Je, kinachoendelea nchini kwa matukio ya baadhi ya watendaji wa Serikali na viongozi wetu wa CCM ni kwa ajili ya kumsadia Rais au kuna ajenda ya siri?

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
220
250
Nasema hivi kwa sababu kuna kila dalili za baadhi ya watendaji wa serikali wamebeba ajenda zao za siri na wanawatumia baadhi ya watendaji viongozi kuwashauri vibaya au kuwarubuni kwa kutumia udhaifu wao hao viongozi kwa kuwaamini.

Hii inatokana labda na utendaji wao wa awali walijiaminisha kwa utendaji wao sasa wanatumia hali hiyo kuaminiwa kumshusha au kumuharibia..Pia ndugu zangu wanaCCM hamna kipindi ambacho tunatakiwa kutuliza akili na kuongea kwa staha bila kuvipa vyombo vya ulinzi njia panda kama wakati huu.Wakati naouzungumzia sio wa utawala wa awamu ya tano ila wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa mapinduzi makubwa ya hii miaka 10,awamu ya nne hili kwao limekuja mwishoni ila awamu ya tano na awamu zote zifuatazo watakuwa nalo kipindi chao chote.

Hii ina maana gani tachague sehemu za kuongea na tusiaminiane sana hata kama wote tumevaa kijani.Baadhi yetu wamejaa ajenda za siri wanazozijua wao,hivyo hufumua baadhi ya mambo au kunena alafu hujificha kwa mwavuli wa chama. Wasomi wanaongezeka kila leo na wananchi wanazidi kuelimika kila leo,wanahifadhi matamshi yetu pia wapashana habari juu ya matamshi yetu au vitendo vyetu kwa haraka sana na pia huyachambua na kuyajadili kwa makundi vijiweni,makazini mpaka mitandaoni.

Hivyo sio kila mtendaji wa serikali au chama anaporoka au kutenda vile isivyo au kinyume na sheria kwa kisingizio cha kumlinda Mh. Rais kwamba ni mwenzetu au anauchungu na nchi kama Mh. Raisi wa awamu hii,wengi wanatumia udhaifu huu na njia kumuharibia kwa makusudi kwa kuwa wanajua wengi wetu hatutajua nia yao na lawama hazitakwenda kwao ila zitaenda kwa mlengwa wao.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,352
2,000
We unaamini hao niliowataja hapo,wanayoyafanya hajui kwamba wanaharibu kwa kisingizio cha uzalendo?
Ukiitazama hoja yako kwa angle tofauti ni lazima uhitimishe kuwa, hakuna namaanisha hakuna mwanaccm hata mmoja anayemsaidia mwenyekiti wao kwa namna yoyote ile! Ona matendo yao, hotuba zao zisizo na mpangilio, ona miswada ya sheria wanazozipeleka bungeni na jinsi wanavyozipitisha kizima moto (kikotoo), ona uhamasishaji ulivyodumaa na jinsi wasivyojali anguko la uchumi ( $= 2500tshs)!
Ni kama wamemsusia nchi either kwa kuwa maslahi yao yamebanwa na au wapo mkao wa fisi kusubiri kudondoka kwa mkono wa binadamu!
Mkulu lazima alione hili ili ajitune either kwa kuwashirikisha zaidi anaowaita wapinzani kwani wengi wa waliopo kwenye chama chake wanaiishi kauli ya Mwl. Nyerere kuwa, upinzani wa kweli utatoka ccm! Na wanasubiri!
 

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
220
250
Me binafsi bado naendelea kusisitiza kwa haya yanayoendea nchini,lazima kutakuwa na ajenda ya siri iliyopangwa ikapangika vizuri...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom