#COVID19 Je, kirusi cha corona kina kasi ipi ya kujibadilisha?

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
JE KIRUSI CHA CORONA KINA KASI IPI YA KUJIBADILISHA?

Leo 16:30hrs 07/03/2021

Nianze kwa maswali fikirishi,Je kuna umuhimu wa watu kupata chanjo ikiwa kinga yako ni imara? Chanjo ina phase 4,uchukua miaka 5 hadi 10 kupita phase zote 4 kwa majaribio hadi kupata chanjo ambayo ina majibu yote ya madhara atayopata mtu baada ya chanjo,je chanjo hii imefikisha Miaka miwili, je ipo kwenye phase ya ngapi? Je, itamuangamiza kila kirusi anayejibadili kutoka kirusi kimoja kwenda kingine?

Mwili wa binadamu umeundwa na trilioni za seli, ndani ya kila seli kuna kiini ambacho kina aina 23 za chromosomes zinazobeba habari za maumbile ya mwili wa mwanadamu, kwenye chromosomes kuna urithi(vinasaba),nusu ya urithi kutoka kwa Mama na nusu kutoka kwa Baba,urithi huo tunauita DNA, ambayo inajumuisha kemikali inayoitwa deoxyribonucleic acid (DNA)

Taarifa zote za jinsi miili yetu inavyojengeka na kufanya kazi inabebwa kwenye hizo DNA. Kazi zote za miili yetu inafanyika kwenye saitoplasm ya seli zetu,kazi zote zinazofanyika kwenye kwenye mwili zinafanyika kwa maelekezo na usimamizi wa DNA,Ili DNA iweze kusimamia kazi inayofanyika kwenye saitoplasm huwa inatengeneza molecule ya Ribonucleic acid -RNA na kuituma huko kwenye saitoplasm kwenda kusimamia kazi husika,

Kirusi cha corona kinapoingia kwenye mwili wa mwanadamu,kinaingia kwa mfumo wa RNA ili kwenda kumchanganya DNA,kirusi iko cha corona kinakwenda kufanya kazi ya RNA ile ambayo imeundwa na DNA lakini inakwenda kufanya kazi kinyume nyume kwa kuleta majanga,tofauti na RNA inayoundwa na DNA ambayo inapokea maelekezo toka DNA, kirusi iko cha corona hakipokei maelekezo bali kinafanya kazi ya corona kwenda kuharibu mapafu na kugandisha damu mwilini.

Kama kilivyo kirusi cha mafua ambacho uwa kinabadilika kwenye kitambaa cha makamasi na kuzalisha kirusi kingine (new strain)nacho kirusi cha corona uwa kinabadilika,pengine kila mwaka tutahitajika kupata chanjo mpya ya kirusi fulani cha corona,kama ilivyo kwa kirusi cha mafua ambacho hutengenezwa kulinda watu kutokana na virusi vitatu au vinne vinavyoweza kusababisha ugonjwa huo wa mafua katika msimu wa mafua unaofauta,lakini hata wakati chanjo hailingani na virusi hivi ambavyo vinabadilika,je tutakuwa na chanjo za aina ngapi kwa virusi hivi vinavyobadilika badilika?

Chanjo zinatolewa kwa utaratibu maalum wa doses zake,dose ya kwanza ni ya kushtua tu (activate or prime) hizo seli za askari wa kinga (T memory & B memory cells),dose ya kwanza haikupi kinga yoyote, unahitaji doses zingine baada ya kipindi fulani (booster doses),kwa hizi chanjo za covid-19 unahitaji dose ya pili baada ya wiki 4 kwa Moderna na AstraZeneca na wiki 3 kwa zile chanjo za aina nyingine,hapo ndipo tunasema umepata chanjo (fully vaccinated) itakayoweza kukukinga usipate ugonjwa huo kwa kipindi fulani - kipindi hiki kwa kawaida ni miezi 6 ambapo utalazimika kupata booster dose nyingine.

Kinga uchukua takriban wiki 3 hadi 4 kwa kinga kuundwa mwilini
baada ya kupokea chanjo,na kinga hudumu katika msimu mmoja pengine kwa miezi sita,Masharti ya chanjo hizi za bure ni kwamba zichanje watu wenye afya nzuri walio na umri wa miaka 18 hadi 45.Wasiwe na magonjwa mengine ye yote including morbid obesity.Wamediriki hata kutuamuru kuwa watu hawa wawe ni walimu na polisi wetu,achana na ile chanjo ya kuuzwa dola mbili na lazima uchanjwe mara mbili jumla dola 4 watayopewa wagonjwa,wazee na manesi,wauguzi.

Kwa nini wanataka watu wa aina hii ndiyo tuwachanje wakati watu wa aina hii miili yao iko imara kukabili virusi vya corona kwa asilimia 99.9%?
Kwa mjanja atagundua kuwa wanataka kuwafanyia a phase IV clinical trial watu hawa ambayo matokeo yake yanaweza kuondoa wasi wasi walionao watu wao huko ughaibuni kuhusu hizi chanjo.

Wanatusubiri sisi tuchanjane,hadi sasa nchi 10 za Afrika zimekubali 'msaada' huu na faster faster zimepelekewa hizo chanjo na wameanza kuchanjana,Nchi inayokataa au kusuasua kupokea 'msaada' huu inaandamwa kinoma na inachukuliwa kama adui. Sisi hatujaukataa bali tumewaambia watupe muda wa wanasayansi wetu kufanya uchambuzi na utafiti. Loo ona mashinikizo tunayoyapata hadi kutoka kwa watu tunaowaheshimu sana. Tupeni muda kidogo. Uamuzi tutatoa bila kushinikizwa tuzitoe wapi na tumchanje nani,Black people have higher immunity than other races and species.

Kimkokotenge,nitoe maswali elekezi,chanjo hizi hazijapitia hatua zote nne yaani phase 1 hadi phase 4, Zimekuwa fast-tracked!! zingepitia hatua zote zingetumia miaka 10 kukamilika,lakini sasa zimetumia miezi 10 tu,kwa sababu hiyo maswali yafuatayo hayana majibu:

1. Nini athari za muda mrefu za chanjo hizi?

2. Je Kinga inayotokana na chanjo hizi itadumu katika miwili wa mwanadamu kwa muda gani?

3.Je chanjo hizi zinaweza kumkinga mtu dhidi ya aina nyingine ya kirusi cha corona?

4.Je Makampuni yaliyotengeneza chanjo hizo,yako tayari kuwajibika na athari za vifo,kuzimia,kuvimba mwili,mabaka mwilini,na athari kwenye vinasaba katika vizazi vijavyo?

Ikumbukwe kuwa kila siku aina nyingine ya virusi vya korona vinatokea kama matokeo ya mutation (mabadiliko katika mpangilio amino acids kwenye vinasaba vya virusi vya Corona),Mfano chanjo iliyoagizwa mwanzo na Afrika ya kusini haikuweza kudhibiti aina mpya ya corona iliyotokea Afrika ya kusini,wamepata hasara na inabidi watafute nchi ya kuiuzia!

5. Corona ni lengo linalotembea yaani it is the moving target! Je virus vya Corona vina kasi ipi ya kujibadilisha?

Nimalizie kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea za dawa ya ukimwi (ARV) kuweza kutumika kukinga kirusi cha corona,ikiwa kirusi cha Ukimwi ni cha RNA chenye genetic code 9 na kirusi cha corona nacho ni cha RNA chenye genetic codes 56 ambacho gamba lake la protein linaweza kuharibiwa na sabuni ya kuogea au kunawia mikono,hata joto la nyuzi 45 hadi 56 huweza kukisambaratisha kirusi iko,Sasa kikiwa kimeshaingia ndani,kwa nini tusitumie ARV kukiua kirusi iko kwa sifa nilizozitaja hapo juu,

Kwa Wamama wajawazito ni shida sana ukipata kirusi cha corona kwa kuwa kinga ya mwili inakuwa imeshuka na kirusi iko kitakushambulia kwa urahisi zaidi na kukushinda,kwa mtu mwenye kinga ya mwili imara hana shida maana kinga ya mwili ina uwezo wa kukipiga na kukiua,ila kwa wenye kisukari na magonjwa mengine yenye kushusha kinga ya mwili,kirusi cha corona kikiingia kinakwenda kugandisha damu,shida ya damu kuganda,utapowekewa mtungi wa oxygen 100% ikiingia mwilini mashine itasoma 70 kurudi chini maana oxygen inatopaswa kubebwa na damu,haitabebwa tena kuzungushwa sehemu mbalimbali za mwili,hivyo basi kusababusha vifo vya wapendwa wetu,

Tukumbuke barakoa zinazotoka Ulaya nazo zimeanza kuleta allergies za mafua na kupiga chafya,muhimu tuwekeze kwenye kinga ya mwili,tengeneza juice ya mboga mboga,changanya vitu viwili tu either karoti na mchicha au matembele na karoti,Mungu analo kusudi hadi pale mataifa yote yatapopiga magoti mbele zake ndipo dawa itapatikana,kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimpulizia pumzi ya uhai puani na ukajengeka mfumo wa upumuaji katika mwili wa binadamu,yeyote atae jaribu kuharibu mfumo huo,hiyo ni vita yake na Mungu aliyetengeneza mfumo wa upumuaji katika mwili wa Binadamu.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Leslie Mbena,
Dar es Salaam.
0755078854.

