Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,140
- 5,231
Nimekaa nikiyatafakari baadhi ya maandiko ambayo niliyasoma mahali na kubaini mapungufu fulani yenye ka chembechembe ka upotoshaji.
Kisha nikajiuliza swali je, nani atawajibika endapo mawazo yangu yakiwa sahihi (pengine ni ujinga nilionao juu ya tafsiri ya maandiko husika ndo yananifanya nione kuna dosari) juu ya nilichokikisia kuwa hakiko sawa?
Je, ni yule aliyegushi na kuwakosesha wenzake kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe?
Au ni yule aliyefuata mafundisho hayo kwa upofu akiamini ni matakatifu pasipo kuyachunguza undani au uhalali wake?
Au wote watapatwa na adhabu moja ya kutojua sheria siyo kinga dhidi ya kuvunja sheria?
Mfano wa maandiko hayo ni kama haya; naomba kunukuu kifungu kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha biblia:-
Sala ya Bwana Luka 11
2 Akawaambia, Msalipo, Semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], jina lako litakaswe, ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni]
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [ lakini tuokoe na yule mwovu]
Utaona kuna maandishi yapo kwenye mabano kwangu binafsi hapo ndipo palipo na utata wenyewe:
1. [Yetu uliye mbinguni] naamini hii ni dhana ya kupotosha yenye lengo la kumwondosha muamini katika mstari wa kujua kuwa Mungu wake yu mahali popote na hata ndani yake pia.
2. [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni] hii ni kauli mbiu yenye mfanano wa karibu sana na mafundisho ya illuminati (As done below here so above)
3.[lakini tuokoe na yule mwovu] sina cha kueleza hapa ila ni sawa na kumwombea adui (shetani) msamehewe pamoja.(labda kama dhamiri nitofauti na kauli)
Take home value: Hii sala bila ya hivyo vipengele hapo kwenye mabano ina make sense zaidi, hivyo kwa fikra zangu naamini kabla ya kuongezewa vipengele nilivyovibainisha kwa mabano hapo juu ilipaswa kuwa hivyo.