Je Kikwete arudishe fedha za nguo anazonunuliwa na nchi yake "maskini'? atumie mshahara wake?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Katika majibu yao Ikulu imesema kuwa Rais Kikwete haitaji kununuliwa nguo na mfadhili yeyote au kupelekwa shopping. Kwamba, "toka akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa anapokea posho ya mavazi. Na sasa kama Rais jukumu lote la mavazi yake ni la serikali"! Najiuliza hivi hadi Rais ananunuliwa nguo na wananchi wake maskini huku akipokea mshahara mnono. Kwanini asitakiwe arudishe fedha zote za kununulia nguo alizopewa na taifa lake maskini juu ya mshahara wake?

Ni wazo tu ambalo limenijia. Au kumtaka arudishe tutakuwa tunamnyima "haki" yake kwa sababu "sheria haimkatazi". Je kitu kikiwa kisheria maana yake ni kiko kimaadili? when a thing is legal does it me it is also moral and ethical? In other countries for example abortion is legal but is it moral?

Je tukijua kiasi kilichotumika kumnunulia nguo tangu akiwa FM hadi sasa kama Rais haziwezi kutosha kunaksisha madarasa kadhaa ya shule za kata?

kama anagharimiwa na kukirimiwa vitu hivi vyote na nchi yake.. gari, afya, mavazi, chakula hata kuhudumia wageni.. analipwa mshahara kwa ajili gani.. maana wengine wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi wanazofanya ili waendeshe maisha yao.. sasa yeye maisha yake yote yanaendeshwa na fedha za Watanzania hadi tai na viatu.. aidha mshahara wake upunguzwe au arudishe hizo fedha... nawaza tu
 
Je kitu kikiwa kisheria maana yake ni kiko kimaadili? when a thing is legal does it me it is also moral and ethical? In other countries for example abortion is legal but is it moral?

Mbona hii 'reasoning' hujaitumia kule kwa rafiki yako?
 
Mwanakijiji
Sipingani na mawazo yake na naheshimu uhuru wa kutoa mawazo. Lakini natofautiana kidogo sana nawe kwasababu sidhani kama kazi ya mshahara ni kununua nguo pekee. JK ana watoto ambao inabidi wasome, sidhani kama Ikulu inawasomesha ama inawalipia ada, anatakiwa kutoa pesa yake mfukoni kulipia ada ya watoto wake. Atapata wapi pesa kama sio mshahara wake na posho zake?
Pia JK ana ndugu ambao kwa namna moja ama nyingine wanamtegemea yeye, Mama, babu, bibi na hata wakwe kama tujuavyo extended family zetu waafrika. Fedha ya kuwasaidia haitoki kwenye kasma tu ya Ikulu, ni ile ya mshahara wake.
Hiyo ni mifano tu michache lakini naamini yapo mambo mengi ambayo anatakiwa kuyafanya kwa fedha ya mfukoni mwake na sio kufanyiwa na IKULU> Kama hoja yako ya kwamba kwakuwa anapata mshahara basi hapaswi kufanyiwa mambo mengine bali atumie mshahara wake, nauliza kitu kimoja kwamba vipi kuhusu wakurugenzi na makatibu waku na hata watendaji wengine ambao wanapewa fedha ya mafuta, simu, umeme majumbani na bado wanapewa mishahara mikubwa? Mbona hao hatuwaulizi na hatusemi wasipewe mshahara?
Narudia sipingani na hoja yako na naheshimu mawazo yako, na huu ni mtazamo wangu tu.
 
Katika majibu yao Ikulu imesema kuwa Rais Kikwete haitaji kununuliwa nguo na mfadhili yeyote au kupelekwa shopping. Kwamba, "toka akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa anapokea posho ya mavazi. Na sasa kama Rais jukumu lote la mavazi yake ni la serikali"! Najiuliza hivi hadi Rais ananunuliwa nguo na wananchi wake maskini huku akipokea mshahara mnono. Kwanini asitakiwe arudishe fedha zote za kununulia nguo alizopewa na taifa lake maskini juu ya mshahara wake?

Ni wazo tu ambalo limenijia. Au kumtaka arudishe tutakuwa tunamnyima "haki" yake kwa sababu "sheria haimkatazi". Je kitu kikiwa kisheria maana yake ni kiko kimaadili? when a thing is legal does it me it is also moral and ethical? In other countries for example abortion is legal but is it moral?

Je tukijua kiasi kilichotumika kumnunulia nguo tangu akiwa FM hadi sasa kama Rais haziwezi kutosha kunaksisha madarasa kadhaa ya shule za kata?

kama anagharimiwa na kukirimiwa vitu hivi vyote na nchi yake.. gari, afya, mavazi, chakula hata kuhudumia wageni.. analipwa mshahara kwa ajili gani.. maana wengine wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi wanazofanya ili waendeshe maisha yao.. sasa yeye maisha yake yote yanaendeshwa na fedha za Watanzania hadi tai na viatu.. aidha mshahara wake upunguzwe au arudishe hizo fedha... nawaza tu
Ni miongoni mwa posho legelege ambazo wabunge wa CDM wanazipigia kelele ili zifutwe alkini Serikali Legelege imekataa kuzifuta kwa sababu inaonekana zitaathiri AFYA ya wakubwa serikalini akiwemo huyo RAISI wako. Sasa hebu piga mahesabu mwenyewe ujionee fedha za wavujajasho zinavyoliwa bila huruma, achilia mbali zile bilioni 50 za U- VASCO DA GAMA. Kazi kwelikweli.
 
mimi kinachoniuma kabisa ni hii tabia ya viongozi wote wa serikali masikini kupewa kila kitu huko walala hoi ambao ndo walisitahiki kupewa wakiwekwa pembeni. hawa watu wanamishahara minono, per diem kubwa, lakini ni hao hao wanaolipiwa huduma zote na serikali bure eg
umeme
maji
usafiri
nyumba
mavazi(kitu ambacho hata sijapata kukifikiria, sijui na chupi pia?)
ulinzi
chakula
Sasa hawa wanapokea mshahara wanini? kwanini wasisubiri pension tu huko uzeeni?
Hii nchi hii muda wake umbioni.
 
Acheni majungu.. hii habari tayari imesha expire.. mnairudisha humu ili nini??
Tumekosa kabisa cha kuzungumzia?
 
Braza hebu futa hii kauli inalidhalilisha taifa. Kwa mtu mwenye mawazo mafupi anaweza kudhania rais alipakatwa, manake waarabu ndio zao kupakata wengine. Tafadhali iondoe post yako kwani ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu. Zawadi ni zawadi jamani..

Ndugu yangu, hata kama hii post inachukiza lakini huu ndio ukweli wenyewe. Pamoja na wananchi kumvesha rais wao na kumghalamia kwa hali na mali (refer post ya Mwkjj) bado mwarabu ametuzidi ujanja. SVipande vya suti tano tu vilitosha na akamtoa out kabisa..Londoni...lo! napita tu.
 
Acheni majungu.. hii habari tayari imesha expire.. mnairudisha humu ili nini??
Tumekosa kabisa cha kuzungumzia?
Mkuu hii kitu inakufaa, jipachike kunako: pink_dildo.jpg
 
Braza hebu futa hii kauli inalidhalilisha taifa. Kwa mtu mwenye mawazo mafupi anaweza kudhania rais alipakatwa, manake waarabu ndio zao kupakata wengine. Tafadhali iondoe post yako kwani ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu. Zawadi ni zawadi jamani..

mkuu hiyo post ni ya uchungu sio yeye ni matatizo aliyonayo na mkuu wa nchi..
 
Heshma mbeeeeele kama tai Mzee Mwanakijiji!!!!!!

Siku zote maji ndio hayo yashamwagika kuyazoa tena kazi bora mtu kuyapigia deki tu na pengi ukilazimisha kuyanya ndio hivo yaweza geuka kuwa sumu mwilini mwako.

Pengine watu tuendelee kujifariji hapa kwamba afadhali ya hiyo kashfa ya suti, je kukija kutolewa video clips za EVENTS chumbani kempinki kuna mtu bado ataendelea kuvuta sigara hapa????????
 
Nchi ya ajabu sana, hivi kama hata mawaziri wananunuliwa nguo kwa kodi ya wananchi si ina maana kuna matumizi mengi ya ajabu kwa nyadhifa mbalimbali ambayo hatuyajui bado?? Wananunuliwa hadi nguo, na bado wao ndo wezi wakubwa wa mali zetu (kupitia rushwa, uzembe, mikataba ya hovyo nk) Ndo maana hawajui mateso ya wananchi wao.
 
