Je, Katiba mpya itakuwa na madhara gani kwa serikali ya JK ( Ndani ya Miaka 5)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Katiba mpya itakuwa na madhara gani kwa serikali ya JK ( Ndani ya Miaka 5)?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rich Dad, Dec 20, 2010.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wandugu,

  Mwenye ufahamu naomba atujuze wadau wa JF, Je mabadiliko ya katiba yakifanyika mapema ndani ya miaka hii mitano ambayo bado JK atakuwa mtawala unadhani kutakuwa na madhara gani ( I mean Consequences zake)?


  Kwa upeo wangu mdogo nadhani itasababisha kupungua kwa madaraka ya Rais ( dilution of Power) ambayo itapelekea mambo yafuatayo:-
  1. Rais ataanza kutawala kwa taabu kutokana na nguvu ya sheria itakayoibuka na hivyo kumwajibisha yeye pamoja na watuhumiwa wengine wa scandal kubwakubwa tunazozijua na tusizozijua mfano: EPA, RADAR, Kiwira Coal mines, RIchmond n.k
  2. Pili, nahisi katiba mpya itaamuru mihimili mitatu ya seriakali ( BUnge, Mahakama na Baraza la Mawaziri) ifanye mabadiliko makubwa ya kimuundo wa uongozi kwenye nafasi za kuteuliwa pamoja na zile za kuchaguliwa kwa kura za wananchi walio wengi.
  Je wewe huoni kwa sababu hizo nilizotaja hapo juu ndo inasababisha ucheleweshaji wa hiki kilio cha watanzania kilichodumu kwa muda mrefu?
   
 2. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nadhani Mdau swali lako limejengwa on wrong premises! Ningefikiri kuwa suala la Katiba halijadiliwi kwa vile JK yupo madarakani! Hivyo kujadili katiba kwa kumwangalia JK kutatuondoa kwenye objectivity na kutufanya kumjadili yeye. Tazama tayari unaanza kuuliza implication ya katiba mpya kwa EPA! Hii ndo inaweza kuleta woga miongoni mwa wanasiasa na wazandiki kuchelewesha kutungwa kwa katiba mpya kama njia ya kukwepa kuwajibika. Matokeo yake wanaweza KUWAWEKA watu ving'ang'anizi madarakani hata pale ambapo hawasitahili au wamepigiwa kura ya kwaheri kama walivyomfanyia Bagbo wa Ivory Coast.

  Ni vema kujadili suala la katiba kwa muktadha wa wananchi na taifa kwa ujumla, badala ya kumwangalia JK kana kwamba ndiye mtoa maamuzi ya mwisho ya kitu kipi kiingizwe na kipi kisiwemo (kulingana na yale yanayoweza kuwa yametokea)

  Binafsi nadhani hakuna sababu ya watawala kuona woga kuunda katiba inaweza kuwapa maamuzi watanzania (badala ya sasa inayowapa madaraka makuba watawala). Endapo kuna makosa lakini yalisababishwa na kuwepo kwa katiba mbovu, sioni sababu ya kuwawajibisha watu, badala yake ni SOMO tumejifunza watanzania. Hebu fikiria endapo Mandela angeamua kuwarudi MAKABURU baada ya kuingia madarakani (he had all the reasons to do that), nini kingetokea? Bila shaka, hadi leo Mandela anasimama kama kiongozi anayeheshimika sana duniani kwa namna alivyochukulia mambo ya hapo nyuma

  Hivyo, mimi naona si vema kutumia katiba KUWARUDI watawala wa sasa na hata wale waliopita
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usisahau bado JK ananguvu ya kimaamuzi aliyopewa na hiyohiyo katiba inayolalamikiwa.......kama ilivyokuwa kwa marais wengine waliopita JK anaweza akaamua kuziba masikio mpaka amalize term yake!
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  KWELI EEEH ndo maana Pinda anasema atamshauli Raisi nilikuwa sielewi! kama wananchi wameamua kwanini serikali imshauli raisi!?
  Sasa nimeelewa hili likatiba libomu linafanya maamuzi yoote yatoke kwa raisi, hata kama ni litaahila flani! jk plz tunaomba basi ibadilishwe, akiiingia kwenye uraisi kichaa nchi imekwisha kweli jk huoni hiloo!
   
 5. n

  nyantella JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  katiba isiwe kwa kwa ajili ya kujibu mambo ya muda mfupi kama anavyofikiria rich dad! it has to stay na kujibu masuala mengi ya wananchi wote both kiuchumi na kijamii so rushing will take us no where! hala issues za tume huru ya uchaguzi sioni kama ni possible maana sasa hivi tuanaona kuna taasisi nyeti ambazo zinalikisha information ambazo CDM ndizo wanapatia umaarufu na katika hiyo tume huru habari zita leak kama kawa maanake wapo kati ya wajumbe (labda wawe malaika!) watakua pro CCM wengine pro CDM, CUF, TLP, UDP etc. na kila mtu atafanya kivyake!!! and in short uzalendo tu ndio ungehitajika katika hili!

  so thekatiba we need isiangalie pressure groups kama CDM ambao sasa hawana issue baada ya serikali kusema katiba itaundwa wanakosa cha kupigia kelele!
  i am out!
   
Loading...