JE KAULI MBIU/SERA YA KILIMO KWANZA ILIFANIKIWA/IMEFANIKIWA???/KILIMO NDO UTI WA MGONGO

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Serikali yetu Makini iliyoko madarakani imekuja na kauli Mbiu ya HAPA KAZI TU na naona watu wanaiunga mkono kwa asilimia kubwa kwani uwajibikaji katika taasisi mbali za Serikali pia za watu binafsi umekuwa mkubwa na wenye ufanisi hongera Serikali la hilo..

Pia Sera nyingine ni Nchi yetu kuwa na VIWANDA mbalimbali kwa lengo la kuzalisha ajira kwa wingi na kuzuia uagizaji wa bidhaa nyingi kutoka mataifa Ya nje.

Serikali iliyopita ilikua na kauli mbiu Ya KILIMO KWANZA na kweli ilitia bidii sana kuhakikisha kilimo kinafanikiwa nchi mwetu Kwani kilimo Ndo UTI WA MGONGO ikiwa ni pamoja na kutoa PEMBEJEO KWA WAKULIMA kwa bei nafuu,Kusambaza MATREKTA,na pia kuzalisha wataalamu wengi wa kilimo.

Swali langu ni Kabla ya Kuja na sera ya Viwanda Je SERA YA KILIMO KWANZA ILIFANIKIWA/IMEFANIKIWA??

Na ilikuwa ni SERA YA MIAKA MINGAPI?
NIMEULIZA IVYO KWA SABABU ILI VIWANDA VIFANYE KAZI LAZIMA MALIGHAFI ZIWEPO IKIWAMO NI PAMOJA NA MAZAO YA KILIMO.

Karibuni TUJUZANE...
 
Hapa kazi tu ni msisitizo wa KILIMO KWANZA, ona ndani ya KILIMO kwanza bila kuchapa kazi itakuwa kaulize ile haina maana ,sasa wewe mwenyewe umejionea watu wanavyochapa kazi subiri baada ya miaka mitano mkuu ili tuone matokea
 
Kwanza watu waliosoma kilimo certificate na diploma mpk sasa hawana kaz wapo mtaan tuu ilihali waliambiwa wakimaliza moja kwa moja wanapata ajira ila mpk now hakuna kinachoendelea wengi wameajiliwa na kampun binafsi tuu
 
Back
Top Bottom