Je Kisiasa kupigania haki ni kosa?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Naomba kuwasilisha ili wale wenye mawazo zaidi wanafungue macho kwa upana zaidi. Hivi ni kosa kupigania haki, Je haki haipiganiwi?

Nauliza hivyo kwa sababu tumezaliwa TZ lakini mambo yanayofanyika tangu enzi za mwinyi hadi leo mfululizo bila kikomo yanatia aibu kuamini kuwa tz bado inawatanzania ndani yake au wote ni wageni. Ufisadi, wizi, uporaji, uongo na udanganyifu, matumizi mabaya ya serikali, siasa za wizi wizi wa kura hivi, rais anafurahia kuchagua tume ambayo inasimamia uchaguzi eti mfumo/katiba ndo inaruhusu!!! utashangaa kuna mambo mangapi kwenye katiba yamebadilishwa hata katiba bila kubadilishwa, waziri kiongozi yuko wapi, huo ni mfano tu. Sasa kama unaweza futa jambo ambalo limo kwenye katiba achilia kubadili kifungu cha katiba ili haki itendeke unashindwa???? tuna rais anayependa kutumia udhaifu wa katiba kwa faida yake binafsi????? kama rais ni muungwana hata chembe moja angeona haifai kuchagua tume ya uchaguzi wakati na yeye ni mgombea, harafu anataka watz tuamini kuwa hajapata urais kwa kupendelewa na mfumo mbaya ambao upo. kichekesho kweli kweli, nadhani hili linatokea tz tu, au africa pekee.

Sasa swali langu ni kwanini watz tunakuwa woga hata kudai haki zetu, kudai haki ni kosa??? kusema ukweli ni kosa??Jamani tunakufa maskini wakati nchi ni tajiri???!!! aibu hii tutamwambia nani??? Kwani kudai haki kwa vitendo ilikomea kwa babu zetu kina nyerere kawawa etc??? nisaidieni naona kiu ya kudai haki inanikaba koo.
 
Back
Top Bottom