Je, kila kosa ni jk tu wa kulaumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kila kosa ni jk tu wa kulaumiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salimia, Mar 2, 2011.

 1. S

  Salimia JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nadhani tubadilike kidogo na kutomtupia Rais wetu lawama kwa kila jambo. Nchi inaundwa na wizara na taasisi lukuki zenye watu wenye majukumu mbalimbali ya kumsaidia Rais, directly or inderectly. Hawa wote sio Rahisi kwa Rais kuwafikia moja kwa moja, anao watendaji na wasaidizi wake ambao endapo hawatawajibika ipasavyo, kinachotarajiwa hakitatokea.
  Mathalani, tuna matatizo kweli ya kutegemea sana donors, na mara nyingine tunataka pia donors wafikirie maendeleo ya nchi yetu na twakubali mambo yote tunayoelekezwa tufanye bila kuyapima. (Hapa yupo anayewajibika na hili moja kwa moja). Mfano mzuri ni viwanda vilivyouzwa ovyo ovyo kwa kisingizio cha trade liberalisation , matokeo yake wawekezaji wenyewe kumbe hawakuwa na nia yeyote ya kuviendeleza...vingi kwa miaka mingi sasa (kabla hata ya
  JK) havifanyi kazi. Hofu yangu visije kutaifishwa tena! Tunawaamini sana donors ,world bank na wafanyabiashara na wawekezaji wa nje, ukweli ni kwamba mwekezaji yeyote awe China , Saudia ,Russia , UK au USA wote nia yao ni kuchukua rasilimali zetu nyingi iwezekanavyo ili wazipeleke kwao. Watu wanasema China wanakuja kusaidia maendeleo ya Afrika.This is totally naive and wrong!! China anashindana na marekani na nchi nyingine kuja kuchukua resources zetu nothing else...maendeleo ya Afrika yataletwa na waafrika wenyewe sio mtu mwingine. Uingereza majuzi imekataa ofa ya China kufanya ujenzi kwa project ambayo wenyewe waingereza waliiacha kwa kuona gharama ni kubwa sana..sasa wachina walitaka waijenge kwa gharama ya chini sana lakini Waingereza wamegoma!!hawataki kusikia!! Wenzetu wako macho wanajua kuwa kuna usanii katika mambo kama hayo.
  Kwa yote hayo,, JK peke yake bila msaada wetu kama Watanzania tunaoipenda nchi yetu, hataweza. Mwalimu alisema play your part, it can be done. Nasi badala ya kulalamika kutw humu,, lets play our part.
  Karibuni mnaojua kutukanana. Mimi napita fasta hapa.
   
 2. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Kikwete ni mbishi na siyo mtu wa kusikiliza wananchi wake na washauri wake ni washikaji wake ambao wengi wao hawakupiga buku wamegushi vyeti. kikwete hana upeo wa kufikiria hana akili. Asipo laumiwa Kikwete alaumiwe nani? wasaidizi wake? Kama wasaidizi wake wanavurunda anashindwaje kuwafukuza kazi ikiwa amewezakuwaajiri? Sisi Wananchi hatujaajiri waziri hata 1, Hao wote wameajiriwa na Kikwete na Kikwete ameajiriwa na Wananchi kwa kuchakachua kura zao sasa kwanini tuwalamikie wengine wakati Kikwete ndio aliyepewa dhamana na kuapa kuwa atalinda nchi yetu na rasilimali zetu. Kikwete anastahili Lawama zote zilizopo kwenye nchi yetu akubali akatae
   
 3. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Out of touch like jk
   
 4. S

  Salimia JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu, hujasomeka, unasema?
   
 5. w

  warea JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa tumlaumu nani?
  Mawaziri wote, wakurugenzi wote, makatibu wakuu wote, wakuu wa mikoa na wilaya wote, yeye kawateua na hataki kuwaondoa wakiboronga.
  Kazi kwake. Wala hajasema kazi inamlemea apunguziwe madaraka. Tena anapenda angeweza awachague na wa upinzani!
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sa alaumiwe nan?wewe umetoka mirembe?
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Holy Crap!
   
 8. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Mungu akusamehe,kwani hujui unalo ongea kuhusu Jk.Pia hujui kazi na majukumu ya Rais,Kwa taarifa yeye ni dereva wa nchi,hivyo anapaswa kuwa wajibisha wote walio chini yake kwa makosa wanayoyafanya.Ila huu ni usiku naona ukalale wenda akili zako kesho zitarudi.
   
 9. S

  Salimia JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndiyo mkuu natokea Mirembe, ndiyo maana nimesema napita fasta sana narudi huko tena.
  Tatizo la watanzania ni wavivu,, mtu anangoja maisha bora nyumbani anacheza karata, pool, bao na kunywa kahawa kutwa. Jioni JK HAFAI. Wake up my people, sisi tuwe mfano na si kulalamika tu. Hata akiingia Dr wa ukweli,, mtaanza kumlaumu muda mfupi tu baadaye kwa kutegemea miujiza.
  Narudi Mirembe wakuu.
   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  JK ni Mr Never Told, yaani bwana haambiliki, waswahili tunasema kama hujui kusoma ina maana hata picha huoni, sasa JK hata kama haambiwi na wasaidizi wake yeye hayaoni haya!
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna msemo wa Kiingereza unao sema "With great power comes great responsibility." Niambie ni nchi gani unayo ijua wewe ambayo mambo yakienda vibaya kiongozi mkuu halaumiwi? Mfano ni wa sasa wa Marekani ambapo Obama kakuta uchumi ni mbaya lakini lawama bado ana pata yeye kwa sababu he is the sitting president.

  Ila pia kwa Tanzania unabidi utambue nguvu za raisi. Raisi ana teuwa mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya mpaka baadhi ya wabunge. Ina maana viongozi wengi wakuu wa serikali wana teuliwa kwa utashi wa raisi. Sasa wayu hawa wakishindwa tumlaumu nani? Hata kama makosa yote si yake binafsi ana beba lawama kama mtu aliye mteuwa kashindwa kufanya kazi.

  Uraisi si lele mama mkuu. Uraisi si kupigiwa mizinga wala kupewa saluti. Uraisi si kupishwa barabarani. Uraisi ni jukumu kubwa. Tatizo wengi wetu tuki tafuta vyeo tuna tamanishwa na sifa za nafasi fulani bila kufikiria majukumu yake. Kikwete aliomba mwenyewe ridhaa ya kuongoza nchi. Alikua na uhuru wa kuto kugombea. Sasa kwa vile kataka mwenyewe abebe yote yanayo kuja na ofisi mazuri na mabaya.
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  usiwe kilaza wewe gari haliwezi kwenda bila dereva au dereva mlevi anaweza kuangusha gari uongozi wa kikwete wala siufagilii kabisa anafumbia macho magenge ya wezi na huu uvivu uliopo makazini hivi sasa unatokana na yeye mwenyewe kulea magenge ya wezi utamwambiaje ammtu aamke na kufanya kazi wakati wakubwa wake ni wezi maana kila akijitahidi kuvuja jasho kinachopatikana wanagawana wao haijaniingia akilini kabisa na samahani nimetumia maneno makali sababu nimeboheka sana na kauli zako kwamba watanzania ni wavivu si kweli
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Acha upuuzi wako.

  JMK ni lazima alaumiwe kila kona hata pale kosa likiwa ni la mtendaji katika ngazi ya Wilaya.
  Wewe unajifanya hujui madaraka aliyonayo Rais wa TZ.
  Rais wa Tanzania ndiye anaye teua watendaji wote wa serikali ya Tanzania vile apendavyo.
  Hawajibiki kisheria kumteua mtu kutokana na uwezo wake Elimu yake au uzoefu wake.
  Rais anaweza kumteua Mjinga yeyote kushika wadhifa wowote autakao kwa sababu amepewa uwezo huo.


  Serikali ya CCM imeshindwa kuongoza nchi kila sekta inalegalega ikiwa ni pamoja na CCM yenyewe.
  Watendaji wote wa serikali wameteuliwa na Rais kwa sababu ambazo yeye mwenyewe JMK anazijua.

  Sidhani kama ni haki kutoa pendekezo la kutaka tubadilike kuhusu kumtupia lawama JMK kwa kila jambo wakati yeye JMK anaona Raha kuteua Mashemeji, Nyumba ndogo na Washikaji wake kushika nyadhaifa muhimu ndani ya serikali bila hata kujali uwezo wao na elimu yao kwa ujumla.
  Rais JMK ndiye ameunda serikali mambo yakiharibika yeye pekee yake ndiye wa kulaumiwa.

  Kama si mzigo kuteua Lundo la watu katika nyadhifa zote ndani ya serikali ni vipi iwe si raisi kwake JMK kuwafikia moja kwa moja watu aliowateua??
  Yeye JMK hajasema kwamba anapata shida kufanya uteuzi,ameshindwa kufanya uteuzi kwa sababu ni kazi nzito,au ameomba asaidiwe kufanya uteuzi wa watendaji wa serikali ya CCM.
  Hilo wazo kwamba JMK hawezi kuwafikia watendaji wengi moja kwa moja linaenda kinyume kabisa na ukweli kwamba yeye JMK anawateua moja kwa moja.
  Kam kuna Tatizo TRA let say meneja mmoja wa TRA ana kula Rushwa ya wazi yeye anatakiwa kula sahani moja na mtu aliyemteua yaani Kamishna wa TRA.

