Uchaguzi 2020 Je, kauli hizi za 'Tamaa ya Madaraka na kutomtuma mtu kugombea' alizotoa Rais Magufuli ni dongo kwa Makonda na Gambo?

Ukimsikiliza msemaji wa Rais anakwambia wazaramo wanausemi ambao unabamba sana mjini usemao Mwana kulitafuta Mwana kulipata pia Mama Samia naye anakwambia wateule wa Rais wajifunze kuridhika Ukija kwa JPM mwenyewe anawaambia mie sijatuma mtu...
Seems una hoja lkn umeshindwa kuitoa kwa wasomaji. All in all Makonda katumwa! Makonda hana akili za kufanya lolote bila maelekezo! Kwa hili kuachia madarka hawezi kuthubutu bila Jiwe kumpa support!
 
Anaandaliwa kuwa waziri na hata msishangae akawa waziri mkuu.
Tuwe makini sana na kauli za wanasiasa. Wanajua kucheza sana na akili zetu.
 
Bashite .....
Mi naona kabisa koroboi utambi unazama. Magu hanaga mambo ya kiswahili Kwanza Hana Siri akisema hakutaki ,hakutaki kweli, akisema sijakutuma ujue hujatumwa Hana kupapasa papasa mambo.

Kwenye hili makondo hawezi kosa tundikwa dripi za kutosha.
Na kwa vile Magu ni kama mungu ndani ya ccm basi tegemea Kigamboni kutoswa Makonda kura ya maoni mpaka atashangaa.
Tamko la magu ni kama kawaambia "simtaki huyo"
 
Rais Magufuli baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Dodoma amenena kwamba viongozi mbalimbali hawaridhiki kabisa na madaraka hasa waliozaliwa mwaka 82 (1982).

Pia soma> Uchaguzi 2020 - Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole...

Kauli hii imenifanya niangalie mwaka aliozaliwa Paul Makonda na Mrisho Gambo na kukuta wote wamezaliwa mwaka 1982. Naamini hii haiwezi kuwa bahati mbaya ila Rais alimaanisha alichokisema.

Nanuia kusema kwamba Makonda na Gambo mpaka sasa wana hali mbaya na huenda ukawa mwisho wao kisiasa.

Baadhi ya nukuu za Rais Magufuli...

Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982.

Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais, waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambapo hadi leo alfajiri wapo 829

Nawapongeza waliotia nia lakini niwahakikishie hakuna aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu, kama wapo wanaosema mimi nimewatuma ni waongo na hii meseji iwafikie Wana-CCM wote nyinyi wapimeni wagombea kulingana na mnavyoona wanafaa

Sijatuma mtu [kugombea ubunge]. Siwezi nikatuma mtu kupitia mgongo wa pembeni. Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma, kwanini nihangaike kukutuma, si ningesubiri tu kwenye viti vyangu 10 nikakuteua kama ningeshinda.

Kwa siasa za magu ukimpenda/usipompenda style yake, basi usiweke sana moyoni utaumia.
Rejea mambo ya vyeti vya magumashi alisema nini na alifanya nini?
Rejea uteuzi na utenguzi wa mwigulu alisema nini na alifanya nini?
Rejea uteuzi na utenguzi wa mrisho gambo alisema nini na gambo amefanya nini? Gambo hajachukua fomu kwa bahati mbaya.
Rejea malalamiko ya ndani na nje ya nchi kuhusu makonda, lakini amechukua fomu tena akiwa bado yuko ofisini. Baada ya kuchukua fomu ndio uteuzi wake umetenguliwa.

Mkulu alisha sema kwamba inategemea atakavyo amka. Usijiwekee uhakika wala usijikatishe tamaa kwa kiongozi wa aina hii, lolote linaweza kutokea na maisha yakaendelea.
 
Amin anin nawambien.
Paul makonda ameandaliwa kugombea jimbo la kigamboni na bada ya kuwa mbunge atakuwa waziri wa mambo ya ndani au waziri mkuu.
Mi nawambia haya ili badae yakitokea mjue nilisema.
 
Usimwamini sana Magu.

Kinyume chake huenda ndio ukweli ii msije kusema aliwaandaa ili aje awape uwaziri.
Mkuu wewe ndie umeona kwa jicho la tai, acha wanaorukaruka kama maharage kwa sufuria waendelee kushangilia.
 
Rais Magufuli baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Dodoma amenena kwamba viongozi mbalimbali hawaridhiki kabisa na madaraka hasa waliozaliwa mwaka 82 (1982).

Pia soma> Uchaguzi 2020 - Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole...

Kauli hii imenifanya niangalie mwaka aliozaliwa Paul Makonda na Mrisho Gambo na kukuta wote wamezaliwa mwaka 1982. Naamini hii haiwezi kuwa bahati mbaya ila Rais alimaanisha alichokisema.

Nanuia kusema kwamba Makonda na Gambo mpaka sasa wana hali mbaya na huenda ukawa mwisho wao kisiasa.

Baadhi ya nukuu za Rais Magufuli...

Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982.

Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais, waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambapo hadi leo alfajiri wapo 829

Nawapongeza waliotia nia lakini niwahakikishie hakuna aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu, kama wapo wanaosema mimi nimewatuma ni waongo na hii meseji iwafikie Wana-CCM wote nyinyi wapimeni wagombea kulingana na mnavyoona wanafaa

Sijatuma mtu [kugombea ubunge]. Siwezi nikatuma mtu kupitia mgongo wa pembeni. Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma, kwanini nihangaike kukutuma, si ningesubiri tu kwenye viti vyangu 10 nikakuteua kama ningeshinda.

Kumbe jamaa limetaja hadi miaka ya 1980s

Ila magufuli nae kwa kusengenya wanzake hajambo.
 
Back
Top Bottom