Kuna vita za nguvu mbili tu ulimwenguni, wema na ubaya. MUNGU kakupa mamlaka ya kuushinda ubaya kwa wema, Hiyo nguvu ya kuushinda wema inatoka kwa kwa mwingine. Unapoushinda wema kwa kutumia ubaya maana yake ni kuwa yule mwingine amekuwezesha na umeshinda. Unaposikia kuwa palikuwa na vita mbinguni maana yake ni kuwa wapo walioamini wanauwezo wa kumwangusha MUNGU. Na mawazo ya kupigana na MUNGU mbegu yake huanzia hapo hapo kwenye swali ulilouliza la MUNGU anaweza kweli? Ukishajiuliza uliza kinachofata yule anayetoa nguvu za kuushinda wema atakupa nguvu za kutosha na utashinda.kwa hiyo;
MUNGU anayeweza kukupa mamlaka na bado mamlaka hayo yakapingwa na kiumbe kingine?
kama jibu ni NDIO kwa hiyo mungu anaweza mengi na sio yote?
kama jibu ni HAPANA hao wafalme wa uajemi walipata wapi nguvu ya kumpinga malaika alietumwa na MUNGU mpaka siku 21 zinapita?