Je, kazi ya Makamu wa Rais ni nini na kazi ya Waziri mkuu ni nini?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Mimi nilikuwa na matumaini makubwa kuwa Mh Rais Kikwete atapiga panga mmoja kati ya hawa, ama Makamo wa Rais au Waziri mkuu,hivi vyeo vinalingana na kuwaweka wote hawa nikuvuruga pesa za umma kiholela holela tu, huyu makamo wa rais ndio kabisa hana kazi kabisa ispokuwa sifa kubwa yake nikucheka cheka na kuvaa suti tu.

Nina matumaini makubwa 2015 watakapo ingia Chadema kushika Dola Baraza la Mawaziri litakuwa dogo na lenye kuchapa kazi mzuri, imani yangu ni hio kwa kipindi kifupi tu chadema tayari wamesha onyesha mwanga wa matumaini na mifano mingi hai.

Lakini miaka 50 hivi sasa chini ya utawala wa ccm tumechindwa watanzania kutatuwa matatizo ya umaskini tulio nao katika jamii zetu, rasilimali zote tulio pewa na Mungu huliwa na wachache tu , huku Watanzania walio wengi wakichindwa na mlo mmoja wasiku.

Watanzania sio ma-blind tunaona viongozi wetu wa ccm wanavyo tanuwa kwa magari ya kifahari na majumba ya kifahari huku watanzania wakihaha kwa chida na machaka ya kidunia.

Hakuna kiongozi mzalendo na mzuri mweye kula raha huku raia wake kuhaha na ziki za maicha , lakini Chadema imekubalika kutokana na kuwa karibu na Wananchi wao kwa chida na hali, mtu anapewa v8 la mamilion analikataa , wabunge wa chadema wamekataa kuongezwa kwa posha kutokana na kuangalia nyuma ummati wa Watanzania ulio wachaguwa kula ziki.

Inatilicha moyo sana kuwa bado kuna matumaini Chadema kuwa hawajatuwacha mkono , ccm bila ya ufisadi hawana long life, na dawa pekee kwa ccm nikubana sehemu zote za ufidsadi ,tukiweza hivyo itakuwa end of the road ccm.
 
swali zuri...i know waziri mkuu ni kiongozi wa shuhuli za serikali bungeni, bt swali ni kwamba bunge likiwa limehairishwa mawaziri wote wakawa wamerudi dar...je waziri mkuu kazi yake wakati bunge halipo ni nini?? huyu makamu wa Rais ndio kabisa sijui anafanya nini zaidi ya kumuona kwenye magazeti akiwa mikoani anatoa hotuba mbele ya wana ccm au akitembelea miradi flani flani labda kama mtu hapa anajua exactly kazi ya makamu wa Rais ni ipi

Je Rais akisafiri nani anakua in charge wa hii nchi..makamu wa rais or waziri mkuu

Swali la mwisho.... Rais wa hii nchi kazi yake ni nini?!! am sure katika katiba hakuna sehemu inasema wajibu wa rais ni kuhudhuria misiba ya viongozi wote wa tanzania na africa au watu mashuhuri tanzania au kusafiri nchi za nje mara kwa mara:glasses-nerdy:
 
makamu wa rais a.k.a dinyo a.k.a mr. Mkasi yeye kazi yake ni kuzunguka mikoani akiwa na mkasi wake kwa ajili ya kuzindua shule, hospitali, saccoss,

huyu waziri mkuu a.k.a bacary sagna kazi yake yeye ni kulia tu bungeni aijidai eti yeye ni mtoto wa masikini!
 
Wakuu naomba mnaojua mnijuze kama ikitokea Rais anakufa, je makamu atarithu kitu na automatic kua Rais na kumalizia term bila uchaguzi au kutakua na uchaguzi mdogo?

Mtanisamehe, lakini nimeona ni vyema nijifunze hili kwenu ili niweze kujua umuhimu hasa wa mgombea mwenza au makamu wa Rais
 
Sio Kweli !

Anakuwa Rais kwa muda wakati unaandaliwa uchaguzi mwingine wa Rais, unless ni karibu sana na uchaguzi.....

Kuna kipengele cha muda hapo sikumbuki exactly.......nadhani within 6 months uchaguzi inabidi ufanyike....

Makamu Rais anakuwa Rais moja kwa moja na kumalizia muhula.
 
