Je, kauli za mawaziri hawa kuhusu babu wa loliondo ni kauli za serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kauli za mawaziri hawa kuhusu babu wa loliondo ni kauli za serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Silas Haki, Mar 12, 2011.

 1. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Juzi, Serikali kupitia kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda ilimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kusitisha kwa muda utoaji wa huduma hiyo hadi itakapojiridhisha kwamba dawa inakidhi ubora na inatolewa katika mazingira safi. Hata hivyo, hatua hiyo ilipingwa vikali na wananchi, viongozi wa dini na hata Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymund Mushi ambaye alisema utekelezaji wake utakuwa mgumu kutokana na hali halisi na mazingira yaliyopo katika eneo hilo kwa sasa. Katika kuonyesha jinsi mawaziri wa serikali hii wanavyokurupuka tu na kutoa kauli zao, jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Serikali haina tena mpango wa kuzuia huduma hiyo kwa kuwa inahusisha imani za watu. Swali la kujiuliza hapa ni "JE, MATAMKO YA MAWAZIRI HAWA YACHUKULIWE KAMA KAULI ZA SERIKALI? NI YUPI KATI YA HAWA WAWILI NDIYE ANAPASWA KUZUNGUMZIA SUALA HILI? HIVI SERIKALI HAINA MGAWANYO WA MAJUKUMU KWA MAWAZIRI WAKE? Karibu wadau kwa maoni.
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,462
  Likes Received: 1,375
  Trophy Points: 280
  TAtizo la hii dawa ya babu watu wameipokea kidini tofauti na malengo ya mtoaji wa hii dawa, na waziri Haji na e atakuwa alijiingiza kwenye mtego huu wa udini
   
 3. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Naomba niziangalie kauli za hawa mawaziri kama zilivyotolewa:-

  1. Kauli ya waziri wa afya aliitoa bila kukusudia, haikuwa kwenye speech yake, kauli hiyo ilikuwa baada ya mwandishi wa habari kumuuliza serikali ina mpango gani na hali inayoendelea loliondo, yeye akijijua ndo serikali as he is akakuruouka na kusitisha huduma loliondo.....

  2. Kauli ya Lukuvi naona kama imekusudiwa kuwa ndio tamko la serikali, ndio maana akaita press conferenc kwa ajili ya kuzungumzia suala la loliondo, so, it the agenda.......

  Kama kawaida, tatizo hapo k=ni kuwa kila mtu ni msemaji wa serikali nowdays......... long live ccm government

  Nasubiri kesho sofia simba aipige marufuku, keshokutwa Makinda aseme haijapigwa marufuku and so on.......
   
 4. m

  matejoo Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Haji Ponda hakuwa amejiandaa. Inaonekana pia Lukuvi katumwa kuweka mambo sawa. Hata hivyo hakufikia kiwango stahiki cha serikali ya nchi ya kidemokrasia hivyo naamini kabisa mivutano itaendelea sana. Badala ya kusema serikali itafanya hiki na kile sijui itatoa ulinzi sijui nini angetamka concept ndogo tu "tutashirikiana na wadau" kutafuta suluhisho. Kwani kuna shida gani kwa serikali kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini katika swala la kidini? Shame!!!
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio udini bali ni umbumbu wa mawaziri wetu, mara kwa mara huwa wanatoa kauli za kushangaza na za kupingana.
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa yaliyokwisha semwa yaongezwe yafuafayo; Haji ni waziri kamili(cabinet minister) mwenye dhamana ya masuala ya afya, wakati Lukuvi ni waziri wa nchi tu, kwa mantiki hiyo ni mdogo kwa Haji. Katika hali hiyo amepata wapi ujasiri wa kumkosoa mkuu wake hadharani! Pili kanuni zinazosimamia utendaji serikalini, haziruhusu mawasiliano ya wizara kwa wizara kufanyika kwa kupitia katika vyombo vya habari. Inakuwaje safari hii mambo yakafanyika tofauti?
   
Loading...