Barnaba Bushiri
Member
- Aug 1, 2020
- 46
- 26
Tumeona mtafaruku na mtifuano kwenye Social Media mara tu baada ya wale wanaodaiwa wabunge wa viti maalumu kutoka chama cha CHADEMA kuapa mbele ya spika leo.
Mara tu baada ya tukio hilo katibu mkuu wa chama hicho ameandika kwenye kurasa yake ya twitter kwamba hawajatuma majina ya viti maalumu kwenye ofisi ya bunge.
Lakini zinasambaa taarifa Mdee akimshukuru mwenyekiti na katibu wa chama chake kwa kuwapa wabunge hao ushirikiano wa kutosha.
Lakini swali la kujiuliza ni kwamba wabunge hawa walikwenda kuapishwa bila baraka za chama? Au chama hakikuwa na taarifa za wabunge hawa kuelekea Dodoma?
Je, ni nani mkweli kati ya Mdee na Mnyika?