Je, kuanzisha mahusiano kupitia mitandao ya kijamii ni sawa?

Ryan Herman

Member
Jul 26, 2019
42
46
Habari wanaJF,

Ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii limekuwa kwa kasi kwa sasa. Hii imepelekea watumiaji kuwa wengi pia na wengi wao wakiwa ni vijana.

Watu wengi wamekuwa wakianzisha mawasiliano kupitia mitandano ya kijamii. Mawasiliano hayo hupelekea wengine hadi kuanzisha urafiki au mahusiano ya kimapenzi Kabla ya kukutana ana kwa ana na hutumiana picha zao na husifiana pia.

Je, nisahihi kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mtu mliyekutana mtandaoni?

Je, ni nini madhara ya kuwa kwenye mahusiano?
 
Binafsi naona sawa tu as long as mmeelewana wote wa wili mmepatana mkakubaliana naona kama mitandao nikama njia tu kama mnavyokutana kanisani msikitini na pengine.
Nakubaliana na wewe kuwa ni njia Kama njia zingine ila mitandao ya kijamii wahusika huwa mbali mbali na huchukua muda kuonana ana kwa ana hii haiwezi kuleta madhara ya kweli?
 
Ng'mbe na mbuzi ndio sio sahihi wao mpaka waonane physically....ila kwasie human race sawa.
 
Ila kuna muda itawabidi muonane na hamjuani kitabia
Ndio lengo hasa la mahusiano ,lazima iko siku itabidi mkutane,kama ni swala la kuonana mnaweza hata mkatumia video chats na mkaonana kwenye mitandao kabla ya kukutana physically...
 
wengine tunaingia kazini alfajiri na kurudi saa 6 za usiku,unadhani tutapata wapi muda wakuonana na warembo hiyo mitandao inasaidia na tutaoana humu humu
 
Mkuu watu wana wrong number na wanaanzisha mahusiano mpka kuoana sembuse mtandaon ambapo picha mnatumiana na bado mnakutana na mtaendelea kufahamiana zaidi

Kwa hyo ni njia kama njia nyingine ila kutokana na kuongezeka kwa magonjwa na kupungua kwa binadam waaminifu duniani yatupasa kupima afya zetu na pia kutambulishana kwa ndugu wa asili wa kila pande ili iwe rahis kumtrack mtu kwa chochote
 
Ndio lengo hasa la mahusiano ,lazima iko siku itabidi mkutane,kama ni swala la kuonana mnaweza hata mkatumia video chats na mkaonana kwenye mitandao kabla ya kukutana physically...
Hudhani Kama mtu anaweza kukudanganya kupitia picha hata hizo video calls?
 
Back
Top Bottom