Katika majibu yao Ikulu imesema kuwa Rais Kikwete haitaji kununuliwa nguo na mfadhili yeyote au kupelekwa shopping. Kwamba, "toka akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa anapokea posho ya mavazi. Na sasa kama Rais jukumu lote la mavazi yake ni la serikali"! Najiuliza hivi hadi Rais ananunuliwa nguo na wananchi wake maskini huku akipokea mshahara mnono. Kwanini asitakiwe arudishe fedha zote za kununulia nguo alizopewa na taifa lake maskini juu ya mshahara wake?

Ni wazo tu ambalo limenijia. Au kumtaka arudishe tutakuwa tunamnyima "haki" yake kwa sababu "sheria haimkatazi". Je kitu kikiwa kisheria maana yake ni kiko kimaadili? when a thing is legal does it me it is also moral and ethical? In other countries for example abortion is legal but is it moral?

Je tukijua kiasi kilichotumika kumnunulia nguo tangu akiwa FM hadi sasa kama Rais haziwezi kutosha kunaksisha madarasa kadhaa ya shule za kata?

kama anagharimiwa na kukirimiwa vitu hivi vyote na nchi yake.. gari, afya, mavazi, chakula hata kuhudumia wageni.. analipwa mshahara kwa ajili gani.. maana wengine wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi wanazofanya ili waendeshe maisha yao.. sasa yeye maisha yake yote yanaendeshwa na fedha za Watanzania hadi tai na viatu.. aidha mshahara wake upunguzwe au arudishe hizo fedha... nawaza tu
Mzee Mwanakijiji, posho ya mavazi ni miongoni mwa stahili sio tuu za rais au waziri, mpaka mfanyakazi wa kawaida wa serikali, akipata safari ya nje ya nchi, hustahili kupatiwa posho ya kukidhi kununua suti 2, shati mbili na tai.

Hapo tunazungumzia posho ya nguo tuu ambayo ni stahili, ziko posho kibao kwa kila ngazi, mfano ukiteuliwa nafasi ya ukurugenzi, unapewa mpaka posho ya fanicha!. Ukiteuliwa kwenye zile nafasi 5 za top, unaingia na gari mpya na ukimaliza muda wako, unaondoka nalo linakuwa ni la kwako!. Hata wale wakuu wa vyombo vya dola, spika, jaji mkuu, IGP, CDF, mkuu wa TISS, unapobakiza miezi sita kustaafu, taasisi inakununulia gari jipya ambalo ukistaafu, unastaafu nalo. Makatibu wakuu wakistaafu, wanastaafu na magari yao!.

Hiyo posho ya mawazi ya rais ni peanut tuu ukilinganisha na posho kibao anazokomba, hivi unajua rais anaposafiri nje ya nchi, zaidi ya wale maofisa ambao anaandamana nao, maofisa usalama, advance party, walinzi na maofisa wa serikali kibao, pia anasafiri na mtu wa kumvisha , valet, anasafiri na mtu wa kumbebea laptop yake, anasafiri na mtu wa kuonja chakula chake, anasafiri na daktari wake, anasafiri na ADC wake, anasafiri na katibu wake wa private, achilia wale wasaidizi wake kibao. Siku hizi msafara pia hujuisha waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali achilia mbali ile PPU. Kuna wakati msafara unafikia mpaka watu 100! na wote hawa wanapata posho zote stahili ikiwemo hiyo posho ya mavazi, tena hulipwa per diem na kukuta kule ubalozini wamewalipia kila kitu, kila mlo ni special lunch, dinner or party na fedha zote za chakula na malazi zinaishia mifukoni kama posho!.

Ningeshauri serikali yetu, ifuate mfumo wa serikali ya Uingereza wanatumia utaratibu unaitwa "actuals", ukisafiri ukirudi, una retire risiti za kila ulichotumia, hapa nchini kuforge marisiti ni kawaida, kwa wenzetu ni no, in this way, serikali itaokoa mabilioni ya fedha zinazoishia mifukoni mwa watumishi wa umma kama posho!. No wonder wenzetu wanaweza kujenga mahekalu ya ghorofa kuelekea mbinguni bila kukopa, wakati wazungu wenyewe wenye fedha zao, morgage zinawaumiza mpaka kumiliki nyumba ni kazi, wengi wao ni wapangaji tuu maisha yao yote, sisi huku na umasikini wetu, watumishi wa umma ndio matajiri wa nyumba, akina siye tukiishia kuwa wapangaji wao!.

Ukweli ni kuwa sio warudishe posho za nguo, bali hizo posho za nguo sasa zitalipwa kwa kiwango cha Seville Suit ili rais wetu asipaswe kuaibishwa kwa kulazimika kulipiwa na mwarabu wa Kilimanjaro, na kwenye per diem, yake, room rate itafanywa M. 1.5 ili ilingane na ile rate ya executive room ya pale Kempiski ili rais wetu akijisikia kujipumzisha pale, ajilipie mwenyewe kuliko kulipiwa na kutangazwa hadharani, ati kalipiwa US $ 1,000 pale Kempinski kwa ajili ya zile shughuli za short time!.

Mimi nashauri rais wetu alipwe top salary ili asiabishwe na vijizawadi vya suti na kulipiwa chumba!.

Pasco.
 
Mwanakijiji
Sipingani na mawazo yake na naheshimu uhuru wa kutoa mawazo. Lakini natofautiana kidogo sana nawe kwasababu sidhani kama kazi ya mshahara ni kununua nguo pekee. JK ana watoto ambao inabidi wasome, sidhani kama Ikulu inawasomesha ama inawalipia ada, anatakiwa kutoa pesa yake mfukoni kulipia ada ya watoto wake. Atapata wapi pesa kama sio mshahara wake na posho zake?
Pia JK ana ndugu ambao kwa namna moja ama nyingine wanamtegemea yeye, Mama, babu, bibi na hata wakwe kama tujuavyo extended family zetu waafrika. Fedha ya kuwasaidia haitoki kwenye kasma tu ya Ikulu, ni ile ya mshahara wake.
Hiyo ni mifano tu michache lakini naamini yapo mambo mengi ambayo anatakiwa kuyafanya kwa fedha ya mfukoni mwake na sio kufanyiwa na IKULU> Kama hoja yako ya kwamba kwakuwa anapata mshahara basi hapaswi kufanyiwa mambo mengine bali atumie mshahara wake, nauliza kitu kimoja kwamba vipi kuhusu wakurugenzi na makatibu waku na hata watendaji wengine ambao wanapewa fedha ya mafuta, simu, umeme majumbani na bado wanapewa mishahara mikubwa? Mbona hao hatuwaulizi na hatusemi wasipewe mshahara?
Narudia sipingani na hoja yako na naheshimu mawazo yako, na huu ni mtazamo wangu tu.
Bibi Kuku, Naungana na wewe kwa asilimia 100%, tena sio tuu ni jukumu la serikali kumgharimia, bali posho ya mavazi sio favour, ni stahili kwa mujibu wa stand orders za utumishi wa umma, nadhani hata wabunge wanalamba posho hizi ndio maana wanavaa sana suti!,
 
Acheni majungu.. hii habari tayari imesha expire.. mnairudisha humu ili nini??<br />
Tumekosa kabisa cha kuzungumzia?
<br />
<br />
Uwe mpole tu mkuu. Kuna watu wamekufa miaka kibao iliyopita lkn bado utakuta tunajadili mambo/matukio mbalimbali kuwahusu na hakuna noma..... Hii habari haita expire tutaendelea kuijadili na miaka ijayo tutaitumia kuwaonya watoto wetu, japo itakuwa ngumu wao kuiamini. ".... nchi hii ilikuwa na waziri wa nje ambaye alikubali kulipiwa gharama za chumba cha hoteli na mwarabu, na si hivyo tu alikuwa anatolewa out ya kwenda London kununuliwa nguo na mwarabu!!!"
Hivi huyu ndo yule aliyewapasha wanafunzi wanaopata mimba kuwa wana viherehere??!!
 
Hawezi kukubali kurudisha pesa maana hizo wanaziita zawadi. Maspy wa ulaya wanaziita rushwa. Na sisi watu wa kawaida tunashangaa wenye hekima kwanini hawashitukii mitego midogo midogo ya hawa watu wanaowaamini sana.Wameamua kuwafix
 
Nchi ya ajabu sana, hivi kama hata mawaziri wananunuliwa nguo kwa kodi ya wananchi si ina maana kuna matumizi mengi ya ajabu kwa nyadhifa mbalimbali ambayo hatuyajui bado?? Wananunuliwa hadi nguo, na bado wao ndo wezi wakubwa wa mali zetu (kupitia rushwa, uzembe, mikataba ya hovyo nk) Ndo maana hawajui mateso ya wananchi wao.

Cha ajabu pia ni kwamba kama kuna bajeti inatengwa kwa ajili ya mavazi na vitu vingine kwa nini akubali ofa ya suti toka kwa mwarabu?
 
Back
Top Bottom