ya miaka kadhaa.

Tufanyeje ili tubaki salama?
 
Tuongee kingereza tu hamna namna, mana naona siku hizi watu wanasahau sana kiswahili, hadi diamond kiswahili kinampiga chenga anaelewa english zaidi
 
twende tu hivyo hivyo, tunataka kiswahili iwe lugha ya Afrika. Mabadiliko ya mazingira na utandawazi ndo yanaleta yote hayo, kufupisha maneno mwishowe mazoea. Bora mawasiliano, kwani kazi ya lugha ni nini??? hata kiingereza kuna maneno ya kihuni tu kibao, hasa huko Marekani.
 
Ni kweli Bayyo ipo lugha rasmi na isiyo rasmi (formal & informal) lakini haimaamishi kuongea "broken". Hata isiyo rasmi inakuwa sahihi ila tu haitumiki kwenye mazingira rasmi kama redioni.
 
Kila ninapotazama mbele –tuseme miaka 20 ijayo – kuhusiana na lugha yetu ya Kiswahili, naona tunakoelekea kama taifa si kuzuri sana.

Zamani ilizoeleka utani kwa watu wa kanda ya ziwa ambao kwa ujumla hupata tabu sana kutenganisha /l/ na /r/. Unaweza usijue kasema “kura” au “kula” – maana yote mawili anayatamka kwa kufanana.

Lakini hivi sasa kumezuka shida kubwa isiyohusiana na kabila, na inaendelea kukua hususan kutokana na kurahisika kwa mawasiliano – facebook, instagram, nk.

Kuna shida nyingi hivi sasa lakini mojawapo ni ya matumizi ya /a, e, i, o, u/ kwa upande mmoja na /h/ kwa upande wa pili. Yaani panapotakiwa /h/ anaiondoa; na isikotakiwa anaiweka.

Mfano, mtu anasema: “Ana ela yule” kumbe anamaanisha “Hana hela yule.”

Sasa Watu wanasema:

“apa” balala ya “hapa”
“abari” badala ya “habari”
“adi” badala ya “hadi”
“hingia” badala ya “ingia”
“hona” badala ya “ona”
“hangalia” badala ya”angalia” nk

Na kibaya zaidi, hadi kwenye vyombo vya habari (redio, TV) haya yapo.

Kuna utani usemao: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kikakulia na kulelewa Tanganyika, kikaugua Kenya, kikalazwa hospitali na kufia Uganda, Rwanda na Burundi na kuzikwa Zaire.

Tusipoamka, usemi huu utakuwa kinyume. Wenzetu Rwanda wanaamka; Kenya wako macho – Kitafia kwetu baada ya miaka kadhaa.

Tufanyeje ili tubaki salama?

Anayeongoza kuvuruga Kiswahili ni mtangazaji Sam Mahela.Huyu hawezi tena
.Maria Edward wa Channel 10 amejirekebisha kwa sasa.Regina Mziwanda anaongoza kwa kiswahili kizuri kwa watangazaji wote Afrika mashariki na kati.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom