Je, Katiba yetu inamruhusu Rais Samia kukaa miaka 15 Ikulu?

Thinker96

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
311
66
Hivi imekaaje kwa utaratibu wa Katiba yetu?

Maana:
Pierre Nkurunziza alikaimu miaka mitano ya mwenzie akaja kukaa kumi yake ikawa 15.

Edgar Lungu alikaimu miaka mitatu akakaa yake mitano na akagombea mitano mingine akashindwa.

Je, kwetu Tanzania SSH kwa kuwa amekaimu mitano ya JPM, sasa anaweza kugombania mitano ya kwake ya kwanza 2025 na pia mitano yakwake ya pili 2030?

Imekaaje wajuzi wa haya mambo kwa utaratibu wa kikatiba ulivyo.
 
Hata kukaa siku 15 haimruhusu. Anataka akae miaka minne halafu aseme,"Ah,nilikuwa naonja tu.! Sasa nataka nianze kula."
Madudu,kama ya Putin. Putin alikuwa Waziri Mkuu,halafu akasema ule muda aliokua rais hauesabiki,anataka kuwa rais tena.
Matusi. Anawatukana Warusi na anaitukana dunia. Nasikia Biden anafanya mipango ya kumpiga na ICMB.
 
62( umri wake kwa sasa) + 15 = 77 ikifanya nini Ikulu?
 
Je, kwetu Tanzania SSH kwa kuwa amekaimu mitano ya JPM, sasa anaweza kugombania mitano ya kwake ya kwanza 2025 na pia mitano yakwake ya pili 2030?

Imekaaje wajuzi wa haya mambo kwa utaratibu wa kikatiba ulivyo.
Mkuu Thinker96, kwanza nikupe pole maana kiukweli kabisa, elimu ya katiba bado inahitajika sana kwa Watanzania walio wengi, maana Kiukweli wengi humu ni viazi mpaka basi!.

1. Rais Samia hakaimu urais wa JPM, urais wa JPM ilikoma ile March 17!. Sasa Samia ndiye rais wa JMT na sio kaimu.
4. Hii miaka 4 ya JPM, Samia
anayoimalizia, sio kumshikia JPM, bali ndio term yake ya kwanza. Term yake ya pili ya Samia ni 2025-2030!.

Kiukweli kadri siku zinavyokwenda, ndivyo viazi humu vinazidi kuongezeka!.
Pole!.

P
 
Ya nini wakati CCM mnafaidi ujinga wa Watanzania?
Kila mtu na bahati yake. CCM ndio ilioandikiwa kutawala Tanzania milele. Watanzania wanaipenda, wanaikubali, wanaichagua.

Hili la CCM kutawala Tanzania milele ni ukweli kabisa, wanaobisha bisheni tuu maana kujifurahisha rukhsa!.
P
 
Hivi imekaaje kwa utaratibu wa Katiba yetu?

Maana:
Pierre Nkurunziza alikaimu miaka mitano ya mwenzie akaja kukaa kumi yake ikawa 15.

Edgar Lungu alikaimu miaka mitatu akakaa yake mitano na akagombea mitano mingine akashindwa.

Je, kwetu Tanzania SSH kwa kuwa amekaimu mitano ya JPM, sasa anaweza kugombania mitano ya kwake ya kwanza 2025 na pia mitano yakwake ya pili 2030?

Imekaaje wajuzi wa haya mambo kwa utaratibu wa kikatiba ulivyo.
Samia hajakaimu miaka ya mtu yeyote, ni Rais kamili wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba na anaweza kugombea tena urais kadri katiba inavyosema.
 
Mkuu Thinker96, kwanza nikupe pole maana
kiukweli kabisa, elimu ya katiba inahitajika sana kwa Watanzania wengi ni viazi mpaka basi!.

1. Rais Samia hakaimu urais wa JPM, urais wa JPM ilikoma ile March 17!. Sasa Samia ndiye rais wa JMT na sio kaimu.
4. Hii miaka 4 ya JPM, Samia
anayoimalizia, sio kumshikia JPM, bali ndio term yake ya kwanza. Term yake ya pili ya Samia ni 2025-2030!.

Kiukweli kadri siku zinavyokwenda, viazi humu vinazidi kuongezeka!.
Pole!.

P
Mkuu viazi mviringo au viazi vitamu??
 
Hata kukaa siku 15 haimruhusu. Anataka akae miaka minne halafu aseme,"Ah,nilikuwa naonja tu.! Sasa nataka nianze kula."
Madudu,kama ya Putin. Putin alikuwa Waziri Mkuu,halafu akasema ule muda aliokua rais hauesabiki,anataka kuwa rais tena.
Matusi. Anawatukana Warusi na anaitukana dunia. Nasikia Biden anafanya mipango ya kumpiga na ICMB.
Putin anawatukana Warusi na wakati yeye ni Rais wa Urusi? Ipoje hapo?
 
Mkuu Thinker96, kwanza nikupe pole maana
kiukweli kabisa, elimu ya katiba inahitajika sana kwa Watanzania wengi ni viazi mpaka basi!.

1. Rais Samia hakaimu urais wa JPM, urais wa JPM ilikoma ile March 17!. Sasa Samia ndiye rais wa JMT na sio kaimu.
4. Hii miaka 4 ya JPM, Samia
anayoimalizia, sio kumshikia JPM, bali ndio term yake ya kwanza. Term yake ya pili ya Samia ni 2025-2030!.

Kiukweli kadri siku zinavyokwenda, viazi humu vinazidi kuongezeka!.
Pole!.

P
Mkuu umeeleza vizuri sana lakini kwa kuweka vizuri zaidi hicho kipengele cha 4 kifute maana hakuna hiyo uliyoita "miaka 4 ya JPM" na wala amalizii miaka ya mtu yeyote bali pale alipoanzia inahesabika ndio kipindi chake cha kwanza kilipoanza.
 
Back
Top Bottom