GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,277
- 6,673
Dah, wakuu nimeamua kujiongeza kwa kufuga kanga, ni mradi mzuril lakini kwa changamoto ninayokutana nayo nimenyoosha mikono.
Nilimwekea kuku wa kwanza mayai 12 ya kanga akatotoa yote lakini wamepona 7 tu. Nikaendelea kuwawekea kuku wengine kwa kuchanganya mayai yao na ya kanga,
Mpaka sasa nina kanga wadogo wadogo 32.
Tatizo ninalolipata hapa ni hawa kanga 7 wakubwa, yaani hayo makelele siyo ya Dunia hii. Acha kabisa ndugu yangu yaani wanapiga makelele mpaka majirani wamekuja kunilalamikia, siyo majirani tu hata mimi mwenyewe nimechemka.
Sasa hawa 7 balaa limekuwa hili wakishafika 100 itakuwaje?
Nipeni uzoefu wafugaji wa Kanga huenda kukawa na namna ya kufanya kudhibiti kelele maana si mchana wala usiku kanga ana kelele tu!