GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwa haya nitakayoyaandika hapa simlazimishi Mtu yoyote akubaliane nayo japo ningependa mtulize akili zenu kiumakini kabisa ili muweze kupima kisha mwishoni tunaweza kuelewana lakini pia nitafurahi nikipata changamoto ila iwe ni yenye tija na siyo ya kuharibu kwani yawezekana kupitia huu uzi wangu tukaweza kusaidia kabisa kulimaliza hili tatizo kubwa.
MTIZAMO WANGU WA AWALI
Nilichokigundua hapa ni kwamba yawezekana kuna mazalia ya Watendaji ambao pengine hawakupenda au kumtaka Kiongozi wetu Rais Dkt. Magufuli awe hapo alipo sasa hivyo kupitia uzoefu wao mkubwa ndani na nje ya nchi huku wakipata misaada kutoka kwa nchi au mataifa Rafiki wanaweza kuyafanya haya tunayoyaona sasa. ( hii naipa 20% tu )
MTIZAMO WANGU WA PILI
Nilichokigundua hapa ni kwamba ( na nalihisi hili ndilo linaweza kuwa kubwa kuliko ) yawezekana Watendaji wa hiyo Idara hasa wale wa juu kabisa hawakupendezwa na Uteuzi wa DG na DPG wake kwakuwa waliteuliwa kutokea maeneo mengine huku wale ambao walikuwepo Idarani kabisa na ambao walikuwa wakipigiwa chapuo na Former DG wakiachwa huku wengine wakitupwa mbali kuwa Mabalozi na wengine wakisubiri kupangiwa Vituo vipya vya Kazi.
Nimeenda mbele zaidi hapa na nikagundua kuwa yawezekana kabisa haya matukio ya ajabu ajabu ambayo tunayasikia na hata kuyashuhudia sasa yakawa yanaratibiwa kwa 100% na wale waliokuwa wakitegemea kuteuliwa Wao kuwa Ma DG na Ma DDG wa Idara hivyo kutokana na uzoefu wao mkubwa ndani ya Idara wameweza kujiundia Kikosi chao ambacho pengine kimewahusisha wale Watendaji ( Wafanyakazi ) ambao walikuwa ni Watiifu Kwao.
Nimegundua kuwa pia kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Wakubwa wale waliochukia kutokuteuliwa wao kuwa Ma DG na Ma DDG wa Idara wakawa wamejiundia Kikosi fulani cha hatari hivyo Kazi yao kubwa sasa ni kufanya hayo wanayoyafanya ili kuleta Hofu nchini kisha kumwaribia DG na DDG wa sasa wa Idara halafu Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli ahamaki na afanye mabadiliko haraka ili ile dhana ya tukose wote itimie.
Najua fika kuwa DG na DDG wote ni wana Idara Kitambo sana ILA nina uhakika usio na shaka kuwa siasa za ndani ya Idara ya kupenda madaraka, undugu na uswahiba wao walikuwa hawaijui hivyo basi uwepo wake yeye hapo tena akitokea NIDA kama Mtaalam tu wa IT kunaweza kumfanya aonekane kuwa amewekwa tu hapo hivyo wale aliowakuta ambao hujiita kuwa ndiyo wenye Idara na ambao nahisi wako wengi wakaamua Watoto wa mjini wanasema ' Kukichafua ' au ' Kukinukisha ' ili tu kuwakomoa na kuwachafua ( hii naipa 70% tu )
MTIZAMO WANGU WA TATU
Hapa pia nimegundua kuwa yawezekana kuna Kiongozi mmoja kutokana na uwezo wake hata wa Kielimu tu kuwa mdogo kama siyo wa mashaka mashaka japo Kiutendaji anaweza akawa yupo vizuri kutushinda hata sisi tunajiita kila siku kuwa ni Wasomi ameingizwa katika huu Mtego bila yeye kuushtukia.
Kutokana na Mamlaka yake kama Mwenyekiti wa Kamati nzima ya Ulinzi n Usalama wa Mkoa inawezakana kabisa kuwa akawa amepenyezewa Watu wabaya na wenye ama Uadui na Mheshimiwa Rais wetu JPM au wenye chuki na uteuzi mzima wa current DG na DDG wa Idara kwa sasa ambao hujitahidi kumpa maelekezo ya Kichuki na ya Kiuchochezi huyo Kiongozi wa Mkoa ambapo na yeye kwa kutokuwa na uwezo mkubwa wa Kujiongeza na yeye anajikuta akiingia ' kichwa kichwa ' na kufanya mambo ambayo hutushangaza wengi lakini kwa wale wana Usalama wanaomzunguka vitendo vyake huwa ni ushindi mkubwa Kwao kwani malengo yao huwa yanatimia ( hii naipa 10% tu )
Wana JamiiForums wenzangu huo ni mtizamo wangu tu juu ya mambo yanayoendelea sasa nchini Kwetu na napenda nanyi pia mjumuike nami katika kuyatizama haya na kuyachambua zaidi ila nitapenda pia kama nikipata changamoto za Kiueledi na za Kihoja zaidi kwani ningependa uzi huu wangu uweze basi angalau kusaidia kuelezea nini kinaendelea zaidi ili kama vipi basi michango yetu iweze kuisadia nchi yetu. Pia niwaombe kuwa katika kulijadili hili tuepuke sana kuweka au kuingiza Siasa zetu za Kichama au hata Udini au Ukabila bali tulijadili kama Watanzania na tujikite zaidi katika kutafuta suluhu au ufumbuzi wa kimantiki na wa kujenga kabisa.
Huko nyuma niliwahi kuanzisha humu uzi wa kuwataka Watu wa Idara kuwa wajitokeze haraka kuyazungumzia haya lakini kwa masikitiko makubwa kama siyo kunipuuzia hilo halikufanyika na hatimaye sasa Idara ndiyo inazidi tu kuchafuliwa na tararibu sana Heshima ya Idara inaanza kupotea na karibuni itaanza kudharaulika. Muwe mnasikiliza ushauri wetu kwani kuna wengine hapa duniani zawadi pekee tuliyopewa na Mwenyezi Mungu ni kuwa tu na maono ya mbali sana, kushauri na kutoa tahadhari hivyo Watu wa Idara msiwe mnapuuza maoni ya Watu humu JF na ninaamini laiti mngekuwa mnayafanyia uchambuzi haya yanayosemwa humu na kubadilika leo nchi ingetulia kutoka katika hofu hii juu yenu na hata mtizamo wao wa sasa hasi kwa Kiongozi wao Mkuu wa nchi na hata wa Mkoa ikiwezekana.
Yangu ni hayo tu na naomba kuwasilisha.