Je, kila tajiri hapa Bongo anatumia ndumba (kafara, majini, uuaji n.k)?

Zee Korofi

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,612
1,410
Kama kichwa kisemavyo, nimesoma historia za utajiri za baadhi ya matajiri wakubwa mno hapa TZ, nilikuwa na ndoto za kuwa tajiri kwa kufanya kazi na kutumia weledi mkubwa, ila nimekatishwa tamaa na ukweli unaoonekana kuwa wazi.

Kwanza kabisa niliwahi kukaa na mzee mmoja tukipiga stori, akaniambia kijana ukikua utaelewa nini maana ya utajiri, na hutoutaka tena.

Pia historia na mifano mbali mbali inanikatisha tamaa mno, mimi si mtu wa ndumba namtegemea Mungu TU katika ulinzi wangu ila kuna watu wanasema SIWEZI KUWA TAJIRI KWA KUMTEGEMEA MUNGU PEKEE.

Hii inakuwa vipi? Kwani siwezi kuwa tajiri hapa Bongo bila hizo mambo? Mbona kukatishana tamaa huku?
 
Mkuu kwenda kwa mganga kutaka eti uwe tajiri hamna kitu, maana hata wao wenyewe wanataka wawe matajiri na mbona hawajakua?

Jitihada yako na Mungu alivyokuandikia uwe ndio hivyohivyo, wengine utajiri wameupata kwa kurithishwa na family zao yaani wameukuta wanakuja kuundeleza tu
 
Simamia kile unachokiamini. Hakuna tajiri alowah kukiri kutumia ndumba kwenye kuzisaka. Na hakuna tajiri asiyejua ndumba. Na kama yupo anatumia ndumba, na kama hatumii alitumia ndumba. Na kama hakutumia, anatumia ndumba.
 
Mkuu kwenda kwa mganga kutaka eti uwe tajiri hamna kitu, maana hata wao wenyewe wanataka wawe matajiri na mbona hawajakua??
Jitihada yako na Mungu alivyokuandikia uwe ndio hivyohivyo, wengine utajiri wameupata kwa kurithishwa na family zao yaani wameukuta wanakuja kuundeleza tu
Mbona kuna mapasta wanakuombea upone ugonjwa ilihali wao wanaumwa balaa😀
 
Simamia kile unachokiamini. Hakuna tajiri alowah kukiri kutumia ndumba kwenye kuzisaka. Na hakuna tajiri asiyejua ndumba. Na kama yupo anatumia ndumba, na kama hatumii alitumia ndumba. Na kama hakutumia, anatumia ndumba.
Tungo tata hiyo. Naogopa makafara, so kwenye hizo ndumba kunahusisha makafara?
 
Utajiri una maana nyingi sasa sijui utajiri gani unaongelea hapa.
Utajiri gani unaongelea?

Mafanikio wanapata watu wenye akili pekee na mtu anaeamini kufanikiwa kwa kwenda kwa mganga pia kuamini uchawi definitely hana akili.
na hao unaoona ni matajiri kwa uchawi sio matajiri bali ni wabangaizaji tu wenye uwezo wa kubadirisha mboga.
au wataje hapa tuone kama kuna yoyote anawajua..?

so umeshapata jibu hapo.
 
Kwa unaeamini anamtumia Mungu kupata utajiri, siku utakapojua kilichompatia utajiri utashangaa , ninakusihi tu ridhika na unachopata. Jua tu Mungu hana upendeleo, ampe huyu amnyime huyu! Ni maujanja tu ya binadamu.
 
Kama kichwa kisemavyo, nimesoma historia za utajiri za baadhi ya matajiri wakubwa mno hapa TZ, nilikuwa na ndoto za kuwa tajiri kwa kufanya kazi na kutumia weledi mkubwa, ila nimekatishwa tamaa na ukweli unaoonekana kuwa wazi.

Kwanza kabisa niliwahi kukaa na mzee mmoja tukipiga stori, akaniambia kijana ukikua utaelewa nini maana ya utajiri, na hutoutaka tena.

Pia historia na mifano mbali mbali inanikatisha tamaa mno, mimi si mtu wa ndumba namtegemea Mungu TU katika ulinza wangu ila kuna watu wanasema SIWEZI KUWA TAJIRI KWA KUMTEGEMEA MUNGU PEKEE.

Hii inakuwa vipi? Kwani siwezi kuwa tajiri hapa Bongo bila hizo mambo? Mbona kukatishana tamaa huku?
Mkuu sijui umri wako ila inaonesha wewe ni mdogo sana kati ya 20 na 24 pia muandiko wako unaonesha una uelewa mdogo sana kuhusu ukweli wa dunia bado uko kwenye giza la fantasy ambamo watu wengi wamo ndani yake.

Nikianza kuandika hapa itakuwa ngumu kuelewa hivyo nakushauri soma sana na tafuta maarifa mengi ya kidunia kadri unavyoweza ili ujue reality ilivyo na dunia inavyoenda nje ya hapo mtaani kwenu na kijiweni. namaanisha (kusoma mambo ya maana kuhusu dunia, mambo ambayo yanahitaji matumizi ya akili)

Unahitaji exposure kubwa kuweza kupanua uwezo wako wa akili na maarifa hivyo kuweza kukutoa kwenye hilo giza la fantasy na kuja kwenye reality.

Baada ya muda kupita utakuja kufuta hii mada.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom