Je, Karma ni nadharia halisi na inayoweza kuthibitika katika maisha ya mwanadamu au ni imani ya faraja tu kwa wasio na uwezo waliokata tamaa?

Unajuaje jambo hili limetokea kwa sababu ya karma? Chukulia mfano wa Iddi Amin anayesadikika ni mmoja wa watu katili aliyepata tokea barani Africa,inasemekana alifanya kila aina ya ukatili na udhalimu,alipinduliwa madarakani na baadaye akaishi miaka mingi huko Saudi Arabia,akafariki kwa matatizo ya figo kama wagonjwa wengine wengi wa figo.
Karma iko wapi katika huu mtiririko wote wa maisha yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Karma Kwa Iddy Amin huioni!??
Alifanya Mapinduzi katika Serikali ya Milton Obote...

Baadae nae anaondolewa Madarakani na Obote anarudi madarakani...

Ts Simple as Simple

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimeona kwa ndugu yangu mmoja hiv, yeye ako na tabia ya kukopa na huwa halipi kwa makusudi kabisa, inafikia hata kwenye nyumba anazopanga halipi pango na baadae huwa anahama nyumba A kwenda nyumba B bila kulipa nyumba A, amekua akifanya hivyo kwa muda sasa na sio kama hana pesa la hasha, hela anayo lakini anafanya kwa kukusudia tu mwani anayo kazi ya kudumu kabisa serikalini ambapo anao uchumi wa kati. Sasa kinachotokea kwa maisha yake; ameuza vitu vyake vyote kuanzia gari hadi kitanda na mpaka sasa hana hata makazi.
Kwa hiyo naweza kukubali kweli karma ipo na inafanya kazi.
 
Gnassigbe Eyadema wa Togo alifanya mapinduzi mwaka 1963 na akaitwala Togo kwa takribani miaka 40 hadi alipofariki 2005 na mtoto wake Faure akarithi madaraka mpaka sasa,hiyo karma kwa nini haikufanya kazi kwake?
Gaddafi kuondolewa madarakani kwa mapinduzi ya umma ni karma iliyotokana na kumpindua mfalme Idris 1969?
Karma Kwa Iddy Amin huioni!??
Alifanya Mapinduzi katika Serikali ya Milton Obote...

Baadae nae anaondolewa Madarakani na Obote anarudi madarakani...

Ts Simple as Simple

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huwezi kujua inafanya kazi unajuaje ni karma? Kwa nini useme ni karma na sio matatizo tu kama yanayowapata watu wengine?
Swali langu ni je karma inaweza kuthibitika kutenda kazi kwa mtu?
Mkuu karma inafanya kazi kwa bahati mbaya sana inapofanya kazi watu hatujui including mwenyewe anayetafunwa na karma hajui, yaani anajiona yupo kawaida tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi wale wanaofanya hivyo na maisha yao yanaendelea kama kawaida,hawauzi vitu vyao na badala yake wanazidi kununua vingine?
Mimi nimeona kwa ndugu yangu mmoja hiv, yeye ako na tabia ya kukopa na huwa halipi kwa makusudi kabisa, inafikia hata kwenye nyumba anazopanga halipi pango na baadae huwa anahama nyumba A kwenda nyumba B bila kulipa nyumba A, amekua akifanya hivyo kwa muda sasa na sio kama hana pesa la hasha, hela anayo lakini anafanya kwa kukusudia tu mwani anayo kazi ya kudumu kabisa serikalini ambapo anao uchumi wa kati. Sasa kinachotokea kwa maisha yake; ameuza vitu vyake vyote kuanzia gari hadi kitanda na mpaka sasa hana hata makazi.
Kwa hiyo naweza kukubali kweli karma ipo na inafanya kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliofungwa bila makosa,wanaofanya kazi kwa bidii na kuishiwa kudhulumiwa,wanaopotea wanakuwa wamepanda nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watoto yatima wanaonewa, wengine wanazaliwa vilema, wengine afya zao dhaifu siku zote, kuna watu watafutaji sana ila hakuna kitu wanafanikiwa, KARMA kitu mbaya sana inafiri kutoka kizazi kimoja hadi kingine angalia maisha utakayowarithisha wanao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kama nilivyopata kufahamu kupitia maelezo mengi kuhusu Karma, Karma inaweza isimfikie muhusika katika muda wote wa uhai wake, lakini yenyewe itakuwepo na kufanya malipizi yake kwa vizazi vyake vilivyopo hadi pale deni litakapokwisha. Hivyo basi sisi wengine tunaishi kwa kulipa yale mazuri au mabaya waliyotenda wazazi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini vizazi vyake vilipishwe mambo ambayo havikutenda? Kanuni ya haki na hukumu si kila mtu anapaswa kuhukumiwa kwa yale aliyotenda tu!

Back
Top Bottom