Je, Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia kuanzia shule za sekondari mpaka vyuo vikuu? Jadili

achana na kiswshili, ongeza mkakati wa uelewa wa english. pili tuko na wenzetu wa EAC, tusiende kivyetuvyetu, do things in consideration that we are east africans, that should be the spirit
Nipe mfano wa nchi moja tu iliyoendelea ambayo haitumii lugha mama katika elimu.
 
sawa hizo lugha zinafundishwa taangu awali, ila je ni ipi ambaayo wwanafunzi wanayoielewa zaidi ya nyingine? kuna baadhi ya ndugu zangu wasukuma walikua wanapelekwa shuleni huku wakiwa hawajui kiswahili wala kiingereza. ila wanamaliza darasa la saba wakiwa wanajua kiswahili na sio kiingereza.

hata hivyo, hapa mada sio kujifunza lugha ya kishwahili au kiingereza, bali kutumia lugha itayowarahisiahia wanaafunzi kuelewa maasomo.

kwakua hapa tunazungumzia kuelewa masomo (haha haya ya nadharia) kwa kutumia lugha fulani. tuchukulie elimu yetu sasa ni nadharia na iko hivi na tunataka wanafunzzi wetu waielelewe kama ilivyo. tua point ya moja kwa moja juu ugumu wa kutumika kwa kiswahili ktk hii hii elimu yetu ya nadharia na baadaala yake ukaona ni rahisi zaidi kwa wanaafunzi kutumia kiingereza.

mimi nimetoa faida ya kutumika itaakua
*kwanza, sisi wenyewe tutajifunza lugha yetu kwa kujiongezea misamiati. kama sisi wenyewe waswahili hatutaki kukijua kiswahili, tunategemea nani kutoka nchi gani atakijui kwa niaba yetu?

*wanafunzi wataanza kuelewa vyema masomo yaao. kwanza tukubaliane kua, kiswahili cha kufundishia hakitakua kigumu kama unavyosema wewe, ndio maana hata hapa tunabadilishana mawazzo kwa kutumia kiswahili rahisi na tunaelelwana. sasa tujiulize kujifunza kitu kwa lugha unayoielewa na kwa kujifunza kwa lugha usioielewa, wapi kuna urahisi? tusifichane kwa hili,

kuna vijana wanashindwa kuelewa vyema masomo yao kwakua wanashindwa kushiriki vyema darasani kutokana na kutofahamu lugha ya kiingereza. sasa kwanini tukumbatie kitu kinachowafanya wanafunzi wengi kubaki na ujinga, wakati lengo letu ni kuelimisha kizazi chetu?



sawa kiswahili ni kigumu na kiingereza ni kigumu. ila lengo sio kujifunza kiswahili au kiingereza faswaha, bali lengo ni kurahisihsha kuelewa kwa wanafunzi. sasa kwakua lugha zote ni ngumu, tuangalie yenye uafadhali ambayo itarahisisha kuelewa kwa wanafunzi. lengo letu wanafunzi wetu waelewe, na sio kukariri. nilishuhudia nilipokua form five. mwalimu wa chemistry alifululiza wiki nzima hajaongea neno lolote la kiswahili. siku moja alifafanua kitu kwa kiswahili. darasa zima likapumua, kisha kijana mmoja akainua mkono na kusema. "kwakweli mwalimu tangu ulipoanza kufundisha, hapo ulipochaanganya na kiswahili, ndipo nilipokelewa zaidi". hapa unapata picha kua kumbe kula lugha inamafanya mtu aelewe zaidi na nyingine unamuacha mtu na ujinga fulani. tusiukumbatie ujinga.




lengo letu sio kujua lugha tu, bali hasa hasa ni kuelewa masomo. kwakua bado hatujabadili elimu ya kiutumwa, basi tutumie lugha mabayo itarahisisha hata kuielewa hiyo hiyo elimu ya kiutumwa. waliofunguka mapema,

wanatumia lugha zao kufundishia ili kurahisisha kueleweka kwa masomo, na lugha za kigeni zinabaki kama maasomo ya kawaida.
Lugha zote nisawa maaan mwalim hata kam anaongea au kufundia lkn lzm atumie kiswahili eili wanafunz wa weze kuelew vzr aup mkuuu
 
"Kiingereza ndio Kiswahili cha Dunia"
-- Mwalimu Julius Nyerere. circa 1986.


Swali lingekuwa: Ungempeleka mwanao kusoma katika shule inayotumia Kiswahili tu kufundishia?
 
Kizazi ambacho kwa bahati mbaya kilijikuta katika umbumbu wa lugha ya Kiingereza ndicho kinachodai kwamba lugha ya kufundishia iwe Kiswahili.Si kwa vile ndilo jambo sahihi la kufanya ,lahasha, ni kwa vile wao ni mbumbumbu wa lugha ya Kingereza.Katika mazingira hayo, si busara kuamua kuachana na Kingereza,busara ni kugangamala kukijua Kingereza kwa kuwa sisi si kisiwa.

Mfumo wetu wa Elimu mbovu ndio uliotufikisha hapa tulipo na bila juhudi za makusudi ambazo sizioni, hatuwezi kutoka hapa tulipo.Kwa bahati mbaya kila awamu ya utawala kwa makusudi au kwa kutokujua imekuwa inaturudisha nyuma kielimu.

Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako ambae aliingia kwa mbwembwe nyingi akiahidi kuboresha elimu na yeye naona kachoka ile mbaya.Kiukweli kutoka hapa tulipo kielimu itakuwa kudra tu ya mwenyezi Mungu.Elimu yetu iko taabani sana.Vijana wetu wanaojiita wasomi ni mbumbumbu kabisa.
 
Kizazi ambacho kwa bahati mbaya kilijikuta katika umbumbu wa lugha ya Kiingereza ndicho kinachodai kwamba lugha ya kufundishia iwe Kiswahili.Si kwa vile ndilo jambo sahihi la kufanya ,lahasha, ni kwa vile wao ni mbumbumbu wa lugha ya Kingereza.Katika mazingira hayo, si busara kuamua kuachana na Kingereza,busara ni kugangamala kukijua Kingereza kwa kuwa sisi si kisiwa.Mfumo wetu wa Elimu mbovu ndio uliotufikisha hapa tulipo na bila juhudi za makusudi ambazo sizioni, hatuwezi kutoka hapa tulipo.Kwa bahati mbaya kila awamu ya utawala kwa makusudi au kwa kutokujua imekuwa inaturudisha nyuma kielimu.Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako ambae aliingia kwa mbwembwe nyingi akiahidi kuboresha elimu na yeye naona kachoka ile mbaya.Kiukweli kutoka hapa tulipo kielimu itakuwa kudra tu ya mwenyezi Mungu.Elimu yetu iko taabani sana.Vijana wetu wanaojiita wasomi ni mbumbumbu kabisa.
Unaonekana wewe umekariri tu. Hebu nitajie umuhimu wa Kiingereza kwa nukta kama 5 tu hivi? Nataka kujua kama unajua unachoongea. NB: Kiingereza ni muhimu ila je tunaujua huo umuhimu wake au tumekaririshwa tu kuwa Kiingereza ndio kila kitu. Tueleze.
 
Kuwepo na shule za Kiswahili kuanzia nursery mpaka vyuo vikuu vya Kiswahili na pia ziwepo shule za kiingereza kuanzia nursery mpaka vyuo vikuu. Kisha wananchi waachwe wachague wanapoona panawafaa watoto wao. Mimi na familia yangu tutachagua shule za kiingereza.
 
Miaka ya nyuma (1950s & 1960s) kujifunza Kiingereza ilianzia darasa la 3 (Standard III). Kiwango cha lugha hiyo kwa walioingia Form I kilikuwa cha juu na walimudu masomo yote

yaliyofundishwa kwa Kiingereza isipokuwa Kiswahili chenyewe. Hata Kifaransa kilifundishwa na kutahiniwa katika ngazi ya Sekondari! Na walioendelea na masomo / mafunzo zaidi Kiingereza hakikuwatatiza wakiwepo hapa nchini hata nje!

Swali - Ni kitu gani kimesababisha hizi kelele za sasa? Jibu - Tumepuuzia kuwekeza vya kutosha kwenye elimu; elimu ya kutenda!

Hata kuandika na kuzungumza Kiswahili fasaha ni taabu hivi sasa!
Kwa kadiri dunia inavyokwenda sasa, inabidi siyo tu kujua Kiswahili fasaha, pia kujua kwa ufasaha Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kirusi nk!

Kwa sasa Kiingereza kiendelee kutumika kufundishia ila kuwepo mkazo wa kupata waalimu bora wa kuifundisha lugha hiyo, na nyinginezo.

Kinachotakiwa - tuache kushabikia masuala ya maana kisiasa bali mambo ya msingi ya kujiendeleza kiuchumi!
[If you think education is expensive, try ignorance! .....]
 
