kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia bila kiingereza ni changamoto sana hasa kwa masomo ya sayansi. katika masomo haya kuna dhana (concept) ambazo ni abstract sana na zingine ni concrete na zinamaneno ya kukopa hasa kwenye lugha ya kigriki na kilatini kutokana na watu waliogundua dhana hizo, hivyo kuyabadili maneno yote kuwa katika kiswahili ni kazi kubwa na ngumu na inahitaji kuwa na rasilimali nyingi na za kutosha. lakini pia mtu unaweza kuwa unaelewa kitu katika lugha mama (traditional language) lakini ukashindwa kukitafasili katika lugha ya kiswahili, je utaweza kutafasili hayo maneno ya kigriki na kilatini kuwa katika kiswahili?....binafsi naunga mkono hoja ya serikali katika sera ya elimu ya 2014 kuhusu hlugha ya kufundishia na kujifunzia.....
Tamko.....3.2.19. Lugha ya Taifa ya Kiswahili itatumika kufundishia na
kujifunzia katika ngazi zote za elimu na mafunzo na
Serikali itaweka utaratibu wa kuwezesha matumizi
ya lugha hii kuwa endelevu na yenye ufanisi katika
kuwapatia walengwa elimu na mafunzo yenye tija
kitaifa na kimataifa.
3.2.20. Serikali itaendelea na utaratibu wa kuimarisha
matumizi ya lugha ya Kiingereza katika kufundishia na
kujifunzia, katika ngazi zote za elimu na mafunzo.