Je, kampuni ikisajiliwa huhitaji leseni tofauti tofauti?

IPILIMO

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,823
2,000
Hello wana jamvi!

Kama Kamapuni imesajiliwa na yenye kujihusisha na shughuli mchanganyiko; mfano kusupply stationery, kusupply lubricants nk JE inatakiwa kuwa na leseni kwa kila shughuli? Kampuni ni ya kitaifa, leseni ni za mahali ambapo ofisi imewekwa mf. manispaa au jiji fulani. Je leseni ya biashara through out the year itakuwa ni ipi, inatolewa wapi? maana ukienda kufungua akaunti ya kampuni kwenye benki zetu wanasema lazima uwe na LESENI sasa ipi; ya stationery au ya lubricants? imenitokea mimi, nilienda halmashauri ya jiji, nikaomba kupatiwa maelezo ya kupata LESENI WAKANIULIZA kwa shughuli gani, nikwambia ni kampuni inayo deal na shughuli nyingi, wakasoma memorandum yangu wakasema kuna karibia business 13 tofauti, na kila moja LESENI YAKE kwakuwa kila moja ina ghrama yake!! nikashindwa kuelewa, nikaenda benki wakanambia sifungui akaunti bila leseni, nikawauliza leseni ngapi wakasema moja tu ya kampuni, na kwamba hawatarajii kuona kampuni ikawa na leseni nyingi!!

SO NATARAJIA KURUDI JIJI kuuliza vema, japo wagumu kutoa maelezo; kimsingi mimi naelewa kuwa inawezekana kweli kampuni moja ikafanya kazi nyingi tofauti tofauti, hivyo kuwa na gharama tofauti tofauti, kama ni KWELI leseni ziwe tofauti kadri ya shughuli za kampuni KWANINI mamlaka zisingeweka mfumo wa leseni moja kwa kadri ya usajili wa kampuni?
Naomba maelezo kwa wenye kuelewa zaidi juu ya hili, na hasa wale Maafisa Biashara wa halmashauri na kwingineko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom