Je, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina mamlaka juu ya Spika?

Hata sijui kama unajua maana ya neno hiari? wamejiita hivyo kwa sababu wameshafukuzwa uanachama, na kiuhalisia hakuna mbunge kule bungeni au kikatiba anayetambulika kama mwanachama wa hiari, so usipoteze muda wako tena kuokoteza kitu kingine ambacho hakina maana, bora upumzike tu.
Utakuja kuelewa mbeleni; that was just a hint.
 
Sasa jiulize nani mwehu kati ya mimi na wewe kupitia hiyo post yako.

Mimi ninaesema ni swala la wanasheria zaidi maana kuna vagueness kwenye katiba au wewe kiazi unaelazimisha lazima iwe hivi; hapo hapo unakuri una legal knowledge limitations.

Kazi kweli kweli
Ibara ya 71(1)(e) haina utata wowowte we kilaza. Ipo plaina and clear. Kilaza kama wewe ndio unahangaika,mpuuzi wewe unatakiwa uvae pampasi
 
Kwenye nchi yoyote ya kidemokrasia kunapokuwa na Katiba iliyoandikwa hiyo katiba inakuwa na mamlaka makuu juu ya Taifa zima. Sio Spika, Rais hata Jaji mkuu anaweza kuwa na mamlaka dhidi ya Katiba.

Mamlaka ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanapatikana kwenye ibara ya 64(5) ambayo yameweka bayana kuwa hakuna mtu au sheria yoyote itayotungwa itakuwa kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kama ninakosea niko tayari kukosolewa, ibara ya 71 (1) (e) imeweka bayana kuwa mbunge atapoteza ubunge wake kama uanachama wake utakoma kwenye chama kilichompa ridhaa ya kugombea ubunge. Hii ni wazi wabunge 19 wa CHADEMA waliofukuzwa sio wabunge halali hata kama waliapishwa kwa kanuni za bunge. Na spika anawatetea kwa sheria gani, au kanuni gani ambazo zinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Pia inasikitisha sana Spika wa bunge kudharau maoni ya wastaafu. Kwani ibara ya 71(1)(e) imefutwa? Kwani hii ibara haipo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka spika Ndugai awe anadharau maoni ya wastaafu na kudai hawajui kinachoendelea? Nini hicho kinachoendelea? Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebadilishwa? Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina mamlaka juu ya spika?

Jambo la msingi ambalo Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa akubumke ni kuwa bunge ni wananchi, ndio maana tunatuma wawakilishi wetu huko,la sivyo kila mtanzania angekuwa mbabe na kujiamulia anavyotaka. Na hakuna mtu kwenye nchi hii aliye juu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nilikuwa offline nimechelewa kuona andiko lako. Katiba katika nchi ya ki Africa especially Tanganyika ?!. Kwani mhula uliopita walipokuwa wanatunga sheria ya kutoshtakiwa ulikuwa ughaibuni ?!. Ndiyo madhara ya kuwa na wabunge wa chama kimoja kwa uwingi bungeni
 
Ahaaaa jaduong mbona unataka kuzalisha mada zingine? Kwani ile sheria inazuia wasishitakiwe? Au unawashitaki kupitia kwa Ag?
 
U
Ahaaaa jaduong mbona unataka kuzalisha mada zingine? Kwani ile sheria inazuia wasishitakiwe? Au unawashitaki kupitia kwa Ag?
Jaribu tu hata ktk sakata hili huwezi kumfanya chochote . Not only Spika , na wale wengine unaowafahamu.

Mmeiharibu sana nchi yetu . Ona sasa mmepora kura majimboni, mnakuja kugundua kuwa mambo hayaendi bila upinzani bungeni !!. Na sasa mnalazimisha mliowakataa majimboni waingie kwa gharama zozote.
 
Chagu kumbe upo vizuri namna hii? Sasa kipindi chote kwanini ulikuwa unaitesa nafsi yako aisee
 
Nimekuambia zaidi ya mara moja kuwa hayo mambo nimeona kwa macho yangu. Achia mbali wakala watatu wa upinzani waliozuiwa kuingia vituoni.
Sometimes mnaokota mawakala hawakidhi vigezo, ndio maana mnapoteza.
 
UJaribu tu hata ktk sakata hili huwezi kumfanya chochote . Not only Spika , na wale wengine unaowafahamu.

Mmeiharibu sana nchi yetu . Ona sasa mmepora kura majimboni, mnakuja kugundua kuwa mambo hayaendi bila upinzani bungeni !!. Na sasa mnalazimisha mliowakataa majimboni waingie kwa gharama zozote.
Jaduong kwenye hili hata Spika anajua amepotoka, huwezi kukanyaga katiba wazi namna hii. Ndio maana akina Halima wameona aibu.

Hayo mengine Jaduong ni malalamiko tu ambayo hayana ushahidi.
 
Kama ipi? Zaidi ya hii aibu ya spika kuforce king?
Ulitoa maoni gani kipindi cha sakata la mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kutoruhusiwa kukagua baadhi ya maeneo?
Au ile Tsh trillions 1.5 ambayo haijulikani ilikoenda ulitoa maoni gani?
Kipindi cha uchaguzi tuliona pia baadhi ya wagombea waliotoa changamoto kubwa wakishushiwa rungu la kustopishwa kupiga kampeni kwa makosa ambayo chama tawala kiliyatenda na kuvuka mipaka? Mambo ni mengi muda hautoshi
 
Nitoe maoni gani kwa ishu ya CAG ambayo bunge ilipatiwa majibu na PAC? Hilo la wagombea ni juu ya Chada kusema kweli, ilikuwa na wagombea wabovu ndio maana walienguliwa.
 
Back
Top Bottom