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Labda kwa kutusaidia wengine ,hapa mada ni kama ya kitabibu zaidi,tusaidie majibu ya maswali uliyoanza nayo ili na tusio na uelewa wa kitabibu tuweze kushiriki ipasavyo.
 
Chanjo hiyo haitakuwa na maana maana kirusi kitajigeuza tena?
 
Huelewi maana ya hizi nucleic acids (NA) DNA na RNA.. DNA ni common nucleic acid kwa animal cells na RNA mostly ni nucleic acid inayopatikana kwenye plant cells.

virus ni RNA.. anapoingia mwilini anakwenda kwenye nucleus.. anatulia anamsoma DNA anavyofanya kazi ... anajitengeneza/anajibadili/replicate kama DNA ilivyo (sifa kuu ya virus ni uwezo wa kujibadili kama kinyonga akiwa eneo lenye rangi ya kijani au njano, nyekundu, blue nk na yeye anakuwa hivyo ili asionekane kirahisi). Baada ya kutengeneza copy ya DNA anakuwa active na kuchukua kazi ya DNA nakufanya kazi zake kinyume na utaratibu wa kawaida ndio hapo dalili zinaanza.

Kila cell ina kazi maalum (specific) mfano puani ni maalum kwa kunusa, ulimi (ladha), mapafu, ini, figo, utumbo, nyayo zina kazi moja tu.. corona virus anashambulia mfumo wa hewa tu.

Nimejitahidi kueleza kifupi sana kwa lugha nyepesi kiujumla jumla
 
Huelewi maana ya hizi nucleic acids (NA) DNA na RNA.. DNA ni common nucleic acid kwa animal cells na RNA mostly ni nucleic acid inayopatikana kwenye plant cells...
Upotoro mwingine kutoka kwa ''mtaalam'' wa kiafrika. Maneno meeeeeeengi, vitendo sifuri. Njaa zenu mbaya sana. Anyway mmeshamjua anayewateua huwa anataka watu wajinga wajinga ili awa-control ndiyo maana mna act ujinga.
 
Upotoro mwingine kutoka kwa ''mtaalam'' wa kiafrika. Maneno meeeeeeengi, vitendo sifuri. Njaa zenu mbaya sana. Anyway mmeshamjua anayewateua huwa anataka watu wajinga wajinga ili awa-control ndiyo maana mna act ujinga.

Hoja yako ni ipi. Badala ya kueleza hoja iliyoko mezani, unaanza kumnanga mtoa hoja. Ni shida kweli.
 
Hoja yako ni ipi. Badala ya kueleza hoja iliyoko mezani, unaanza kumnanga mtoa hoja. Ni shida kweli.
Hakuna hoja hapo. Ni upuuzi mtupu. Huu uanana sayansi wa maneno hautupeleki popote. Yule naibu waziri wa afya kilaza anadai ni mwanasayansi, Magufuli naye nilisikia siku moja anajigamba ni mwanasayansi.

Uana sayansi wao mbona hawaunyeshi ukaonekana kwa vitendo. Wenzetu wako wanafanya tafiti, wanatengeneza chanjo, wanahangaika na kila kitu sisi huyu mjinga anakuja kuwa-challenge watu wenye akili waliotumia muda na kila aina nyenzo kwa maandishi ya kipumbavu kabisa. Njaa zake za kutafuta vyeo tu hakuna zaidi.
 
Km who imejirizisha na hyo chanjo nyie tz n nani mkatae? Chanjo inayotolewa ulaya na inayoletwa afrika inatofauti gani? Km hyo chanjo n mbaya inamaana wazungu wameamua kujiangamiza? Chanjo iletwe itumike kwa hiari kwa wanaotaka!
 
Hakuna hoja hapo. Ni upuuzi mtupu. Huu uanana sayansi wa maneno hautupeleki popote. Yule naibu waziri wa afya kilaza anadai ni mwanasayansi, Magufuli naye nilisikia siku moja anajigamba ni mwanasayansi. Uana sayansi wao mbona hawaunyeshi ukaonekana kwa vitendo. Wenzetu wako wanafanya tafiti, wanatengeneza chanjo, wanahangaika na kila kitu sisi huyu mjinga anakuja kuwa-challenge watu wenye akili waliotumia muda na kila aina nyenzo kwa maandishi ya kipumbavu kabisa. Njaa zake za kutafuta vyeo tu hakuna zaidi.
Punguza mihemuko soma vizuri nilichoandika, nimempinga huyo jamaa kwa upotoshaji wake kuhusu virus
 
Km who imejirizisha na hyo chanjo nyie tz n nani mkatae? Chanjo inayotolewa ulaya na inayoletwa afrika inatofauti gani? Km hyo chanjo n mbaya inamaana wazungu wameamua kujiangamiza? Chanjo iletwe itumike kwa hiari kwa wanaotaka!
Tunakazi kweli kutengeneza ubongo wa waafrica ukae sawa.kweli bado safari ni ndefu.watu wenye mitazamo Kama yako,ni mzigo kwenye hili bara la Africa,ambalo hata hao wazungu wanalitolea udenda kila siku. AFRICA YOU HAVE A LONG WAY TO GO.
 
Hakuna hoja hapo. Ni upuuzi mtupu. Huu uanana sayansi wa maneno hautupeleki popote. Yule naibu waziri wa afya kilaza anadai ni mwanasayansi, Magufuli naye nilisikia siku moja anajigamba ni mwanasayansi. Uana sayansi wao mbona hawaunyeshi ukaonekana kwa vitendo. Wenzetu wako wanafanya tafiti, wanatengeneza chanjo, wanahangaika na kila kitu sisi huyu mjinga anakuja kuwa-challenge watu wenye akili waliotumia muda na kila aina nyenzo kwa maandishi ya kipumbavu kabisa. Njaa zake za kutafuta vyeo tu hakuna zaidi.
Tulia wewe,Uchumi wetu utakapofikia kiwango cha high middle income country mwaka 2025 bila shaka tutakuwa na maabara zetu wenyewe za uhandisi wa vinasaba (genetical engineering laboratories) za kiwango cha kimataifa kama zile za BioNTech ya ujerumani iliyohusika kutengeneza chanjo ya Pfizer au ile ya Oxford University iliyohusika kutengeneza ile chanjo ya AstraZeneca.

Ngoja kwanza tumalize bwawa la umeme la Nyerere na SGR ya umeme. Yanayokuja yanafurahisha. Vuta subira. Roma haikujengwa siku moja. Ngosha bado tunaye.
 
Km who imejirizisha na hyo chanjo nyie tz n nani mkatae? Chanjo inayotolewa ulaya na inayoletwa afrika inatofauti gani? Km hyo chanjo n mbaya inamaana wazungu wameamua kujiangamiza? Chanjo iletwe itumike kwa hiari kwa wanaotaka!
.."Tafiti Ili kupata chanjo/tiba kwa kawaida ina hatua nne, kila moja sio chini ya miaka 03 kwahiyo mpaka utafiti ukamilike sio chini ya miaka 10....ndio maana chanjo hii haina majibu kwa sababu majaribio hayakukamilika wanaotumia hii chanjo wanaingia katika majaribio tu..."

Ndio nimeondoka nayo hii toka kwa Prof. Mgaya (NIMR)
 
Vile huoni aibu kusoma wikipedia na ambayo hukuilewa kwa 100% na kukimbilia hapa? Sababu ya buku saba? Hapa hupati tuzo kama ya utalii Morogoro. Hapa ni sayansi baba sio hizo blah blah. Clinical virologist angesahihisha bandiko lako kwa upendeleo angekupa alama 15%. Kukutia moyo kuwa ulifanya assignment ya kusoma lakini yamekuzidi kimo. Istilahi imekupiga chini sana.

Mwili wa binadamu una chromosomes 46. Chenye chromosomes 23 katika mwili wa binadamu ni mbegu za kiume na mayai ya kike tu. Kazi ya meiosis hiyo! Lengo likiwa mbegu na yai vikiungana ndipo upate 46. Hili ndilo jambo rahisi sana katika genetics. Limekupiga chenga. Yale yenyewe kwako ni sifuri. Kumbuka hapa huwaandikii mataga. Kuna watu hapa wana taaluma zao wapo kimya!
 
Asante mleta mada, moderators wa JF wakutendee haki, uzi upelekwe panapostahili. JF Doctor forum.
 
Tunakazi kweli kutengeneza ubongo wa waafrica ukae sawa.kweli bado safari ni ndefu.watu wenye mitazamo Kama yako,ni mzigo kwenye hili bara la Africa,ambalo hata hao wazungu wanalitolea udenda kila siku. AFRICA YOU HAVE A LONG WAY TO GO.
Na ndio maana tunatukanwa waafrica, kumbe ni kutokana na watu kama hao
 
Yawezekana kwamba wazungu wanatumiwa kama "control" kwenye ammo hmajaribio haya ya chanjo. Wao Wanachanjwa placebo!

Halafu waafrika ndio wanafanyiwa majaribio kwenye hii chanjo. Ndiyo maana chanjo ya awamu hii imelenga kuchanja asilimia 20 tu ambazo hazitoshi kufikia herd immunity ambayo hufikiwa kwa watu asilimia 60 kuwa na Kinga!
 
Mkuu, Kwani shemeji yetu ameshapona changamoto zetu?

Ama na wewe zilikuandama kwa kupata maambukizi.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom