Je Kila mtu anaruhusiwa kugombea ubunge au tabia pia inaangaliwa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kila mtu anaruhusiwa kugombea ubunge au tabia pia inaangaliwa??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Papizo, Jul 6, 2010.

 1. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kwa ujumla sielewi sheria gani zinachukuliwa mtu akitaka kugombea ubunge,Labda mtu yoyote yule anaweza kwenda kuchukua form na kujaza basi,Sidhani kama kuna sheria zozote zinaangaliwa kama background na tabia pia.

  Kwa ujumla huyu jamaa naona kama hana nidhani kabisa na wala hapaswi kugombea ubunge kwa chama chochote kile,si mfahamu wala sina mawasiliano nae ila naona kama hana nidhamu na hana maadili hata kidogo,Nadhani ukicheck huo wimbo wake hapo chini ndio tutaona kama ana akili kidogo na je akiingia bungeni ataongea nini cha maana??Sielewi ila naona hafai kugombea ubunge kwa matusi aliyoimba kwenye huo wimbo wake,Sifikirii kabisa kama mtu na akili zake anaweza kuimba wimbo kama huu then aingie madarakani.

  Naamini nchi yetu inateketea na sisi wenyewe tuona na ni nani wa kuiokoa kama sio sisi??
   

  Attached Files:

 2. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sidhani kama umeshafika Dodoma kipindi cha Bunge ndugu yangu. Tabia? Nakushauri uende kule ukajionee uzinzi, usodoma na gomora, ulevi, wizi, ufujaji, dharau, kejeli, kashfa, uharibifu wa ndoa za watu, mabinti zetu na mauzauza mengine ambayo kama ni mtu mwenye haya na soni basi lazima utamwaga chozi. Kamwe usiongelee tabia njema na ubunge au wabunge katika sentensi au sehemu moja. Ni wachache sana ambao ni waadilifu.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa mmoja wa watoa rai kule kwene ile thread CHADEMA wakaja juu kama wamemwagiwa maji ya betriii..Lakini unategemea nini kwene taifa hili linalokufa kwa kasi??????
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwa nafsi yangu nakubaliana na wewe ...........lakini labda chadema wamemuacha agombee kwa kuwa wanajua hatapata.
   
 5. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wala hawezi kupata,......
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  rais, mbunge na diwani upewa ajira na wananchi; sheria za uchaguzi ziko wazi!
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kundi la watu wa aina yake nalo linahitaji kuwakilishwa Bungeni, hajakosea kutaka kugombea. Vinginevyo ukitaka asigombee mfungulie mashtaka kama unaona amefanya kosa, mahakama ikimtia hatiani kwa kosa la jinai atakuwa amekosa sifa. Kwa kuwa hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai, ana haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nadhani Sugu yupo frustrated alipaswa kutulia kwanza, nionavyo mimi akipewa madaraka makubwa wakati huu atalipa visasi kwa wabaya wake. Anyway anaweza ku-apologize na maisha yakaendelea.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sugu ana constituency yake kubwa inayofisadiwa na watu wanaolindwa na wafuasi wa ccm;ndio maana anataka ubunge ili apate mahala pa kuweza kuweka sauti yao iliyonyikani hivi sasa ili iweze kusikika.Nyie mnaosema hawezi huo Ubunge mnatumia vigezo gani? Kama mwanamuziki mwenzie Komba anaweza, Sophia Simba mpaka anakuwa waziri kwanini Sugu ashindwe? Hii nchi inaendeshwa kwa kisanii na ndio maana hata wanamuziki wakina Hadija Kopa na Asha Baraka ni wajumbe wa NEC ya ccm na hivi sasa wanashiriki kuchagua Rais wa Zanzibar Mtarajiwa!
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Watu kama Sugu ndo tunawahitaji! Jamaa ameongea ukweli bila woga, ndo tunachohitaji kwenye nchi hii! Matusi yana mahala pake duniani, safi kabisa alivyoyatumia.
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Yaani suala la tabia na sifa za wagombea wa nafasi za kisiasa haswa ubunge kama lipo basi ni ndanai ya makabrasha na makaratasi tu! haki ya nani tena!

  Naungana na PatPending ; tena Sugu ana afadhali kwani kama ni tabia ametuonyesha hadharani kuliko hizo nyingi za vificho na unafiki mkubwa za wengine amabao tayarai wanazo nafasi hizo!
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Naona post yako ni ya kumtunkana huyu jamaa, ugomvi wenu wa kwenue bongo flava uishie hukohuko. Besides wabunge waliopo wa ccm ni nani aliye bora zaidi ya huyu jamaa, ukiachilia Dr. J.P. Magufuli?
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kikatiba kila mtu anayetimiza masharti ya kuwa mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na rekodi yake nzuri (si mlalifu) anaweza kugombea na kuwa kiongozi. Zamani waliokuwa wanagombea nafasi za uongozi walikuwa ni wale wenye nia na moyo wa kuleta maendeleo. Kizuri zaidi ilikuwa hata uslama wa taifa walikuwa wanscreen ili kujua ni nani wanaweza kugombea nafasi za uongozi au wanastahili kuteuliwa kwenye nafasi za uongozi.

  Siku hizi uongozi unanunuliwa tu, ukiwa na hela basi unapeta, hata kama wewe huna lolote kichwani huna uzalendo kwa Tanzania. Unasikia wakati miwngine kutokana na mtu kuwa kimada wa fulani basi anapigiwa pande, kwa hiyo sasa ni kama kila mtu anaweza kuwa mbunge au hata kuteuliwa kuwa kiongozi.
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Nenda pale chako ni chako au saturday na kisha 84 night club dodoma ndo utaelewa uchafu wa hao wawakilishi wenu wa bongo, ni totoz kwa sana, kilevi pembeni na baadae usingizi mnono.
   
 15. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  huyu nae katumwa na wazee agombe?????manake wagombea wote wa Bongo wanaingia na gia ya kuombwa na Wazee.
   
Loading...