HATA KIINGEREZA MANENO YA KIGIRIKI NA KILIYAACHA KAMA YALIVYOKUA. HATA SISI HATUTATAFRISI NENO PHYSICS KUA KUA NENO TULUTILU, BALI TUTAITAFSIRI KAMA NENO FIZIKIA. mbona PSYCHOLOGY tunajua kama SAIKOLOJIA na hakuna kilichoharibika wala ugumu!!!
sio rahisi kama unavyofikiria hapo unatafasiri maneno, na bado maengine magumu na abstract conecpt mfano tafasiri pia neno enantiomer, chirality, plane polarized rotation, staggered conformation quantum, multiple integral....na hapo concept kibao ambazo ni abstract.
 
Kuwepo na shule za Kiswahili kuanzia nursery mpaka vyuo vikuu vya Kiswahili na pia ziwepo shule za kiingereza kuanzia nursery mpaka vyuo vikuu. Kisha wananchi waachwe wachague wanapoona panawafaa watoto wao. Mimi na familia yangu tutachagua shule za kiingereza.
huu ni utafiti tutakua tunafanya na kuchezea elimu...
 
Kiingereza ni cha Waingereza na wengineo waliopenda ama kulazimika kukitumia. Sisi tulilazimika kukitumia kabla ya uhuru maana ilikuwa lugha ya Mkoloni. Mawazo ya Serikali ya Tanzania baada ya Uhuru yalikuwa mazuri sana. Lugha ya mtu ina mafao mengi sana kuliko yale tunayoweza kuyaona kwa haraka. Nyote mnajua ya kwamba lugha ya mtu inampa "utambulisho" (identity) msemaji miongoni mwa mataifa ama makabila yaliyopo katika jamii husika.Utambulisho unampa mtu heshima na kuulinda utamaduni wake.

Utamaduni wa mtu unaulinda utu wa mtu.Kwa maana hiyo basi lugha ya kigeni inaondoa mengi ya hayo. Mtu anaupoteza utambulisho wake anapopoteza asili yake na utamaduni wake na kukumbatia ule wa pili yaani wa watu wengine. Hicho ndicho kinachowasumbua WaMarekani weusi kule Marekani hicho kiunganishi wamekipoteza. Ni Waafrika kwa ngozi na rangi ya ngozi lakini utamaduni wao ni mwingine kabisa. Kwa wazungu haupo ni wa aina yao tu. Na ndio maana utakuta mara wamejipa majina ya Kiafrika kama vile Ron "Karenga"; ama ya kidini kutoka ngambo kama vile "Imamu Baraka" ama "Abdul Malik Al Shabaaz". Wakajenga shule wakaziita "Ujamaa shule." Wakabuni sikukuu yao inayoitwa mpaka leo "Kwanzaa." Wengine wakatamani kutafuta asilia yao Afrika wakangoa nanga na kutua katika pwani ya Liberia katika kambi ya Munroe iliyokuja kuitwa "Monrovia," mji mkuu wa Liberia leo. Huko Marekani ya Kati watu wakapenda nao kurudi Afrika wakaunda dhana ya "Uafrika" ama "Back To Africa Movement," au "Turudi Afrika." George Padmore raia wa Trinidad na Marcus Garvey Mjamaica wote kwa nyakati zao waliongoza vuguvugu hilo wakagombana sana na wazungu wa Marekani ya Kati na kwingineko. Miaka michache iliyopita Alex Haley akachapa kitabu "Roots," kuonyesha uzito walio nao WaMarekani weusi wa kuijua asili yao.

Sisi tuna asili yetu na lugha zetu husususan ya Kiswahili ambayo inaweza kuutunza utu wetu na utamaduni wetu Watanzania na kutufanya tuheshimike nje ya mipaka yetu na ndani mwetu. Ukitaka uraia wa Marekani, Finland, Sweden na Ujerumani miongoni mwa masharti ni kujua kuizungumza lugha husika.Sisi tunataka kukumbatia tu lugha za watu. Vyuo vikuu vingi tu duniani katika nchi za watu vipo vinavyofundisha kwa Kiingereza lakini vingi ni kikwao tu. Korea Kusini, Uchina, Ujerumani. Na sisi tufundishe kwa Kiswahili watu waje kwetu wajifunze kiswahili (wakitaka) mwaka mmoja ama miwili kisha waendelee na masomo ya kiufundi ya chuo kikuu.Mnakumbuka kwa nini vijana wa Soweto walikubali kufa Afrika Kusini? Moja ni kugoma kujifunza masomo hadi chuo kikuu kwa lugha ya kaburu ya "Afrikaans."

Kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia vyuoni haina maana kwamba Kiingereza hakitakuwepo. Kitafundishwa na kufundisha kweli kweli isipokuwa rasmi Kiswahili ndio lugha ya kufundishia. Wachina wameweza, Wajerumani wameweza na Waitaliano wameweza. Hapo ndipo tutaheshimika na hawa wazungu. Kuna siku nilikuwa katika mkutano wa kimataifa wa kidini, nikapewa nafasi ya kuomba. Nikawaambia waliokuwepo kwamba ningependa kuomba kwa Kiswahili ili msikie jinsi lugha yetu ilivyo tamu pia. Baada ya kumaliza walifurahi na kuniheshimu kwani niliwaonyesha kwamba najivunia Uswahili wangu na Utanzania wangu hata kama nipo katikati yao.

Tukikitumia Kiswahili tutaoa mchangi mkubwa sana katka ulimwengu wa Kielimu kwa sababu tutaingiza maneno mengine ya Kiswahili yatakayokubalika na kutumika kama ya kisomi kutokana na utajiri wa maana utakaodhihirika katika maneno hayo. Kwa mfano lazima neno "pole" litapata sehemu kubwa sana ya kufurahiwa. Wao huliita neno hilo "magic Swahili word." Pole kwa kufiwa! Pole kwa kujifungua! Pole kwa Kuumwa! Pole sana kwa juhudi yako! Pole kwa Mtihani! Pole sana ndugu umepambana mpaka umeshinda!

mwaka fulani tulikuwa pale Cuo Kikuu na watafsiri wa lugha waliokuwepo kutoa mada zao waliombwa kufikiria kutafsiri vitabu vya kiingereza vya kimasomo ili kukikuza Kiswahili Lugha ya taifa na kuwezesha Vyuo vyetu kuwa na vitabu vya Kielimu vingi katika Kiswahili. Hiyo ni njia mojawao ya kujiandaa. Kutafsiri vitabu vilivyopo vya kielimu ama kuandika vingi vingine vipya vya Kielimu. Wasomi wetu walio Waswahili wanapaswa kufikiria jukumu hili tunapojadili jambo hili. Wachina wameweza, Wajerumani wameweza, Wafaransa wameweza na siis tutaweza.
 
Tatizo la kiswahili ni vitabu na nakala za kielimu. Kama huwezi kusoma kingereza itakuwa ngumu kusoma vitabu na nakala nyingi sana za kisomi dunia nzima. Ni vizuri kujua kiswahili na English zote vizuri tusije tukawa kama sasa na PHD degrees kwenye english lakini hawawezi kuongea
 
sio rahisi kama unavyofikiria hapo unatafasiri maneno, na bado maengine magumu na abstract conecpt mfano tafasiri pia neno enantiomer, chirality, plane polarized rotation, staggered conformation quantum, multiple integral....na hapo concept kibao ambazo ni abstract.

hayo maneno pia sio ya kiingereza. tutayaiba kama waingereza walivyoiba. mbona waingereza hawakuamua kujifunza kwa kutumia kigiriki au kilatini? badala yake wakaiba misamiati tu. waliona ili kizazi chao kielewe zaidi, waliamua kutumia lugha yao (yaani kiingereza) kama lugha ya kuelezea/kufundishia hiyo misamiati.

sababu zilizowafanya waingereza kuamua kujifunza kwa kiingereza chao, wakati concepts za kisayansi na kifalsafa zote zilikua ktk lugha ya kilatini au kigiriki; ndizo zitazotufanya na sisi tutumie kiswahili chetu. kiswahili hakitashindwa kama kiingereza ambavyo hakikushidwa. ikishindikana kitumika kiswahili, tutakua tumeshindwa sisi kwa sababu ya kutoamua, ila kiswahili chetu hakitakua kimeshindwa.
 
Kiingereza ni cha Waingereza na wengineo waliopenda ama kulazimika kukitumia. Sisi tulilazimika kukitumia kabla ya uhuru maana ilikuwa lugha ya Mkoloni. Mawazo ya Serikali ya Tanzania baada ya Uhuru yalikuwa mazuri sana. Lugha ya mtu ina mafao mengi sana kuliko yale tunayoweza kuyaona kwa haraka. Nyote mnajua ya kwamba lugha ya mtu inampa "utambulisho" (identity) msemaji miongoni mwa mataifa ama makabila yaliyopo katika jamii husika.Utambulisho unampa mtu heshima na kuulinda utamaduni wake. Utamaduni wa mtu unaulinda utu wa mtu.Kwa maana hiyo basi lugha ya kigeni inaondoa mengi ya hayo. Mtu anaupoteza utambulisho wake anapopoteza asili yake na utamaduni wake na kukumbatia ule wa pili yaani wa watu wengine. Hicho ndicho kinachowasumbua WaMarekani weusi kule Marekani hicho kiunganishi wamekipoteza. Ni Waafrika kwa ngozi na rangi ya ngozi lakini utamaduni wao ni mwingine kabisa. Kwa wazungu haupo ni wa aina yao tu. Na ndio maana utakuta mara wamejipa majina ya Kiafrika kama vile Ron "Karenga"; ama ya kidini kutoka ngambo kama vile "Imamu Baraka" ama "Abdul Malik Al Shabaaz". Wakajenga shule wakaziita "Ujamaa shule." Wakabuni sikukuu yao inayoitwa mpaka leo "Kwanzaa." Wengine wakatamani kutafuta asilia yao Afrika wakangoa nanga na kutua katika pwani ya Liberia katika kambi ya Munroe iliyokuja kuitwa "Monrovia," mji mkuu wa Liberia leo. Huko Marekani ya Kati watu wakapenda nao kurudi Afrika wakaunda dhana ya "Uafrika" ama "Back To Africa Movement," au "Turudi Afrika." George Padmore raia wa Trinidad na Marcus Garvey Mjamaica wote kwa nyakati zao waliongoza vuguvugu hilo wakagombana sana na wazungu wa Marekani ya Kati na kwingineko. Miaka michache iliyopita Alex Haley akachapa kitabu "Roots," kuonyesha uzito walio nao WaMarekani weusi wa kuijua asili yao.

Sisi tuna asili yetu na lugha zetu husususan ya Kiswahili ambayo inaweza kuutunza utu wetu na utamaduni wetu Watanzania na kutufanya tuheshimike nje ya mipaka yetu na ndani mwetu. Ukitaka uraia wa Marekani, Finland, Sweden na Ujerumani miongoni mwa masharti ni kujua kuizungumza lugha husika.Sisi tunataka kukumbatia tu lugha za watu. Vyuo vikuu vingi tu duniani katika nchi za watu vipo vinavyofundisha kwa Kiingereza lakini vingi ni kikwao tu. Korea Kusini, Uchina, Ujerumani. Na sisi tufundishe kwa Kiswahili watu waje kwetu wajifunze kiswahili (wakitaka) mwaka mmoja ama miwili kisha waendelee na masomo ya kiufundi ya chuo kikuu.Mnakumbuka kwa nini vijana wa Soweto walikubali kufa Afrika Kusini? Moja ni kugoma kujifunza masomo hadi chuo kikuu kwa lugha ya kaburu ya "Afrikaans."

Kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia vyuoni haina maana kwamba Kiingereza hakitakuwepo. Kitafundishwa na kufundisha kweli kweli isipokuwa rasmi Kiswahili ndio lugha ya kufundishia. Wachina wameweza, Wajerumani wameweza na Waitaliano wameweza. Hapo ndipo tutaheshimika na hawa wazungu. Kuna siku nilikuwa katika mkutano wa kimataifa wa kidini, nikapewa nafasi ya kuomba. Nikawaambia waliokuwepo kwamba ningependa kuomba kwa Kiswahili ili msikie jinsi lugha yetu ilivyo tamu pia. Baada ya kumaliza walifurahi na kuniheshimu kwani niliwaonyesha kwamba najivunia Uswahili wangu na Utanzania wangu hata kama nipo katikati yao.

Tukikitumia Kiswahili tutaoa mchangi mkubwa sana katka ulimwengu wa Kielimu kwa sababu tutaingiza maneno mengine ya Kiswahili yatakayokubalika na kutumika kama ya kisomi kutokana na utajiri wa maana utakaodhihirika katika maneno hayo. Kwa mfano lazima neno "pole" litapata sehemu kubwa sana ya kufurahiwa. Wao huliita neno hilo "magic Swahili word." Pole kwa kufiwa! Pole kwa kujifungua! Pole kwa Kuumwa! Pole sana kwa juhudi yako! Pole kwa Mtihani! Pole sana ndugu umepambana mpaka umeshinda!

mwaka fulani tulikuwa pale Cuo Kikuu na watafsiri wa lugha waliokuwepo kutoa mada zao waliombwa kufikiria kutafsiri vitabu vya kiingereza vya kimasomo ili kukikuza Kiswahili Lugha ya taifa na kuwezesha Vyuo vyetu kuwa na vitabu vya Kielimu vingi katika Kiswahili. Hiyo ni njia mojawao ya kujiandaa. Kutafsiri vitabu vilivyopo vya kielimu ama kuandika vingi vingine vipya vya Kielimu. Wasomi wetu walio Waswahili wanapaswa kufikiria jukumu hili tunapojadili jambo hili. Wachina wameweza, Wajerumani wameweza, Wafaransa wameweza na siis tutaweza.
nimependa jinsi uliyoelezea. naonga mkono kuulinda na kutangaza utamaduni wetu kupitia kiswahili.
 
Kuwepo na shule za Kiswahili kuanzia nursery mpaka vyuo vikuu vya Kiswahili na pia ziwepo shule za kiingereza kuanzia nursery mpaka vyuo vikuu. Kisha wananchi waachwe wachague wanapoona panawafaa watoto wao. Mimi na familia yangu tutachagua shule za kiingereza.
Kwa sababu wewe na familia yako ni waingereza au?
 


Kuna watu wanasema kuwa lugha ya kufundishia kwenye mfumo wetu wa Elimu iwe Kiingereza kwa sababu Kiingereza ndo lugha ya dunia na uandishi wa vitabu mbali mbali na ugunduzi wa technologia nyingi ikiwepo kompyuta uko kwenye lugha ya kiingiereza.

Watetezi wa hoja hii wanasema nchi nyingi zlilizoendelea zinatumia kiingereza kwa hivyo sisi tulio nyuma kimaendeleo hatuwezi kuacha kufundisha watoto wetu kwa lugha hiyo ya dunia.

Watetezi wa hoja hii wanasema tusipojifunza kiingereza tutashindwa kuwasiliana na nchi tajiri duniani kama Uingereza, marekani nk ambazo zinatumia kiingereza. Kushindwa kuwasiliana huko kutaathiri mahusiano yetu na nchi Tajiri na mwishowe tutashidwa kufanya biashara na nchi hizo. Kubwa zaidi, hata vijana wetu hawataweza kuajiriwa katika nchi hizo.

Watetezi wengi wa hoja hii ni wanasiasa ambao watoto wao ama wanasoma nje ya nchi ama wako ndani ya nchi lakini kwenye shule za st xyz au accademy ambazo shule zinazotumia kiingereza kama lugha ya kufundishia.

Kwa upande wa pili, Wako wanaosema kiingereza isiwe lugha ya kufundishia kwenye shule na vyuo vyetu. Watetezi wa msimamo huu wengi wao (si wote) ni wataalamu wa vyuo vya juu, wao wanasema kiingereza ifundishwe kama lugha nyingine yo yote kama kifaransa, kichina, kireno, kiarabu nk ili watanzania wawasiliane na watu wengine duniani. Wao wanataka lugha ya kufundishia shuleni na vyuoni iwe kiswahili.

Sababu zao ni kama hizi zifuatazo:

Kwamba wanadai kuwa kisayansi Binadamu yo yote hufikiri kwa kutumia lugha ya kwanza wa wazazi wake, kisha hulazimika kutafsiri lugha hiyo kichwani kama atalazimika kuongea kiingereza na kwamba mchakato huu unarudisha nyuma au unachelewesha ubunifu wa watoto na hivyo tunaishia kuwa na wasomi waliokariri badala ya wasomi wanaoibua vitu vipya.

Matokeo yake wahitimu wa vyuo vikuu hawaji na ugunduzi wo wote mpya na mwisho wa siku wasomi wetu wa kukariri kiingereza wameshindwa kututoa kwenye lindi la umasikini pamoja na rasilimali nyingi tulizo nazo.

Pili, kwa kuwa kiingereza yenyewe ni tabu, wengi wanadhani kuwa wanafunzi wengi wa sekondary wakifika shuleni wanaanza kuhangaika na lugha ya kiingereza matokeo yake uelewa/ufaulu wao kwenye masomo lengwa unaathiriwa.

Watetezi wa hoja hii wanatoa mifano ya nchi kama China, Korea kusini, Malaysia nk ambazo zimeendelea kwa kutumia lugha zao za asili na hawatumii kiingereza hata kwenye mifumo yao ya Elimu. China kwa sasa ndo mkopeshaji wa Marekani.

Kati ya watetezi wa hoja hii wako Dr Martha Qoroo( Dean wa Chuo kikuu cha Dsm) na Jenerali Ulimwengu (mmiliki wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania)

Tume ya jaji Warioba kwenye rasimu yao ya pili walitangaza kiswahili kama lugha rasmi ya Taifa lakini hawakusema pia kwamba Kiingereza kisiwe lugha ya kufundishia -- waliipa kiswahili nguvu lakini kuhusu lugha ya kufundishia walikaa kimya.

kwa maneno rahisi akina Warioba walikwepa mjadala huu na kuamua kukaa katikati, japo katikati yao inaelemea upande wa Kiswahili zaidi hata kama ni kwa kiasi kidogo sana.