  Si haki wala si nidhamu kumtetea JMK kwamba hastahili lawama zote juu ya Uzembe ndani ya serikali ya CCM.
  JMK ana uwezo wa kubadili watendaji wote wasiweza kazi ndani ya Serikali ya CCM wakati wowote ule bila pingamizi lolote.
  Kinacho mshinda JMK kuwaadabisha ni Ufinyu wake wa akili, uwezo ulo dumaa, Ukilaza(Amefikia ukomo wa uwezo wake wa kupambanua mambo anfaa kuwa katibu kata siyo rais) Kuchekacheka, Uhandisamu, Umalaya,Ubabaishaji na zaidi UFISADI.

  Sasa ulitaka tukulaumu wewe??
   
 14. S

  Short white Senior Member

  #14
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  JK anastahili kulaumiwa kila kosa linalofanyika kwenye serikali yake! Yeye ni mkuu wa kaya kwahiyo mambo ya ovyoovyo na ya kijingakijinga yanapotokea ndani ya kaya anastahili kubeba lawama. Endapo hatotaka lawama inambidi kufanya maamuzi mazito endapo mambo ya kijinga yanapotokea kwa hao aliowapa kazi ya kumsaidia.
   
 15. S

  Salimia JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mathalani watu wako wilayani ama jimbo maendeleo duni,, hilo nalo JK? Mbbunge je mlyemchagua wenyewe inakuwa vipi hapa? Huu ni mfano mdogo tu,, lakini ipo mingi yenye kuwianana na huu. Ndiyo maana si "kila kosa" JK tu ndiyo wa kulaumiwa. Napita tena wakuu
   
 16. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu urais siyo sehemu ya kujaribu. Sio suala la kusema hata nikikaa miaka kumi sitaweza kutoa shida zenu. Hivi kweli Kikwete angekuja mwaka 2005 na kutwambia hawezi tekeleza hiki na hiki kuna mtu angemchagua? Ukisikia tu hotuba za Kikwete utajua ni mtu aliyedhani urais ni sehemu ya kucheza ngoma. Awamu ya kwanza alitoa ahadi zenye matumaini makubwa bila kufikiri mara mbili, mwisho wa siku anakuja kushangaa hawezi kutekeleza hata chembe. Upuuzi tu. Tena hata hakujifunza kwa awamu ya kwanza, maana awamu ya pili kazidi kutoa ahadi lukuki zinazotekelezeka lakini yeye asizoweza zitekeleza.
   
 17. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo Kwenye RED umesema tatizo la kina nani wavivu? hakuna Mtanzania aliye-mvivu, Tatizo Kikwete wako ndio Mvivu katika uongozi wake kama sio Mvivu nchi isngekuwa hapa ilipo. Ufisadi, Mikataba Feki,Umeme, Maji, Ajira, huduma za Jamii na matatizo mengineo ambayo unaweza kuyaongezea au kuyataja yanayokabili taifa letu. Huo Wote ni Ujinga au Uvivu wa Kikwete na wenzake kuyatatua hayo nilioyataja. Unafikiri unapogombania uongozi unakuja kula kuku na mrija? siunakuja kutumikia Taifa na kulinda rasilimali zake ambazo wewe ndio mmoja wao wakulindwa kama alivyoapa. Sasa kama hawezi kazi kwanini asing'atuke au kujiuzulu? Kama hataki Lawama aende akalime Mananasi huko Chalinze kama kuna mtu atamlalamikia.
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Na mimi nazidi kumlaumu Kikwete kwa kuwasikiliza wapuuzi kama wewe wanaomtetea bila kuhoji madaraka makubwa aliyokabidhiwa. Watu kama Salimia hawakosi kumshangilia dereva aongeze mwendo hata kama anaonekana hana uwezo wala ujuzi wa kuliendesha gari. Tatizo ni kwamba Kikwete alililia madaraka yaliyo nje ya uwezo wake na akina Salimia kama vipofu vile wakampa. Hapana, the buck stops with the President, full stop.
   
 19. S

  Shauri JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi kabisa bosi?nakuunga mkono kwa asilimia 50%.kikwete nchi imeshamshinda.atuachie sisi cdm!   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kikwete ana matatizo yake
  kikwete pia ana gundu, anachukiwa sometimes bila sababu
  sisi wananchi pia tuna role kubwa kwenye shida zilizopo
  but the bottom line ni kwamba kikwete ni nahodha kwahiyo macho yetu yote yako kwake
   
Loading...