Je Kikao Kijacho Cha Bunge Kianze na Miswada Au Report Za Uchunguzi

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,314
3,987
Tukiwa Bado na kizunguzungu cha Richmond naomba wadau wote na wabunge wetu katika kikao Kijacho, waanze na Report za Ufisadi ulioikumba nchi yetu katika kipindi cha BWM, na hata za Zamani kama Debt Conversion etc.
Hivyo wakiwa wanajianda na hilo naomba nipendekeze baadhi ya issue za kujadiliwa.
Report ya Madini ya Bomani na Zilizo Tangulia
Report ya Richmond
TICTS
Utekelezaji wa ushauri wa CAG
Ubadhirifu uliofanyika katika Vyama vya Ushirika vilizo pelekea Serekali kuchukua madeni ya hivyo Vyama wakati walaji wapo na wana julikana lakini wabeba mzigo ni sisi sote
Kuna Mswada wa Kufuta Queries za CAg za Pesa Nyingi tu ili zisijirudie, yaani ili serekali iache kupata hati chafu, sasa baada ya kufuta hizo expenditure je ni hatua gani zimechukulia dhidi ya hao wabadhirifu. etc
Wenye kashafa au masuala ya kujadiliwa naomba tuwasilishe hapa Jamvini.
 
Tusubiri JK awashughulikie wale waliotajwa kwenye ripoti ambao hawapo bungeni kama Hosea,makatibu wakuu na makamishna baada ya ziara ya Bush then tutapata pa kuanzia
 
Sijaelewa nia hasa ya swali lako maana unajua kabisa whatever we will discuss here haitaweza kubadili mpangilio wa namna ya kufanya kazi za Bunge .
 
nia ni kuwataka wabunge wa weke shinikizo ili wajadili ubadhirifu ambao ume tokea na sasa unafunikwa kila siku bila hatua zinazo faa kuchukuliwa kwa nia ya kulindana. sasa huyo mbunge awe wa chadema/ccm au cuf au udp yote sawa.
 
Utaratibu na kanuni za Bunge katika kuendesha vikao vyake ziko vipi hadi hili liwekewe shinikizo ?
 
Shinikizo ilio tokea kwenye issue ya Richmond ilikuwa utaratibu au? Maana Spika alisha sema Mpaka Alhamisi Yeye Anakwenda America, je kilicho tokea baada ya hapo ni nini? Utaratibu?
 
Tusubiri JK awashughulikie wale waliotajwa kwenye ripoti ambao hawapo bungeni kama Hosea,makatibu wakuu na makamishna baada ya ziara ya Bush then tutapata pa kuanzia

Mwisho wa Mechi moja ni maandalizi ya Mechi ijayo. Hapo utamuweka mshindani wako kwenye tip top. Otherwise utafanya maandalizi ya kukurupuka , afterall unaweza kuondoa maada yako ikiwa imepitwa na events na ukumbuke nimeweka maada mbali mbali sio ya richmond tu, kuna issue za TICTS, Ubadhirifu mwingine serekalini, kwenye Vyama vya Ushirika, Kuna NGO ambazo zimeandikishwa lakini haziwasilishi vitabu vyao vilivyo kahulia kwa mrajisi, kuna issue za BWM na Group lake ambazo labda zime guswa sehemu tu kwenye kiwira Mines tu.
 
Tulale mbele na ripoti za uchunguzi kwanza hiyo miswada isubiri kikao cha bajeti kuna miezi 2 na ushee huko....
 
Tulale mbele na ripoti za uchunguzi kwanza hiyo miswada isubiri kikao cha bajeti kuna miezi 2 na ushee huko....

Mkuu Masatu,

Ni kweli kabisa, tusafisha nyumba yetu kwanza kabla hata ya kuleta miswada mipya. Hizo sheria zote hazitusaidii kitu kama hao mafisadi wanaendelea kutuibia.

Mwaka huu uwe wa kuchunguza na kuadhibu mpaka tutakavyopata uhakika wa angalau kwamba nyumba yetu inaanza kuwa safi na akina Mwanyika, Hosea, Rostam, Yona, Ballali na wengine wamechukuliwa hatua.
 
Kwenye Kikao kijacho Ningependa au Kuomba Wabunge Waombe Taarifa ya Hatua zilizochukuliwa na Serekali Dhidi ya Raisi Mstaafu, baada ya kubainika kwamba Alitumia Madaraka ya Uraisi kufanya UFISADI, na kama Serekali haijafanya Hivyo Basi Bunge, lipitishe Muswaada wa Kumvua Kinga Raisi Mstaafu Ili aweze kuchunguzwa, na Ikiwezekana Pension Yake Isimamishwe wakati Uchunguzi Unafanyika Juu Yake
 
Kwangu mimi,naona ni muhimu tuanze kwanza na mikasheshe ya kashfa then mijadala mipya. Ila tunaomba spika asijekudai anataka kuondoka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom