Je, kama wewe ndiye mwenye gari utampa tena lifti mtu huyu?

Nilishampa mtu lift,mafuta yakakata,akashuka akapanda daladala nduki,ilikua ijumaa,Monday nikamkuta tena kituoni usafiri wa tabu kutoka kikijijini kuja town,akafanya kama ananichungulia ili nisimame,tukagongana macho,nikacheki kushoto kulia hamna gari ndukiii.
Hivi ndivyo inatakiwa,unyama unyamani.
 
Nitamuita kistaarabu na kumwambia twende zetu ili uwahi unakoenda maana chuma kimewaka baada ya kukiboost uliponiacha....

Akiwa na akili lazima aone aibu na kujifunza kwa kitendo hicho.
kwa heshima na taadhima naomba hii ndiyo iwe comment yangu
 
ETI?
Upo kituo cha daladala, usafiri ni mgumu, mara unamuona mtu unayemfahamu akiwa na gari lake... unampungia mkono kuomba lifti.
Anakupakia na safari inaendelea... mbele kidogo gari lake linazima, anashuka na kuhangaika nalo. Unashuka na kumwambia una haraka unamuacha hapo.
'Aisee ngoja nikuache mi' nna haraka zangu'
Unaenda kituo cha mbele na kusimama tena ukingoja basi kuwahi mambo yako. Humuulizi hata tatizo ni nini, husaidii hata kusukuma kidogo, wala humuagi kistaarabu kuwa inakulazimu kuwahi uendako.
Ukiwa umedoda tena hapo kituoni, ghafla unamuona aliyekupa lifti akija na gari lake. Kumbe limewaka!
Je, utaomba tena lifti?
Kama wewe ndiye mwenye gari utampa tena lifti mtu huyo?

Urahisi wa kuomba tena lifti na kupewa tena lifti unategemeana na namna ulivyoachana na mtu aliyepatwa na tatizo baada ya kukusaidia.
Wengi tunapoona mtu hana msaada tena kwetu, tunakata mawasiliano haraka sana, hatuonyeshi hata juhudi ndogo ya kutaka kusaidia, hatukumbuki fadhila, na tunasahau shida hazina mwisho.
Dunia hii inazunguka rafiki, katika namna ya ajabu sana unaweza kujikuta ukihitaji tena lifti ya mtu uliyepata kuona hana msaada tena kwako.
Jifunze kuagana na watu vizuri unapoona unatakiwa kuwa mbali nao. Pengine anaweza kuwa alikusaidia ukiwa chini na leo uko juu, unasahau hata kumjulia hali mara moja kwa mwaka kwa kuwa hana msaada tena kwako, yawezekana siku moja ukarudi chini kwa kasi na ukamhitaji mtu huyo huyo akusitiri tena.
Waswahili wanasema usinyee kambi!!
Unapoondoka mahali palipokusitiri, jitahidi kuondoka kwa amani iwe rahisi kwako kurudi. Usione kama hutomhitaji mtu tena, maisha huwa yanajua kutushushua kwelikweli!
Ila turudi kwenye swali utaomba tena lifti au utampa tena lifti baada ya yote .
Nimelipenda hili somo
 
Wakuu mie niliwahi kuachwa hivihivi na jamaa kwenye kapori ukitoka wilaya ya bukombe katikati kabla hujafika pale Mbogwe Mkoa wa Geita, jamaa nilimchukua nyakanazi na anaenda Nzega nilipofika kwenye kapori hako tair ikapata pancha nikashuka nipige jeck nibadilishe tairi wakati nahangaika jamaa akaniambia ana haraka hapo ni kama saa 4 usiku akaondoka mie nikabaki mwenyewe bahati nzuri jamaa mmoja nae kaja yupo peke yake kasimama kanisaidia kubadilisha tair tukaondoka tukapita kahama na mji wa kagongwa ndio tunaelekea isaka kumbe jamaa waliomchukua walikuwa wanaenda maeneo hayo wakamshsha mie nikafika akapiga mkono nikasimama kucheki ni abiria yuleyule nilichokifanya nikamwambia kama una 20000 elfu mpaka nzega twende kama huna baki alilia nami nikakomaa kanitoa kumi na tano ndio nikamchukua wakati nauli kutoka kahama to nzega ni elfu tano tu alisema hatarudia tena
Mnh me ningemwacha akikukabia humo ndani unaweza juta Kwanini ulimpakia tena
 
Siri ya mafanikio ni moja USIOMBE LIFT NA USITOE LIFT nadhan hii ni win win situation kwa wote
 
Unashangaa hivyo mkuu unakuta siku mmejikusanya na wana wikendi moja umejaa umetia wese kwenye Crown..mnaenda piga misele bahati mbaya ukagonga mtu aubgari lingine uharibifu umetokea hio siku ndo utajua wana hua wana cost sana...
 
unampa tu ishara ya dole la katikati kisha unakanyaga mafuta mengi,kuna siku natoka zangu koko bichi,wahindi sijui waarabu wanawake wamepata pancha wananiambia usenge wao sijui walijua ntaanza kuwahangaikia tairi lao,nikasepa zangu
 
ETI?
Upo kituo cha daladala, usafiri ni mgumu, mara unamuona mtu unayemfahamu akiwa na gari lake... unampungia mkono kuomba lifti.
Anakupakia na safari inaendelea... mbele kidogo gari lake linazima, anashuka na kuhangaika nalo. Unashuka na kumwambia una haraka unamuacha hapo.
'Aisee ngoja nikuache mi' nna haraka zangu'
Unaenda kituo cha mbele na kusimama tena ukingoja basi kuwahi mambo yako. Humuulizi hata tatizo ni nini, husaidii hata kusukuma kidogo, wala humuagi kistaarabu kuwa inakulazimu kuwahi uendako.
Ukiwa umedoda tena hapo kituoni, ghafla unamuona aliyekupa lifti akija na gari lake. Kumbe limewaka!
Je, utaomba tena lifti?
Kama wewe ndiye mwenye gari utampa tena lifti mtu huyo?

Urahisi wa kuomba tena lifti na kupewa tena lifti unategemeana na namna ulivyoachana na mtu aliyepatwa na tatizo baada ya kukusaidia.
Wengi tunapoona mtu hana msaada tena kwetu, tunakata mawasiliano haraka sana, hatuonyeshi hata juhudi ndogo ya kutaka kusaidia, hatukumbuki fadhila, na tunasahau shida hazina mwisho.
Dunia hii inazunguka rafiki, katika namna ya ajabu sana unaweza kujikuta ukihitaji tena lifti ya mtu uliyepata kuona hana msaada tena kwako.
Jifunze kuagana na watu vizuri unapoona unatakiwa kuwa mbali nao. Pengine anaweza kuwa alikusaidia ukiwa chini na leo uko juu, unasahau hata kumjulia hali mara moja kwa mwaka kwa kuwa hana msaada tena kwako, yawezekana siku moja ukarudi chini kwa kasi na ukamhitaji mtu huyo huyo akusitiri tena.
Waswahili wanasema usinyee kambi!!
Unapoondoka mahali palipokusitiri, jitahidi kuondoka kwa amani iwe rahisi kwako kurudi. Usione kama hutomhitaji mtu tena, maisha huwa yanajua kutushushua kwelikweli!
Ila turudi kwenye swali utaomba tena lifti au utampa tena lifti baada ya yote .
Jibu unalo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom