Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,439
ETI?
Upo kituo cha daladala, usafiri ni mgumu, mara unamuona mtu unayemfahamu akiwa na gari lake... unampungia mkono kuomba lifti.
Anakupakia na safari inaendelea... mbele kidogo gari lake linazima, anashuka na kuhangaika nalo. Unashuka na kumwambia una haraka unamuacha hapo.
'Aisee ngoja nikuache mi' nna haraka zangu'
Unaenda kituo cha mbele na kusimama tena ukingoja basi kuwahi mambo yako. Humuulizi hata tatizo ni nini, husaidii hata kusukuma kidogo, wala humuagi kistaarabu kuwa inakulazimu kuwahi uendako.
Ukiwa umedoda tena hapo kituoni, ghafla unamuona aliyekupa lifti akija na gari lake. Kumbe limewaka!
Je, utaomba tena lifti?
Kama wewe ndiye mwenye gari utampa tena lifti mtu huyo?
Urahisi wa kuomba tena lifti na kupewa tena lifti unategemeana na namna ulivyoachana na mtu aliyepatwa na tatizo baada ya kukusaidia.
Wengi tunapoona mtu hana msaada tena kwetu, tunakata mawasiliano haraka sana, hatuonyeshi hata juhudi ndogo ya kutaka kusaidia, hatukumbuki fadhila, na tunasahau shida hazina mwisho.
Dunia hii inazunguka rafiki, katika namna ya ajabu sana unaweza kujikuta ukihitaji tena lifti ya mtu uliyepata kuona hana msaada tena kwako.
Jifunze kuagana na watu vizuri unapoona unatakiwa kuwa mbali nao. Pengine anaweza kuwa alikusaidia ukiwa chini na leo uko juu, unasahau hata kumjulia hali mara moja kwa mwaka kwa kuwa hana msaada tena kwako, yawezekana siku moja ukarudi chini kwa kasi na ukamhitaji mtu huyo huyo akusitiri tena.
Waswahili wanasema usinyee kambi!!
Unapoondoka mahali palipokusitiri, jitahidi kuondoka kwa amani iwe rahisi kwako kurudi. Usione kama hutomhitaji mtu tena, maisha huwa yanajua kutushushua kwelikweli!
Ila turudi kwenye swali utaomba tena lifti au utampa tena lifti baada ya yote 😃😃😃.