Je, kujivunia kwetu Kiswahili kuna usalama?

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
762
Kila ninapotazama mbele –tuseme miaka 20 ijayo – kuhusiana na lugha yetu ya Kiswahili, naona tunakoelekea kama taifa si kuzuri sana.

Zamani ilizoeleka utani kwa watu wa kanda ya ziwa ambao kwa ujumla hupata tabu sana kutenganisha /l/ na /r/. Unaweza usijue kasema “kura” au “kula” – maana yote mawili anayatamka kwa kufanana.

Lakini hivi sasa kumezuka shida kubwa isiyohusiana na kabila, na inaendelea kukua hususan kutokana na kurahisika kwa mawasiliano – facebook, instagram, nk.

Kuna shida nyingi hivi sasa lakini mojawapo ni ya matumizi ya /a, e, i, o, u/ kwa upande mmoja na /h/ kwa upande wa pili. Yaani panapotakiwa /h/ anaiondoa; na isikotakiwa anaiweka.

Mfano, mtu anasema: “Ana ela yule” kumbe anamaanisha “Hana hela yule.”

Sasa Watu wanasema:

“apa” balala ya “hapa”
“abari” badala ya “habari”
“adi” badala ya “hadi”
“hingia” badala ya “ingia”
“hona” badala ya “ona”
“hangalia” badala ya”angalia” nk

Na kibaya zaidi, hadi kwenye vyombo vya habari (redio, TV) haya yapo.

Kuna utani usemao: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kikakulia na kulelewa Tanganyika, kikaugua Kenya, kikalazwa hospitali na kufia Uganda, Rwanda na Burundi na kuzikwa Zaire.

Tusipoamka, usemi huu utakuwa kinyume. Wenzetu Rwanda wanaamka; Kenya wako macho – Kitafia kwetu baada ya miaka kadhaa.

Tufanyeje ili tubaki salama?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom