Je kipi/nini kifanyike kusudi rasilimali mikoani zinufaishe wananchi wa maeneo husika pia?

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,819
8,884
Wakuu,

Nataka tujikite kwenye hili swala la maendeleo na uwiano wa uchangiaji kwenye pato la taifa. Kwa mda mrefu sasa, hili swala tumekua tukilikwepa hata kulizungumzia. Kwa wananchi na serikali pia. sababu kubwa ikiwa ni kulinda mshikamano wa kitaifa na kudhibiti ukabila. Mfano leo tunaambiwa Shinyanga ni ya nne kwa uchangiaji kwenye pato la taifa.

Wakati huo huo wananchi wa Shinyanga ni masikini wa kutupwa. Kinyume chake mkoa kama Arusha au Kilimanjaro wananchi wake wana hali nzuri kimaisha na imeendelea kulinganisha na mikoa mingine lakini uchangiaji wao kwenye pato la taifa hauendani na hali yake kimaendeleo. Lakini vile vile ukweli unabaki kwamba wananchi wa hii mikoa ni wapambanaji pia. Lakini pia mkoa kama Pwani...wanafaidika sana (especially kipindi hiki) though its contribution does not reflect what it takes from the pot.

Swali langu kubwa ni nini kifanyike? Kuhakikisha rasilimali zilizo kwenye mikoa husika zinawanufaisha hata wale raia wa hiyo mikoa? mf. ukienda Kilimanjaro utaona ni namna gani raia wameamka katika kutumia fursa za utalii. Hivyo hivyo Arusha. Sasa tujiulize swala la maendeleo ni juhudi za serikali au wananchi wa mkoa/sehemu husika?

Kipi kifanyike? Kuhakikisha dhahabu ya Shinyanga Inanufaisha taifa lakini wanashinyanga wakipewa kipaumbele pia? au Samaki wa Mwanza au gas ya Mtwara??? Maana mimi naona kama tunaahirisha matatizo. Kama mlivyoona swala la gesi kidogo tutoane roho.

And for sure Mtwara wamekumbukwa kwa sababu ya hii gesi. Itakuwaje wananchi wakiamka wakaanza kudai wanufaike na rasilimali zao? Nini wajibu wetu sisi Raia? Nini wajibu wa serikali yetu?

Naomba tutoe ushauri chanya hata wakubwa kwenye taasisi husika wanaweza pitia humu wakapata moja au mawili.
 
Jibu ni rahisi,ondoeni kwanza CCM,imekuwepo miaka mingi lakini inawaona wananchi wa Shinyanga ni mazuzu,former AG bw Chenge anatoka Shy ya zamani alishiriki kuwadhulumu ndg zake,btw unaifahamu sera ya Serikali za Majimbo ya CDM?huo ndio msingi wa kuanzia!
 
lazima kuwe na formula ya ugawanaji wa pato la taifa mikoani/wilayani. isiwe rais au waziri anagawa pesa za maendeleo anavyojisikia.
 
rasilimali kubwa ni rasilimali watu maendeleo yanaletwa na watu hizi figisu unazoleta ni excuse za kuonesha hatujakosea sana. Watu wakiendelea utaona maendeleo yanavyokimbia, kaskazini watu wao walipiga hatua kitambo lakini hawajatuzuia na sisi tusiendelee.

Dhahabu, almasi na vingine ni kuwapumbaza watu wasijione wao ni rasilimali. Hiyo migodi mikubwa mnayotaka kila mtu aone anahusika nayo ni mali ya watu wachache sana. Watu waone fursa sasa, punguzeni idadi ya wanasiasa tuwe na watu katika ujasiriamali wenye tija uone maendeleo. Tunaanzia kidogo kidogo baadae tutakuwa kama wao.

Wakuu,

Nataka tujikite kwenye hili swala la maendeleo na uwiano wa uchangiaji kwenye pato la taifa. Kwa mda mrefu sasa, hili swala tumekua tukilikwepa hata kulizungumzia. Kwa wananchi na serikali pia. sababu kubwa ikiwa ni kulinda mshikamano wa kitaifa na kudhibiti ukabila. Mfano leo tunaambiwa Shinyanga ni ya nne kwa uchangiaji kwenye pato la taifa. Wakati huo huo wananchi wa Shinyanga ni masikini wa kutupwa. Kinyume chake mkoa kama Arusha au Kilimanjaro wananchi wake wana hali nzuri kimaisha na imeendelea kulinganisha na mikoa mingine lakini uchangiaji wao kwenye pato la taifa hauendani na hali yake kimaendeleo. Lakini vile vile ukweli unabaki kwamba wananchi wa hii mikoa ni wapambanaji pia. Lakini pia mkoa kama Pwani...wanafaidika sana (especially kipindi hiki) though its contribution does not reflect what it takes from the pot.

Swali langu kubwa ni nini kifanyike? Kuhakikisha rasilimali zilizo kwenye mikoa husika zinawanufaisha hata wale raia wa hiyo mikoa? mf. ukienda Kilimanjaro utaona ni namna gani raia wameamka katika kutumia fursa za utalii. Hivyo hivyo Arusha. Sasa tujiulize swala la maendeleo ni juhudi za serikali au wananchi wa mkoa/sehemu husika?

Kipi kifanyike? Kuhakikisha dhahabu ya Shinyanga Inanufaisha taifa lakini wanashinyanga wakipewa kipaumbele pia? au Samaki wa Mwanza au gas ya Mtwara??? Maana mimi naona kama tunaahirisha matatizo. Kama mlivyoona swala la gesi kidogo tutoane roho. And for sure Mtwara wamekumbukwa kwa sababu ya hii gesi. Itakuwaje wananchi wakiamka wakaanza kudai wanufaike na rasilimali zao? Nini wajibu wetu sisi Raia? Nini wajibu wa serikali yetu?

Naomba tutoe ushauri chanya hata wakubwa kwenye taasisi husika wanaweza pitia humu wakapata moja au mawili.
 
rasilimali kubwa ni rasilimali watu maendeleo yanaletwa na watu hizi figisu unazoleta ni excuse za kuonesha hatujakosea sana. Watu wakiendelea utaona maendeleo yanavyokimbia, kaskazini watu wao walipiga hatua kitambo lakini hawajatuzuia na sisi tusiendelee.

Dhahabu, almasi na vingine ni kuwapumbaza watu wasijione wao ni rasilimali. Hiyo migodi mikubwa mnayotaka kila mtu aone anahusika nayo ni mali ya watu wachache sana. Watu waone fursa sasa, punguzeni idadi ya wanasiasa tuwe na watu katika ujasiriamali wenye tija uone maendeleo. Tunaanzia kidogo kidogo baadae tutakuwa kama wao.
unataka kusema kaskazini watu walitoa pesa zao mfukoni na kujenga lami, kupeleka umeme na kuweka mirasdi ya maji?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom