Je, kikao cha Rais na Wenyeviti wa Vyama vya siasa isipokuwa CHADEMA ni mpango wa kuzigawa kura za Urais za Tundu Lissu?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,460
17,284
Nimesoma mitazamo mbali mbali ya kikao hiki lakini bado sikupata mwanga wa moja kwa moja kuhusu dhumuni kuu la kikao hiki.

Lissu ndio mwanasiasa pekee ambae anauzika kwa sasa kuliko wakati wote ule! Kama mbobezi wa sheria,kama mwanasiasa mwenye utashi na uwezo mkubwa wa kujieleza,mwenye uthubutu wa kugusa hata wale wasioguswa kwa kusema ukweli wa wazi pasipo uoga!

Katika kipindi hiki kigumu cha nchi yetu inachopitia hasa kutofuata Sheria na kudhulumu haki ya kuishi na uoga wa wananchi kwa Chama dola CCM Lissu ndio suluhisho pekee la nchi yetu hakuna mwingine!mimi simuoni hata kwa tochi

Iwapo upinzani hasa CHADEMA wakisimama na Lissu kama mgombea hakika Rais Magufuli atapata wakati mgumu sana na yeye analijua hilo !Ndipo tunapotazama kikao cha juzi! Je, Lissu akiungwa mkono na vyama vyote pinzani, CCM watauweza mziki wake tena katika kipindi ambacho Tanzania inatazamwa kwa jicho la tatu na hao wanaowaita mabeberu kwenye la demokrasia.

Je, CCM wataambulia hata kura milioni moja?

Kikao kile kwa maoni yangu kinamhusu Tundu Lissu na ugombea wake wa kiti cha Urais!! Rais Magufuli anataka kuzigawa kura za Lissu ili asijegaragazwa vibaya Oktoba mwaka huu!!!

Rais Magufuli yupo tayari Maalim Seif ashinde Zanzibar kuliko Lissu ashinde Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Lissu anamnyima usingizi Rais Magufuli na ndio maana ya kile kikao juzi kuzigawa kura zake huku akilitafuta bao la mkono jingine hapo Oktoba mwaka huu!

Tuendeleze tafakuri ndugu zangu!!!
 
June.05.16.Magufuli.Fighting.Corruption-595x450.jpg
 
Lakini itabidi kwanza TL akili kwamba alitupotosha katika vita ya mageuzi ya madini. Aliwasihi sana wabunge wasipitishe marekebisho ya sheria za madini kwamba tutashitakiwa MIGA na akasisitiza kwamba ACCACIA itatufilisi sisi watanzania. Sasa kwasababu hayo yote yalienda mrama- proved failure, akianza kwa kuomba msamaha hapo kura tutampa. Tutajua ni mwenzetu sisi waTz wa hali ya chini.
 
Watu mbona mna haraka kiasi hicho? Vyama vya siasa viko zaidi ya 20, ndo kwanza Rais amefanya vikao na viongozi wa vyama vitatu,nyinyi mumeshaanza kulaumu,je mlitaka wote waitwe siku mmoja?
 
Mheshimiwa Mbowe alikwisha wasilisha yake kimaandishi na a
Nimesoma mitazamo mbali mbali ya kikao hiki lakini bado sikupata mwanga wa moja kwa moja kuhusu dhumuni kuu la kikao hiki.
Lisu ndio mwanasiasa pekee ambae anauzika kwa sasa kuliko wakati wote ule!Kama mbobezi wa sheria,kama mwanasiasa mwenye utashi na uwezo mkubwa wa kujieleza,mwenye uthubutu wa kugusa hata wale wasioguswa kwa kusema ukweli wa wazi pasipo uoga!!Katika kipindi hiki kigumu cha nchi yetu inachopitia hasa kutofuata sheria na kudhulumu haki ya kuishi na uoga wa wananchi kwa Chama dola CCM Lisu ndio suluhisho pekee la nchi yetu hakuna mwingine!mimi simuoni hata kwa tochi!
Iwapo upinzani hasa CHADEMA wakisimama na Lisu kama mgombea hakika JPM atapata wakati mgumu sana na yeye analijua hilo!Ndipo tunapotazama kikao cha juzi!!je Lisu akiungwa mkono na vyama vyote pinzani je ccm watauweza mziki wake?tena katika kipindi ambacho tanzania inatazamwa kwa jicho la tatu na hao wanaowaita mabeberu kwenye la demokrasia!je ccm wataambulia hata kura milioni moja?Kikao kile kwa maoni yangu kinamhusu Tundu lisu na ugombea wake wa kiti cha uraisi!!JPM anataka kuzigawa kura za lisu ili asijegaragazwa vibaya oktoba mwaka huu!!!Jpm yupo tayari Maalim seif ashinde zanzibar kuliko Lisu ashinde uraisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania!!!Lisu anamnyima usingizi jpm na ndio maana ya kile kikao juzi!kuzigawa kura zake!huku akilitafuta bao la mkono jingine hapo oktoba mwaka huu!!!
Tuendeleze tafakuri ndugu zangu!!!
Mheshimiwa Mbowe alikwisha wasilisha yake kimaandishi na akatuambia ni aliyoyaandika.
 
Kura za Lissu zitakuwa kwwnye 60% na wagombea waliobakia watagombania 40%. Watu washachoka kuishi kwa vitisho na kejeli kila wakiamka! Nchi imekuwa kama Scania iliiyofungwa tairi za basikeli? Inaahindwa kusonga mbele na kila tairi limeinamia opposite direction!
 
Uhakika wa kura za Lissu ni moja tu ambayo ni ya kwake. Lissu mwenyewe Hana uhakika kama mke wake atampigia yeye au CCM achilia mbali watu wake wa karibu, Kwa mantiki hii ushindi kwa Lissu ni mdogo sana.

Miaka ya nyuma hazina ya CHADEMA ilikuwa ni wale wenye umri kati ya miaka 18-25, kwa Sasa kundi hilo wamekuwa ni watu wazima ,wengine wameamua kubadilika, wengine wamejiunga CCM na wengine wanaona CHADEMA si sehemu salama kwa vijana kisiasa.

Mpaka hapo umeona ni kwa namna gani kura za CHADEMA zitakavyopungua kutoka kundi Hilo. Cha kukumbuka zaidi, Lowassa ndio mpinzani wa mwisho kupata zaidi 35% ya kura ,kwa miaka zaidi ya 100 Tanzania haitashuhudia tena wingi wa kura za upinzani wa zaidi ya 20%.
 
Historia haionyeshi yule mgombea wa chama cha kijamaa kama amewahi shinda ushindani wowote nje ya kubebwa si kwenye Siasa, biashara wala elimu
 
Uhakika wa kura za Lissu ni moja tu ambayo ni ya kwake. Lissu mwenyewe Hana uhakika kama mke wake atampigia yeye au CCM achilia mbali watu wake wa karibu, Kwa mantiki hii ushindi kwa Lissu ni mdogo sana.

Miaka ya nyuma hazina ya CHADEMA ilikuwa ni wale wenye umri kati ya miaka 18-25, kwa Sasa kundi hilo wamekuwa ni watu wazima ,wengine wameamua kubadilika, wengine wamejiunga CCM na wengine wanaona CHADEMA si sehemu salama kwa vijana kisiasa.

Mpaka hapo umeona ni kwa namna gani kura za CHADEMA zitakavyopungua kutoka kundi Hilo. Cha kukumbuka zaidi, Lowassa ndio mpinzani wa mwisho kupata zaidi 35% ya kura ,kwa miaka zaidi ya 100 Tanzania haitashuhudia tena wingi wa kura za upinzani wa zaidi ya 20%.
Tume huru ndio kipimo
 
Nimesoma mitazamo mbali mbali ya kikao hiki lakini bado sikupata mwanga wa moja kwa moja kuhusu dhumuni kuu la kikao hiki.

Lissu ndio mwanasiasa pekee ambae anauzika kwa sasa kuliko wakati wote ule! Kama mbobezi wa sheria,kama mwanasiasa mwenye utashi na uwezo mkubwa wa kujieleza,mwenye uthubutu wa kugusa hata wale wasioguswa kwa kusema ukweli wa wazi pasipo uoga!

Katika kipindi hiki kigumu cha nchi yetu inachopitia hasa kutofuata Sheria na kudhulumu haki ya kuishi na uoga wa wananchi kwa Chama dola CCM Lissu ndio suluhisho pekee la nchi yetu hakuna mwingine!mimi simuoni hata kwa tochi

Iwapo upinzani hasa CHADEMA wakisimama na Lissu kama mgombea hakika Rais Magufuli atapata wakati mgumu sana na yeye analijua hilo !Ndipo tunapotazama kikao cha juzi! Je, Lissu akiungwa mkono na vyama vyote pinzani, CCM watauweza mziki wake tena katika kipindi ambacho Tanzania inatazamwa kwa jicho la tatu na hao wanaowaita mabeberu kwenye la demokrasia

Je, CCM wataambulia hata kura milioni moja?

Kikao kile kwa maoni yangu kinamhusu Tundu Lissu na ugombea wake wa kiti cha Urais!! Rais Magufuli anataka kuzigawa kura za Lissu ili asijegaragazwa vibaya Oktoba mwaka huu!!!

Rais Magufuli yupo tayari Maalim Seif ashinde Zanzibar kuliko Lissu ashinde Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Lissu anamnyima usingizi Rais Magufuli na ndio maana ya kile kikao juzi kuzigawa kura zake huku akilitafuta bao la mkono jingine hapo Oktoba mwaka huu!

Tuendeleze tafakuri ndugu zangu!!!
Hao wanaoubeza upinzani hapa Tanzania hawaachi kumeza panadol kila siku. Propaganda za watu kwenda ikulu kugonganisha miguu wala zisiwakatishe tamaa wala kuwahadaa ukweli uko wazi kwa baadhi ya walioenda wazidi kuthibitishia umma kilichowapeleka wala sio kuwasaliti wananchi wapimeni hao watu kwa umakini sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom