Je, Katibu Mkuu wa CHADEMA analipwa mshahara? Mbona Dkt. Slaa na Dkt. Mashinji wameondoka wakiwa wadaiwa sugu wa benki?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,513
141,246
Jana nilimsoma pahala humu JF mkuu Douglas Sallu akiwa ametoa tangazo la benki fulani likiwataja kwa majina na picha wadaiwa sugu wa benki hiyo.

Miongoni mwa wadaiwa hao yumo Dr. Mashinji.

Dr. Slaa alipoondoka Chadema naye alikuwa na deni na nyumba yake kule mbweni almanusura ipigwe mnada sema tu CCM waliingilia kati na kumlipia.

Ndiposa najiuliza iweje hawa makatibu wakuu wanashindwa kulipa madeni ya mikopo yao au hawalipwi mishahara kupitia benki husika?

Niishie hapo,

Maendeleo hayana vyama!
 
Kudaiwa na benki ni jambo la kawaida tu na mara nyingi iwapo mkopaji anapitia kipindi kigumu cha mrejesho hukaa na benki yake na kuandaliwa namna ya kufanya.
Nimekuelewa bwashee hata ikitokea kwa JJ Mnyika najua ni kawaida!
 
johnthepaptist muogope Mungu, post au thread gani nimeweka hilo tangazo? Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo unazidi kushusha credibility yako hapa jukwaani.

Ninapokuita wewe ni mashine ya umbea siyo kama nakuvunjia heshima bali ni sifa uliyojizolea hapa jukwaani.

Na kwa taarifa yako katika thread na posts zote zilizobeba hilo tangazo siku comment kitu. Na kuhusu KM kulipwa mshahara, ni kuwa KM ndiye mtendaji wa Chama ina maana ni full-time job hivyo huyo Dr. Mashinji alikuwa anapata mshahara tena mzuri tu, suala la kudaiwa na benki ni la kwake binafsi.
 
Unataka jibu gani ili upate amani ya roho yako ? Kwamba ela zote chadema anakula mbowe? Mbunge kama msukuma nae alikua mdaiwa nbc maana yake serikali haimlipi? Kwa kawaida mikopo huwa ni pesa nying kuliko kipato unachopokea ila inabidi uwe makini kuchukua mkopo ambao unalipika, kwakweli hoja hapa ni ccm inatoa dau gani kuwavua hawa watu kiulaini hivi!?
 
Hapa nazungumzia Makatibu wakuu wa Chadema kuwa " Wadaiwa Sugu"
Sijaielewa concern yako ni nini haswa, mikopo ya benki ni sauala la benki na mteja wake wala siyo la chama. Mzee huu umbea unakusaidia nini, mbona zamani ulikuwa unaleta mada fikirishi, unafeli wapi siku hizi? Au ndiyo akili zimeanza kufubaa kutokana na umri mkubwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nazungumzia Makatibu wakuu wa Chadema kuwa " Wadaiwa Sugu"
Mtu yoyote anaweza kuwa mdaiwa sugu, pasipo kujali chama chake au nafasi yake. Hao uliowataja kuwa makatibu wakuu hizo ni nyadhfa tu ambazo haziwazuii wao kukopa kwa malengo ya kufanya maendeleo yao binafsi.
 
Wanaccm wanaraha sana wanakopa benki kwa biashara zao kisha CCM inawalipia madeni! Kweli ukimchukia mtu hata mti wake utaukata.
 
Mtu yoyote anaweza kuwa mdaiwa sugu, pasipo kujali chama chake au nafasi yake. Hao uliowataja kuwa makatibu wakuu hizo ni nyadhfa tu ambazo haziwazuii wao kukopa kwa malengo ya kufanya maendeleo yao binafsi.
Nilidhani ni mikopo ya Wafanyakazi bwashee?
 
Kwa hiyo unamaanisha mtu anaelipwa mshahara hawezi kukopa? Kwa kifupi umeongea kinyume,kwa taarifa tu ni kwamba mtu anaelipwa mshahara ndiye anaekopeka kirahisi kuliko mtu ambae halipwi mshahara!
 
Back
Top Bottom