Sidhani kama CCM watamruhusu kwani walishamkata kuwa hana maadili.
Siyo tu huyo VP alikatwa na kamati ya maadili ya CCM, bali pia kutokana na nukuu ya Katibu Mkuu wa CCM Kinana ni kuwa mwanaccm yeyote ambaye hakutinga kwenye top 5 yao iliyokwenda NEC ni kapi la kutupa!

Kwa maana hiyo itawezekanaje tena 'kapi' limrithi sitting President?!
 
kwa hiyo umefikiria ikitokea goli la mkono refa akalikubali tutaongzwa na mwanamke..aiseee
 
Wakuu naomba mnaojua mnijuze kama ikitokea Rais anakufa, je makamu atarithu kitu na automatic kua Rais na kumalizia term bila uchaguzi au kutakua na uchaguzi mdogo?

Mtanisamehe, lakini nimeona ni vyema nijifunze hili kwenu ili niweze kujua umuhimu hasa wa mgombea mwenza au makamu wa Rais
Mkuu Zamunda nadhani siyo vyema kufanya 'uchuro' na kufanya imagination ya kufariki kwa President kipindi hiki, badala yake waTz wote tujikite katika maombi kwa Mungu wetu ili amlinde na ampe afya njema JK ili aweze kumaliza salama kipindi chake cha Urais kwa kipindi kilichobaki anbacho hakizidi miezi 3, ili aweze kutimiza tendo la kihistoria hapa nchini kwa kuwa Rais wa kwanza kutoka chama tawala cha CCM kukabidhi madaraka yake kwa Rais aliyechaguliwa na wananchi toka chama cha upinzani, jambo ambalo litakuwa historia kwa kuwa halijawahi tokea toka nchi yetu ipate uhuru wake toka kwa mkoloni miaka 54 iliyopita.
 
Na yeye atakua na Makamu?

Ibara 37(5) endapo kiti cha rais kitakuwa wazi kutokana na rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za kuchaguliwa au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti ibara 40, kisha kushauriana na chama chake rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa makamu wa rais na uteuzi huo utadhibitishwa na bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote
 
Sio Kweli !

Anakuwa Rais kwa muda wakati unaandaliwa uchaguzi mwingine wa Rais, unless ni karibu sana na uchaguzi.....

Kuna kipengele cha muda hapo sikumbuki exactly.......nadhani within 6 months uchaguzi inabidi ufanyike....

Zilikuwa siku 60 baada ya kiti kuwa wazi ila bunge likafanya ammendment mwaka 2000 na kufanya makamu kumalizia muda uliobaki katika kipindi cha miaka 5 kisha kumteua makamu wa rais anayethibitishwa na bunge. Ibara 37(5)
 
Hizi ndizo kazi za Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu kama nilivyozinukuu kutoka kwenye Tovuti Rasmi ya Ikulu.

Utawala wa Jamhuri ya Muungano una Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri wa Mkuu na Baraza la Mawaziri.
Rais wa Jamhuri la Muungano ndiye Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serekali, Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
Rais ndiye kiongozi wa Utawala wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais ndiye msaidizi mkuu wa Rais kwa mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa ujumla na hasa ana wajibu wa kumsaidia Rais katika;
i. Kufuatilia utelekezaji wa kila siku wa mambo ya muungano
ii. Kufanya kazi zote atakazopewa na Rais
iii. Kufanya kazi zote na majukumu ya ofisi ya Rais, wakati Rais asipokuwepo au anapokuwa nje ya nchi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ndiye Kiongozi wa shughuli za Serekali Bungeni na ana mamlaka ya kudhibitisha, kusimamia na kutelekeza kazi za kila siku na mambo ya Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha anatekeleza jambo lolote ambalo Rais atamwelekeza kuwa lifanywe.
Rais wa Zanzibar ndiye Kiongozi wa Utawala wa Zanzibar, Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar
Baraza la Mawaziri ni pamoja na Waziri Mkuu, anayeteuliwa na Rais kutokana na Wabunge wa Bunge la Taifa. Serekali inatekeleza kazi zake kupitia kwa Wizara zinazoongozwa na Mawaziri. Kila wizara ina dhmana ya kazi na sekta yake.
 
Kumbe info nilizokuwa nazo ni outdated !. Ok, nimekupata.....

Zilikuwa siku 60 baada ya kiti kuwa wazi ila bunge likafanya ammendment mwaka 2000 na kufanya makamu kumalizia muda uliobaki katika kipindi cha miaka 5 kisha kumteua makamu wa rais anayethibitishwa na bunge. Ibara 37(5)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom