Je, katika shughuli za Mtanzania wa kawaida anaweza kuwa anahujumu uchumi au kutakatisha pesa bila kujua?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Watu wengi hatuna idea juu ya maana halisi ya kutakatisha Pesa, mbaya zaidi wengine wanadhani uhujumu uchumi ni sawa na kutakatisha pesa,

Tudadavue hapa.

Je, katika shughuli za raia wa Tanzania wa kawaida anaweza kuwa anahujumu au kutakatisha pesa bila kujua?
 
Mfano mdogo.
1. Kuhujumu uchumi. Kujiunganishia maji ya Bomba kinyemela.
2.Kutakatisha fedha
Kuvuka na rundo la pesa kutoka nje ya nchi bila utaratibu
 
Toa maelezo namba 2
 
Toa maelezo namba 2
Kutakatisha fedha ni kua na fedha ambazo ulizipata kwa njia isiyo ya halali kisha ukaanzisha labda biashara fulani ya halali ili kuzuga kua ile biashara ndio inakuingizia kipato kumbe ile biashara unazuga tu ili utakapokua unatumia zile hela haramu ionekane ni kama unatumia hela unazopata kwenye hiyo biashara ya halali,

Kwa kifupi,kutakatisha fedha ni kuzifanya fedha ulizozipata kwa njia ya haramu zionekane kama ulizipata kwa njia ya halali ili kukwepa kuulizwa fedha zote hizo umezipata kwa njia ipi?

Wajuzi watatusaidia zaidi.
 
Safi sana.
Kwa ufupi: Biashara yoyote haramu
 
VICOBA na michezo ya buku tano tano ya kina mama hutumika kutakatisha fedha za madanga ndani ya ndoa
Ndio nawasanua wanandoa
 
Watu wengi hatuna idea juu ya maana halisi ya kutakatisha Pesa, mbaya zaidi wengine wanadhani uhujumu uchumi ni sawa na kutakatisha pesa,

Tudadavue hapa.

Je, katika shughuli za raia wa Tanzania wa kawaida anaweza kuwa anahujumu au kutakatisha pesa bila kujua?
Dogo inakuwaje. Una swagger flan hivi Nashindwa kukuelewa. Unaweza potea jamvini kama wiki mbili hivi. Halafu ghafla unaibuka na mfululizo wa vithread, mada na comments UCHWARA
 
Watu wengi hatuna idea juu ya maana halisi ya kutakatisha Pesa, mbaya zaidi wengine wanadhani uhujumu uchumi ni sawa na kutakatisha pesa,

Tudadavue hapa.

Je, katika shughuli za raia wa Tanzania wa kawaida anaweza kuwa anahujumu au kutakatisha pesa bila kujua?
Yes, kwa mfano wale wanaouza chenji kwenye vituo vya daladala ule ni uhujumu uchumi sababu anauza pesa unakuta anakuuzia Mia Mia ikiwa 900 unampa 1000 yeye anapata shng 100.

Pia kuna tabia ya kukopeshana mtaani kwa riba mnakuta Kuna mtu ukihitaji milioni yeye a akukopa kwa riba pia Sheria inakataza.
 
Watu wengi hatuna idea juu ya maana halisi ya kutakatisha Pesa, mbaya zaidi wengine wanadhani uhujumu uchumi ni sawa na kutakatisha pesa,

Tudadavue hapa.

Je, katika shughuli za raia wa Tanzania wa kawaida anaweza kuwa anahujumu au kutakatisha pesa bila kujua?
Hiki kitenzi kinazaliwa na kiswahili kitarafa.

Kutakatisha,ama kusafisha, kufanya kitu kiondokane na mawaa.

Kwa hiyo fedha yoyote inayopatikana kwa njia haramu na kuifanya kuwa ni mali binafsi halali mf: itokanayo na biashara za madawa ya kulevya, ujangili wa nyara za serikali, wizi wa fedha za serikali nk nk ni kutakatisha.

Hapo sielewi kwanini wizi na ujambazi haujumuishwi kwenye utakatishaji.
 
Back
Top Bottom