Wewe una maoni gani na kwa nini?

"I have two rats and one table" itamke hiyo sentesi kwa kiswahili ujue kuwa kiswahili kigumu
 
Tatizo la kiswahili ni vitabu na nakala za kielimu. Kama huwezi kusoma kingereza itakuwa ngumu kusoma vitabu na nakala nyingi sana za kisomi dunia nzima. Ni vizuri kujua kiswahili na English zote vizuri tusije tukawa kama sasa na PHD degrees kwenye english lakini hawawezi kuongea

Unachosema ni muhimu ila ujue kuipa kila lugha nafasi yake. Kiingereza kina nafasi yake kimataifa na Kiswahili kina nafasi yake kwa taifa. Lazima uwe makini katika kuchagua vipaumbele. Je tunataka watu wachache wazungumze Kiingereza au tunataka watu wengi waelimike kama taifa? Hapo lazima uchanganue.

Sayansi inatuambia kuwa kuwa na akili(intelligence) haimaanishi mtu utaweza kumaster kila kitu hata lugha ya kigeni. Kumaster lugha ya kigeni ni kama kipaji(talent) ambayo sio kila mtu anayo ni kama vile kuna watu wana kipaji cha kuimba wengine hawana ila haimaanishi kuwa hawana uwezo wa kufikiri, kuelewa na kuvumbua mambo.

Sasa unapoifanya elimu kuwa haipatikani isipokuwa kupitia lugha ya kigeni maana yake unawaweka watanzania waliowengi(wasio na kipaji cha lugha ya kigeni ila wana uzwezo mkubwa wa kusoma) katika disadvantage ya kukosa elimu.

Sasa tujiulize hapa Tanzania kuna watu wangapi wana kipaji cha lugha ya kigeni? Hizo data hazipo ila data zilizopo zinaonesha kuwa ni watanzania asilimia 5% wenye uwezo wa kusoma, kuelewa na kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha.

Asilimia 5%!!!! Hii inamaanisha kwa kukifanya kiingereza ndio lugha pekee ya kupitia ili kupata elimu maana yake ni kuwaweka asilimia 95% ya watanzania wasio na uwezo wa lugha kwenye ujinga. Hivi kwanini lugha ya kufundishia iwape kipaumbele asilimia 5% na iwaweke kando asilimia 95% ambao ndio wengi?

Kusema hivi simaanishi Kiingereza kitiwe kapuni na kisihimizwe. Kiingereza kihimizwe ila kichukuliwe kwa kadri ya umuhimu wake na sio kutia chumvi na kufanya kama kwamba bila kiingereza haiwezekani chochote, au tukiwa na Kiingereza ndio tuna kila kitu.

Basi nikwambie kitu, Sisi watanzania tunajua Kiingereza zaidi ya Wachina, hivi sisi ni bora kuliko wao? Kujua kwetu kiingereza kumetusaidia nini? Hayo ndio masuala ya kujiuliza tusiwe tu tunameza bila ya kuangalia uhalisia wa mambo. Kiingereza sio kila kitu.

Kiingereza ni muhimu kwa vile biashara ya kimataifa inahitaji lugha ya Kiingereza, Mambo mengi mapya ya kielimu na kiteknolojia huanza kupatikana kwa lugha ya Kiingereza kabla ya kupatikana kwa lugha nyenginezo. Sasa je sisi Kama Tanzania tuna biashara gani ya kimataifa hata tuwe tunasema eti tusipojua Kiingereza tutakosa ushindani wa soko la kimataifa? Hata kibiriti tunaagiza nje sasa soko gani hilo tunalolipigania. Kwanza tuwe na huo uwezo wa kuzalisha halafu ndio tupiganie soko. Hapa kuna hitilafu za nini kipaumbele!

Kwa kumalizia, Lugha ya Kiswahili itumike kama ndio lugha ya kufundishia na Lugha ya Kiingereza ifundishwe kama lugha tu ili watu waweze kuwasiliana kwa Kiingereza. Pia tuwe na shule, vyuo vitakavyotoa elimu kwa kiingeza ila viendane na haja hiyo pengine asilimia 5 hadi 10 ya taasisi zote za elimu na isizidi hapo.
 
b6d6710129db7c6d4f18dd59a12e7361.jpg
Wanafunzi wa chuo kikuu hadi leo hawajui kiingereza halafu eti ukiue kiingereza?
 
Unachosema ni muhimu ila ujue kuipa kila lugha nafasi yake. Kiingereza kina nafasi yake kimataifa na Kiswahili kina nafasi yake kwa taifa. Lazima uwe makini katika kuchagua vipaumbele. Je tunataka watu wachache wazungumze Kiingereza au tunataka watu wengi waelimike kama taifa? Hapo lazima uchanganue. Sayansi inatuambia kuwa kuwa na akili(intelligence) haimaanishi mtu utaweza kumaster kila kitu hata lugha ya kigeni. Kumaster lugha ya kigeni ni kama kipaji(talent) ambayo sio kila mtu anayo ni kama vile kuna watu wana kipaji cha kuimba wengine hawana ila haimaanishi kuwa hawana uwezo wa kufikiri, kuelewa na kuvumbua mambo. Sasa unapoifanya elimu kuwa haipatikani isipokuwa kupitia lugha ya kigeni maana yake unawaweka watanzania waliowengi(wasio na kipaji cha lugha ya kigeni ila wana uzwezo mkubwa wa kusoma) katika disadvantage ya kukosa elimu. Sasa tujiulize hapa Tanzania kuna watu wangapi wana kipaji cha lugha ya kigeni? Hizo data hazipo ila data zilizopo zinaonesha kuwa ni watanzania asilimia 5% wenye uwezo wa kusoma, kuelewa na kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha. Asilimia 5%!!!! Hii inamaanisha kwa kukifanya kiingereza ndio lugha pekee ya kupitia ili kupata elimu maana yake ni kuwaweka asilimia 95% ya watanzania wasio na uwezo wa lugha kwenye ujinga. Hivi kwanini lugha ya kufundishia iwape kipaumbele asilimia 5% na iwaweke kando asilimia 95% ambao ndio wengi? Kusema hivi simaanishi Kiingereza kitiwe kapuni na kisihimizwe. Kiingereza kihimizwe ila kichukuliwe kwa kadri ya umuhimu wake na sio kutia chumvi na kufanya kama kwamba bila kiingereza haiwezekani chochote, au tukiwa na Kiingereza ndio tuna kila kitu. Basi nikwambie kitu, Sisi watanzania tunajua Kiingereza zaidi ya Wachina, hivi sisi ni bora kuliko wao? Kujua kwetu kiingereza kumetusaidia nini? Hayo ndio masuala ya kujiuliza tusiwe tu tunameza bila ya kuangalia uhalisia wa mambo. Kiingereza sio kila kitu. Kiingereza ni muhimu kwa vile biashara ya kimataifa inahitaji lugha ya Kiingereza, Mambo mengi mapya ya kielimu na kiteknolojia huanza kupatikana kwa lugha ya Kiingereza kabla ya kupatikana kwa lugha nyenginezo. Sasa je sisi Kama Tanzania tuna biashara gani ya kimataifa hata tuwe tunasema eti tusipojua Kiingereza tutakosa ushindani wa soko la kimataifa? Hata kibiriti tunaagiza nje sasa soko gani hilo tunalolipigania. Kwanza tuwe na huo uwezo wa kuzalisha halafu ndio tupiganie soko. Hapa kuna hitilafu za nini kipaumbele!
Kwa kumalizia, Lugha ya Kiswahili itumike kama ndio lugha ya kufundishia na Lugha ya Kiingereza ifundishwe kama lugha tu ili watu waweze kuwasiliana kwa Kiingereza. Pia tuwe na shule, vyuo vitakavyotoa elimu kwa kiingeza ila viendane na haja hiyo pengine asilimia 5 hadi 10 ya taasisi zote za elimu na isizidi hapo.
Sijajua bado kitu gani unabisha Lugha ni muhimu sana kwa elimu. Elimu vilevile haina mipaka kwa nchi yetu na lugha yetu kufundisha elimu ya juu kwa kiswahili itakuwa kurudisha nyuma nchi yetu hasa wakati huu wa dunia kuwa ndogo na uwezo wa kufanya kazi kutoka sehemu yeyote. Mfano Wahindi wanajua kihindi lakini kuna kazi nyingi sana zina enda India kwasababu wanajua kingereza ingawa sio kizuri bado lakini kazi nyingi za accounting, engineering zinaenda India kwasababu ya lugha. Huwezi kufikiria Tanzania ndani ya nchi pekee nchi yetu ingeweza kuwapa watu ajira wengi tu kwa kujua kiingereza. Computer programmer, accounting, engineering sio lazima uwe kwenye nchi yako ndiyo ufanye kazi kwa technologia ya siku hizi
 
Back
Top Bottom