Je, Kauli ya JK kuhusu Kombe inahusiano na ile ya Nape kuhusu kutenganishwa kwa urais na uenyekiti?

LATTICE BOND

JF-Expert Member
May 30, 2011
219
48
Iliwahi kusemwa humu jamvini kwamba matokeo yeyote [Kushiinda au kushindwa] katika uchaguzi wa Igunga ni ongezeko la migogoro ndani ya ccm. Hii inatokana na tabia ya wana ccm wa leo kutokubali kutofautiana kwa hoja badala yake wameingia kwenye mtego wa kutofautiana kwa Majina na koo!!
Ongezeko la migogoro limeanza kujionyesha kwenye kauli zao wenyewe Mfano:
JK kakanusha taarifa ya gazeti la mwananchi kwamba amewapunguzia adhabu wauaji wa Imran Kombe. Katumia utetezi mwepesi kupinga hoja za Mwananchi. [Anayesamahe ni cheo si mtu. Kwa hiyo ku-personalize inatoa picha kuwa hakujibu kama taasisi bali individual]. Tafsiri yangu ukanushaji wake ni onyo kwa kundi lililoshinda igunga kwamba wasilete chokochoko maana bado ana makali ya kuwaadhibu. Hoja yake hiyo ya onyo ilichagizwa na Kauli ya ndugu yetu Nnauye alipowataka wapinzani wa JK ndani ya ccm wanaotaka kofia ya urais na Uenyekiti vitenganishwe WAJITOKEZE HADHARANI. Kauli hizi mbili si kwamba zimetolewa coincidentally bali ni mpango kamili wa kufikisha ujumbe kwa wapinzani wa ndani.
My take:-
CCM wanaogopana ndiyo maana wanashindwa kukaa vikao halali na badala yake wanafanya mijadala kupitia mikutano na waandishi wa habari.
 
Hili hata mimi nimeliona na limenishangaza sana jinsi Ikulu inavyoendeshwa kama nyumba ya familia ya JK
 
Mnara wa Babeli ulianguka kwa kupishana lugha.
The end of the end of ccm.
Unstopable!
 
Back
Top Bottom