Je, kiprotokali Mkuu wa Majeshi (CDF) atampigia salute Meja Generali?

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
232
500
Habari, Juzi Mh. Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan ameteua wakuu wa mikoa wa mikoa yote ya Tanzania bara na miongoni ya walioteuliwa ni aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja General Charles Mbuge kuwa mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brigedia Generali Marco Kaguti ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mara nyingi kwenye ziara za viongozi wakuu wa Serikali, hususani Mh. Raisi, huwa anaambatana na viongozi wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuanzia CDF, IGP, DGTISS, Commissioner wa Magereza, Uhamiaji, Commissioner wa Jeshi la Zimamoto, Mkuu wa PCCB na Mkuu wa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya huko mikoani ili kuthibitisha uwepo wa kiongozi mkuu wa nchi.

Nimeshuhudia mara CDF, General Venance Mabeyo, akiwapigia salute "viongozi wa kisiasa" hasa wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya mfano nilikuwa Kisarawe kupitia TV wakati wa ziara ya "Mwendazake" akizindua mradi wa maji nakushuhudia CDF, General Mabeyo, akimpigia salute Mkuu wa Wilaya hiyo, Miss Joketi Mwegelo. Hili kwa viongozi hawa ambao siyo Askari sidhani kama linashida sana (Ingawa halileti maana vipi IGP AU CDF ampigie Salute raia - but sio mada yangu kwa leo so tuachane nayo) ila shida naiona itakuwaje siku CDF ambaye ni General akiwa Kagera atampigia Salute Mkuu wa Mkoa huo ambaye ni Meja General? Hii imekaaje wanajukwaa au Meja General atampigia Salute Mkuu wake, hapa hata sielewi?

Asante.
 

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
2,171
2,000
akivaa kiraia huyo mkuu wa mkoa atapigiwa salute! akivaa kijesh atapga yeye kwa CDF

ila sjaona hata mmoja aliye kwenye system bado akavaa kiraia wakati ujio wa RAIS au CDF mkoan kwake


picha ambazo JPM yupo ujue na CDF alikuwepo! na uvaaji wa mkuu wa mkoa huyu wa Kagera na sasa Mtwara ni kijesh

Do-i6VlWwAAupmS.jpg


images (1) (9).jpeg


images (1) (8).jpeg
 
May 7, 2021
22
75
Kuna mkuu wa wilaya sajenti,aliteuliwa na JPM,je mshauri wa mgambo wa wilaya ambaye anaweza kuwa meja anampigia saluti afande sajenti DC?
 

kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,905
2,000
chuo cha diplomasia wanatoa short course ya protocol nendeni mkajifunze
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom